Paskali naomba maelezo kwa hili

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
40,975
75,459
Nakuwekea maoni yako sometime back kuwa pesa za escrow siyo za umma. Leo una maoni gani. Nimesoma, you might be right. nakuomba ulifanyie kazi hili.


Wanabodi,

Kwa waliosoma fasihi, kitabu cha "An Enemy of the People" by Henrik Ibsen mnaweza kuniita mimi Paskali kuwa ni "an enemy of the people!", Fedha za Escrow, Sio Fedha za Umma!, hizo Bilioni 320 zilizokuwa kwenye account ya Escrow, hazijaibiwa!, bali zimetumika kulipia umeme! kwa kumlipa mfua umeme, IPTL, hivyo sio fedha za umma!.

Inawezekana PAP ni matapeli, na amenunua IPTL kitapeli, hivyo IPTL chini ya PAP ni kampuni hewa, amefanya utapeli kuinunua IPTL kitapeli, toka kwa wamiliki halali, hayo hayatuhusu, bali malipo ya Tanesco kwenye account ya escrow ni kulipia capacity charges ya mitambo ya IPTL ambayo ni mitambo kweli sio mitambo hewa!, na pia Tanesco inalipia malipo ya huduma za umeme ambao sio umeme hewa, bali ni umeme kweli unaokuwa generated na mitambo ya IPTL, na imeelezwa kuwa Tanesco bado inadaiwa!.Kwa lugha rahisi, hata baada ya PAP kulipwa fedha zilizoko ndani ya escrow account, bado Tanesco inadaiwa!.

Ukiwa mkweli sana wa type ya ukweli huu, pia lazima uwe tayari to pay the price!. Mimi ni mkweli wa kihivi, niko tayari to pay the price of expressing my opinion kuwa Nimesikitishwa!, Huzunishwa!, na Kufadhaishwa na Uongo wa Kamati ya PAC!-Escrow Sio Fedha za Umma!.

Paskali

Ufafanuzi unapatikana hapa kwa Mkuu Ng'wamapalala.
Hoja za Kamati ya PAC zinavyokinzana kuhusu Escrow akaunti kama ni fedha ya umma

Hoja za Kamati ya PAC zinavyokinzana kuhusu Escrow akaunti kama ni fedha ya umma

Kuna baadhi ya watu wanalijongea sakata ya IPTL huku wakiwa wametanguliza emotions badala ya fikra na mitazamo inayojenga hoja zenye maswali yaliyoko ndani ya hoja zilizoko mbele yetu.

Wakati akiwasilisha Taarifa ya Kamati kufuatia matokeo ya ukaguzi maalum wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa katika Benki Kuu ya Tanzania, Mhe. Zitto amenukuliwa akisema, maelezo yaliyotolewa na Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Kamishna Mkuu wa TRA na pia Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU yalidhihirisha kuwa sehemu ya pesa au pesa zote zilizokuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow zilikuwa ni pesa za Serikali.

Baada ya kuyapitia Maelezo ya CAG, TAKUKURU NA TRA nimegundua hayathibitishi kinagaubaga kama pesa zilizokuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow kama sehemu ya fedha au fedha zote zilikuwa ni fedha za umma.

Viongozi wa taasisi hizi katika matamshi yao wanaonekana hawana uhakika bali wanaongozwa na dhana ya kudhani ambayo kisheria haitoa majibu ya uhakika katika uharisia wake.

Ikumbukwe kuwa, Mhe. Zitto alinukuliwa akisema,

Mheshimiwa Spika,
wakati mahojiano ya Kamati na Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Kamishna Mkuu wa TRA pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU tarehe 19 Novemba, 2014 waliithibitishia Kamati kuwa kutokana na makubaliano wa Akaunti ya Tegeta ESCROW, sehemu ya fedha au fedha yote katika Akaunti hiyo ilikuwa ni fedha ya umma.

Katika mahojiano hayo, Maafisa hao walitamka yafuatayo kuhusiana na umiliki wa fedha za Akaunti ya Tegeta ESCROW:
Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
"&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG]; Kwa jinsi tulivyopitia fedha hii, tungesema ipo katika makundi matatu. Kundi la kwanza hiyo fedha ilikuwa na kodi ndani yake kwa hiyo tungesema kulikuwemo na fedha ya Serikali kwa maana ya kodi. Kwa upande mwingine, kwa sababu mpaka ESCROW inafunguliwa kulikuwa na dispute, kulikuwa na kutokubaliana juu ya charges, kwa hiyo kuna fedha ambayo inaweza ikawa ni ya TANESCO na kuna fedha ambayo inaweza kuwa ni ya IPTL &[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];"
Kamishna Mkuu wa TRA
"&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG]; TANESCO walitudhihirishia na kwa evidence kwamba katika kufanya yale malipo kwenye ESCROW Account walilipa pamoja na pesa ambayo ilitakiwa kulipwa kwetu ya VAT. Kwa hiyo, kulikuwa na VAT Component ambayo haikutakiwa kwenda kule &[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];"
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU
"&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG]; ninachoweza tu kusema na baada ya kusoma Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ni wazi kwamba pesa zilivyotoka TANESCO kwenda Benki Kuu bado kwa maoni yetu ni fedha za Serikali kwa sababu ni fedha ya TANESCO. Huo ndiyo mtazamo ambao tunao kiuchunguzi hadi wakati huu."

Kuna sentesi katika maelezo ya viongozi wa CAG, TRA na TAKUKURU ambazo zinaacha maswali mengi badala ya majibu.

Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anasema,
"&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG]; Kwa jinsi tulivyopitia fedha hii, tungesema ipo katika makundi matatu..''
Hoja hapa ni neno TUNGESEMA badala ya TUNASEMA/TUMESEMA. Kwa lugha nyingine, HAWAKUSEMA.

CAG anamalizia kwa kuonyesha hana uhakika kama kuna fedha ya umma au la katika Escrow akaunti.

Hoja ya msingi, Kwa nini CAG kusema, Jibu ni kwamba, CAG hakusema kwa sababu hana uhakika.

Kamishna Mkuu wa TRA katika kunukuliwa alisema,

"&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG]; TANESCO walitudhihirishia na kwa evidence kwamba katika kufanya yale malipo kwenye
ESCROW Account walilipa pamoja na pesa ambayo ilitakiwa kulipwa kwetu ya VAT..''

Hoja ya msingi hapa,

Neno ILITAKIWA KULIPWA kwa lugha nyingine HAIKULIPWA.

Swali la kujiuliza, Kwa nini TANESCO walipe pesa ya TRA kwenye Escrow akaunti badala ya kulipa TRA.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU yeye anadai bado wako kwenye uchunguzi lakini uchunguzi wao umejisimika kwenye maoni ya CAG, kwa lugha nyingine, TAKUKURU haijafikia uamuzi wa mwisho katika uchunguzi wake.

Hii dhana ya PAC ya kutoa hitimisho kama Tageta Escrow akaunti ilikuwa ni fedha za umma imetoka wapi wakati hata wachunguzi hawana uhakika?

NOTA BENE:
Haya maelezo nimetoa kwenye hotuba ya Mhe. Zitto ambayo iko HAPA

Tunaomba tueleweshane na kuelimisha katika mtazamo na fikra za kujenga na siyo kashfa na matusi.

Kitila Mkumbo said:

Pasco,

Kitila Mkumbo said:

1. unaomba tuelewashane wakati tayari umeshatoa hitimisho!!

2. Tangu mwanzo hata kabla ya PAC kuwasilisha kamati msimamo wa Kafulila umekuwa kwamba ndani ya akaunti ya ESCROW kuna fedha ya TANESCO (umma). Hakuna aliyewahi kusema kwamba pesa yote ni ya umma. Kumbuka kwamba hela yote imetokana na shauri mahakamani. Badala ya kuilipa IPTL pesa ilikuwa inakwenda kwenye hii akaunti hadi shauri lingeamuliwa ili kujua kiasi halisi ambacho IPTL walistahili.

3. Mahakama ikaamua kwamba ni kweli kwamba TANESCO walikuwa wanalipa pesa nyingi zaidi kuliko uhalisia.

4. Sisi tukapewa nafasi ya kukokotoa mahesabu ili tuchukue cha kwetu na kinachobaki kiende IPTL.

5. Tumeshindwa au tusema tumekaa kufanya hivyo kwa sababu hiyo pesa tulishaipiga, haipo. Ndio hizo akina Ruge wamezigawa kama njugu. Sasa utasemaje kwamba hakuna pesa yetu pale?.

6. Hata kitendo tu cha akina Ruge kugawa hela ovyo kinakwambia kwamba ile haikuwa pesa yao.

7. Katika hali ya kawaida kama ile ingekuwa pesa yao walioipata kihalali ingewezekanaje waigawe ovyo namna hiyo?

8. Matarajiri wa Tanzania ni Rostam, Bakhresa na Mengi, mbona hatujasikia wakigawana fedha bararani namni ile?.

9. Na kwa nini waliogawiwa wote ni wanasiasa, viongozi na watu wenye mamlaka fulani?

10. Kwa nini Ruge hakwenda kugawa hizi fedha kwa wanafunzi wetu waliokosa mikopo kama kweli ana roho nzuri kiasi hicho?.

11. Haya, wewe unaona ni sawa watu kugawana pesa kama maembe kama walivyofanya?

12. Nchi za wenzetu hata kuingia na dola 10,0000 wanakuzuia lazima utoe maelezo ya kutosha na vielelezo kibao. Hapa kwetu watu wanagawana pesa kwenye rambo wewe unaona ni sawa hiyo? Pasco please!!

Mkuu Mwalimu, Prof. Kitila, kwanza hongera kupata uprofesa, maana hatujakutana humu jukwaani kwenye thread yangu yoyote tangu umekuwa prof, bado nimekuzoea zaidi kama Dr. Pili nimefarijika sana, kunitembelea kwenye uzi huu, its an honor to me and to my thread, kama nilivyofarijika nilipo tembelewa na Mchambuzi na Nguruvi 3.

Kwenye posti yako ume raise hoja 12 za msingi, mwanafunzi unapoulizwa maswali na mwalimu, unaamini kabisa mwalimu anajua, ila anakuuliza tuu ili kuujua ufahamu wako, inapotokea mwalimu anaomba kueleweshwa na mwanafunzi, then mwanafunzi huyo anakuwa more than glad kumuelewesha mwalimu wake, na hapa mwanafunzi atajisikia sasa yeye ndio mwalimu, na mwalimu ndio mwanafunzi wake, hivyo Mwalimu Kitila, karibu katika darasa langu utulie kama mwanafunzi wangu!.

 1. Mimi ni mkweli daima hivyo mara kadhaa huanzia kwa kuweka "the end" na kisha ndipo na "justify the means". The end product hapa "pesa ni za nani?!", naanza kwenye kumtaja mwenye pesa ndipo tuje kuhalalisha kwa nini sio pesa za umma!. Kuna hoja za mijadala, na kuna hoja sio za mijadala ni straight forward, final na conclusive!. Ingekuwa hoja yangu ni mjadala, ningeuliza "Jee Fedha za Escrow ni za Umma?", ili watu walete michango, mwisho tufikie hitimisho kama niza umma au laa!. Hapa kuna ukweli na uongo!, kuna kuaminishana uongo kwa kudanganyana kuwa fedha za umma zimeibiwa!, zimechotwa, zimekapuliwa, hivyo wananchi wamehamanika, kuwa wanaibiwa, wakati ukweli ni kuwa fedha hazikuibiwa bali zimelipwa!. Mtindo wangu wa kutoa conclusive sikuanza leo, tulupoanza tuu huu mchakato wa katiba, nilisema tutapata "bora katiba". Kabla kura hazijapigwa kuipitisha nilisema humu "kura zisipotosha, zitatosheshwa!". Sasa watu wanapigia chapuo kura za hapana, nikasema wazi huko ni kujifurahisha kwa sababu kura za ndio "zitatosheshwa!", na kwenye siasa pia mara kibao nimeweka conclusive humu hata "2015 ni CCM tena!" kwa sababu hatuna any serious opposition, Ukawa mimi nauita ni just a "married of convenience!", conveniences zikiisha kila mtu atashika njia yake!. Escrow sio fedha za umma!.
 2. Hapa tuko wote, ndani pesa za account ya escrow zimechange forms mara tatu, au zime change hands mara tatu, kuna mtu anaitwa depositor, ambaye yeye ni Tanesco, fedha zilipokuwa mikononi mwa Tanesco, ndio zilikuwa fedha za umma, kitendo cha Tanesco kuzitoa ndani ya account ya Tanesco kuzi deposit kwenye escrow account, kumezichange form hizi fedha from kuwa pesa za umma, into pesa za depository, ambaye yeye ni custodian tuu wa fedha hizo hadi mgogoro utakapokwisha!, hivyo wakati fedha zikiwa kwenye safe custody ya custodian, escrow account chini ya BOT, fedha zile sii za umma wala sii za binafsi, some zingeweza kuwa za umma na kurudishwa Tanesco, some zingeweza kuwa za IPTL with a unique options ya possibility with "uncertainty" that "only some" "could" be fedha za umma, za Tanesco's, kutokana na overcharging, but with definite that some are IPTL's with possibility ya all the money ni za IPTL!. Ukijua ni nini kilichotokea kuhusu madai ya Tanesco na ni nini kilikubalika?!. Tanesco wali give in, na kukubali wanadaiwa more than kiwango kilichopo ndani ya escrow account, that na wakaweka schedule of repayment na ndipo Tanesco waka authorize pesa zote zilipwe kwa IPTL!, and that is when all the money zili change form kutoka kuwa fedha za wote na kugeuka fedha za binafsi, and during with drawer by the time fedha zinalipwa IPTL zilikuwa sio fedha za umma!.
 3. Ni kweli Tanesco ilikuwa overcharged hugely hivyo tulikuwa tunaibiwa!, ila wizi wenyewe ni kwa mujibu wa mkataba na tulikubali, kama tulivyokubali kununua radar, ndege ya rais, vifaa vya kijeshi na sasa bomba la gesi na mikataba ya gesi, nenda kanisome hapa Gesi asili: Is it "day light robbery?!"- watanzania tunaibiwa ...Tetesi: Bomba la Gesi Mtwara:A "20 -Year Grace Period" ni Kiini Macho!. Hivyo kama ni kuwa overcharged, kila siku tunakuwa overcharged, overpriced, na huge kick backs!.
 4. Nashukuru kuwa kumbe unajua tulipewa hii nafasi jee unajua tuliitumiaje?!. Hii ndio conversion process ya kuachia fedha za umma zilizoibiwa na kugeuka fedha binafsi!.
 5. Hatukushindwa!, this is where the deal is!, PCCB ni nothing!, Hosea is nothing!, kitu kinachoitwa usalama wa Taifa is nothing!, tangu mwanzo IPTL ni rushwa mwanzo mwisho, what did we do?!. Bodi ya Tanesco ilipata "ganzi!" ya ajabu!, wakaridhia kwa maandishi pesa zote ni za IPTL!. Ruge na Singasinga ni wapiga dili, kama pesa zilikuwa zetu, then kikulacho kii nguoni mwetu!, tusitafute mchawi!, wala tusimbebeshe msalaba mtoto wa Mkulima, wezi wetu tunawajua na ni wale wale toka Richmond, Dowans hadi Simbioni!. Tungekuwa na akili laiti mgelijua huyo Simba mwenye 50% ya PAP ndipo angalau mngenielewa!.
 6. "Mwenye kisu kikali ndiye anaekula nyama!", "fimbo iliyoko mkononi ndiyo uiwayo nyoka!", "the end justify the means!", "Aliyeshika usukani wa gari ndiye dereva" regardless gari ni la nani!, hivyo as long as pesa iko mikononi mwa JR as private money, what he does with his monies!, is non of our businesses!.
 7. Private money is none of our business!.
 8. Kumbe sasa tatizo ni kugawa?!, Ukimuondoa Bakhresa, please don't talk of Mengi and Rostam, kwao this is "missed opportunity!", masking JR angejivutia na kujinyamazia, haya yote yasinge fumka!. Siku zote wahindi wanapiga dili hizi na kujituliza tuli!, lakini masikini wakipata.... Kuna DCP walipiga wahindi watupu wakatulia haikubumburuka!, EPA wahindi walikuwa wanaipiga long time, huku wametulia, Waswahili walipoingia tuu, wanasafiri 1st class, wananunua Vogue custom made kutoka UK, wanasafirisha kwa air cargo, gari zinafika zina kuwa cleared by cash on the spot!, mtaani mbona tulikomaje?!, si ndio dili ikabumbuluka!, wangejinyamazia tuu kama walivyo wahindi yote haya yasingetokea!.
 9. As long as sio hela ya umma, haijalishi nani amegaiwa na kwa huduma gani, ndio maana nikasema PCCB is nothing!, mnaangalia waliogaiwa pesa, haya ni matokeo tuu!, mnaacha kuangalia chanzo cha jinamizi hili la IPTL na kila kitu kiko wazi!, Rutabanzibwa alikataa hongo ya dola 200 na akahamishwa!, unamjua waziri wake alikuwa nani?, kama KM alimegewa dola laki mbili, jee aliyekuwa waziri alipewa ngapi?, unamjua ni nani?. Pesa zikiisha kuwa zako, you are free kuzigawa utakavyo bila kuvunja sheria yoyote!. Hakuna sheria inayokataza kugawa pesa wala jinai yoyote kupokea pesa yoyote kwa kazi yoyote au hata bila kazi yoyote!. Hata mimi kuna wakati "huwapitia wale" na kukubaliana bei, then nikifika huko, ninachange mind, lakini bado nalipa mtu bila kufanya chochote, its my money!.
 10. When the money is yours, you are free to use it as you please!, kwa wingine, umasikini ni laana, hivyo badala ya kuwagawia maskini unamuomba Mungu, maskini wote bora wajifie tuu na umasikini wao, na kumfuatilishia Mungu kuwa mwenye nacho, ataongezewa!, asiye nacho atanyang'anywa hata kidogo alichonacho!, mzee wa vijisenti, kapewa katiba, ndiye mwenyekiti wa kamati ya bajeji na ndie mshauri wa JR wa mambo ya kisheria na umeona consultancy fee yake!.
 11. Yes ni sawa kabisa na amini usiamini, hata mimi Paskali nikiwa nazo, huwa nagawa!, tofauti ni kiwango, kwa uwezo wangu huwa nagawa ten ten, jelo jelo hadi buku buku!, kila nikienda bush, nahakikisha nina kama just 1.M tangu bank naiomba in small denominations, nikitua bush!, kijiji kizima kinajua leo mtoto wa mama fulani ameingia kijijini, kuanzia pombe hadi hizo ten ten, jero jero na buku buku, its my money, I do with whatever I wish that will please me!. Kwenye ule mgao kuna kick backs, kuna asante, kuna just sadakalawe kuwa "ninazo" kuna genuine charity na kuna sadaka!.
 12. Sio nchi za wenzetu hata sisi tunayo FIU pale BOT, miamala yote ya more than 10.m lazima taarifa ziende FIU ndio maana siku hizi hakuna kutoa malipo more than that bila kupitia BOT, the only exception ni same bank transactions ndio maana recipients wote walilazimishwa lazima wafungue account the same bank!. Nawaombeni sana msibabaishwe na huto tujisenti kwenye account za Mkombozi, the real transactions zimefanywa kwenye account yake iliyoko nchi Uholanzi, naamini "wanene" wamepewa asante zao zimehifadhiwa kule "Credit Sussie" transactions zinafanywa kwa "codes" only!, hata bank manageger, hawezi kujua jina la account holders!.
Natumaini mwalimu utakuwa umenielewa!.

Ni wako mwanafunzi mtiifu
 
Nakuwekea maoni yako sometime back kuwa pesa za escrow siyo za umma. Leo una maoni gani. Nimesoma, you might be right. nakuomba ulifanyie kazi hili.
Mkuu Retired , amini usiamini, hii ndio naiona leo!, japo imekuwa by passed by events , next time ukimuuliza mtu kitu, m tag ili ajue, akujibu.

I was very right kuhusu fedha za Escrow, Mzee JR ameonewa bure!, but imemcost mtu kulipa kwa the price of his life kupitia karma.

P
 
Mkuu Retired , amini usiamini, hii ndio naiona leo!, japo imekuwa by passed by events , next time ukimuuliza mtu kitu, m tag ili ajue, akujibu.

I was very right kuhusu fedha za Escrow, Mzee JR ameonewa bure!, but imemcost mtu kulipa kwa the price of his life kupitia karma.

P
Yule mshenzi alikuwa hapendi watu wenye akili kumzidi na watu wenye fedha kumzidi. But Karma never loses location, ikamtandika Mwendazake
 
Back
Top Bottom