Kumbe Hayati Rais Magufuli alikuwa Mwamba kweli kweli!! Taifa hili litakukumbuka daima!!!

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
946
1,000
Hivi karibuni nilitoa maoni yangu kupitia humu Jamiiforums kuhusu Waziri wa Nishati January Makamba na mienendo yake kuhusu TANESCO.

Kama anavyosema Jenerali Ulimwengu yawezekana kweli Tanzania ni Nchi ya ajabu kweli kweli!

Hayati Rais Magufuli amefariki hata mwaka mmoja haujaisha hofu kuhusu hali ya umeme kuwa mbaya imetanda kila mahali!

Nili-doubt mapema sana iweje huyu January Makamba kuapishwa tu kuwa Waziri wa Nishati ,hajatembelea hata miradi kama Stiglers Gorge keshakimbilia Ubalozi wa Marekani kuomba misaada ya umeme!!!

Muda mfupi Waziri aliyekuwepo wa Nishati Medard Kalemani akatenguliwa, MD wa TANESCO Dr.Tito Mwinuka akaondolewa na Bodi ya TANESCO ikavunjiliwa mbali.

Sasa kwa Nchi yenye viongozi makini hapo succession plan iko wapi?

Waziri mpya, MD wa TANESCO mpya ( tena mwenye uzoefu wa usambazaji visimbuzi siyo insider wa TANESCO) na Bodi pia mpya yenye wajuumbe wapya na wengine walikuwa watetezi wa akina Richmond na Dowans katika kesi za upigaji ktk TANESCO katika Mahakama za Kimataifa! Nchi yetu kweli ya ajabu sana hii!

Eti leo January kupitia makuwadi wake kama akina Zitto Kabwe wanamtuhumu Hayati Rais Magufuli kuwa alinyima au kataza matengenezo katika mitambo ya Umeme na wakati mwingine kuwa maneuver wenye viwanda kusitisha uzalishaji ili kuficha mgao wa umeme!!!

Kweli Zitto Kabwe anadhihirisha ninachokijua siku zote kuwa usimwamini mwanasiasa yeyote mwenye njaa!

Yaani Zitto Kabwe kukosa Ubunge na kukosa mishahara na posho za kibunge kwa mwaka mmoja tu umekuwa " Kichwa maji" hivi na kuanza kuwa kuwadi wa January Makamba kwenye matatizo ya kutengeneza ya Umeme !!

Ukisoma tweet za January ambazo hazina hadhi ya Uwaziri na tweet za Zitto zote zina mwelekeo mmoja wa kumbeza na kumlaumu Hayati Rais Magufuli kuhusu hali hii ya umeme wanayotutishia!

Watanzania hata msemeje na makuwadi wenu tunajua Hayati Rais Magufuli alikomesha ujinga ujinga uliokuwa ukifanyika TANESCO! Mliifanya TANESCO " Cash Cow" yenu and now you are back in another form after the demise of Magufuli!

Ukiwasikiliza TANESCO na January kuna mambo mawili wanayo fabricate kama chanzo cha tatizo la umeme!

Mosi ni Matengenezo (Maintenance) na pili Ukame!

Mimi ninachosema wote hawana hoja , akina January waende moja kwa moja kwenye point na wasizunguke na kufanya watu wote ni wajinga!!!

Wanachotaka hawa mumiani ni kuwarudisha akina Symbion na IPTL kwenye kazi/mikataba baada ya kifo cha Hayati Rais Magufuli!!

Wanajificha kwenye maeneo haya mawili,matengenezo na ukame, ili Mwenyezi Mungu akiwaumbua kwa kunyesha mvua basi wabaki na ajenda ya upungufu wa umeme ni kutokana na uchakavu wa mitambo na matengenezo!

Kama hali ni mbaya kiasi hiki nauliza Kamati Kuu ya CCM na NEC huwa kunajadiliwa nini kiasi cha mambo ya msingi kama haya kuzuka na kuleta hofu kwa wananchi na hakuna mwongozo wowote wa maana kutoka katika Chama?!

CCM kama tumeshindwa kuongoza Taifa hili kwa ufanisi TUKUBALI na turuhusu ushindani wa kisiasa ili kupitia ushindani huo wanaweza kupatikani watu wengine wenye maarifa wakaliongoza Taifa hili kwa mafanikio makubwa kuliko haya tuliyo nayo leo !
 

DATAZ

JF-Expert Member
May 25, 2012
1,482
2,000
Huyo ndio amaetufikisha hapa. Angekamilisha ule mradi wa umeme wa gesi kwanza, huenda Leo tusingekuwa hapa. Lakini kwa kuwa alijawa visasi aliona kila alichofanya Kikwete akiharibu na kujimwambafai hakuna mwenye mipango mizuri Kama yeye.

Tuendelee kula giza Hadi hapo mvua itakapotumbuka kwa ujinga wetu
 

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
946
1,000
Huyo ndio amaetufikisha hapa. Angekamilisha ule mradi wa umeme wa gesi kwanza, huenda Leo tusingekuwa hapa. Lakini kwa kuwa alijawa visasi aliona kila alichofanya Kikwete akiharibu na kujimwambafai hakuna mwenye mipango mizuri Kama yeye.

Tuendelee kula giza Hadi hapo mvua itakapotumbuka kwa ujinga wetu
Alikuta gesi ishapigwa mnada kwa hati za dharura bungeni na gesi ingezalishwa bei yake tusingeiweza! Tafuta taarifa !
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
16,497
2,000
... taifa halihitaji miamba; linahitaji watu wenye akili za kutuvusha kutupeleka mbele wote kama taifa. Linahitaji viongozi wenye mission na vision ya leo, kesho, na miaka mingi ijayo hata baada ya wao kuondoka. Halihitaji Master Plans za miaka 5, 10, 25, au hata 50 zilizolundikwa kwenye makabati; linahitaji Master Plans zinazotekelezeka.

Hayo hayawezekani kwa kujenga personalities badala ya mifumo imara na mifumo imara huanza na Katiba bora. Unaposikia kauli kama rais ametoa; rais amekubali; rais ameridhia; rais ame....; rais ame .... hizo ni indicators za kujenga personalities badala ya mifumo; ni dalili mifumo ni dhaifu na wanasiasa wako juu ya mifumo ya taifa hilo! Na taifa la aina hiyo; taifa linalotegemea "hisani" ya rais au viongozi haliwezi kupiga hatua!
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
112,190
2,000
Huyo ndio amaetufikisha hapa. Angekamilisha ule mradi wa umeme wa gesi kwanza, huenda Leo tusingekuwa hapa. Lakini kwa kuwa alijawa visasi aliona kila alichofanya Kikwete akiharibu na kujimwambafai hakuna mwenye mipango mizuri Kama yeye.

Tuendelee kula giza Hadi hapo mvua itakapotumbuka kwa ujinga wetu
Ikitokea mvua hainyeshi itakuwaje mkuu?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom