Hivi inakuwaje mwanamke uliye kwenye ndoa yako uingie ndani saa saba usiku?

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Kama huyu mtu angemfungulia mkewe mlango muda huu, (1:17am), hapo ningeamini ule msemo wa wanazengo kuwa kawekewa Limbwata

Yaani mwanamke timamu, unamuacha mumeo saa nne usiku wakati tayari mlikuwa mmekwishapanda kitandani, unashawishika na mshika masikio mwenzio, mnaambatana kwenda kwa jirani kwa kile mnachokiita Friday Party. Kwa dharau unalewa mpaka saa 7 hii, halafu unabaki ukilalama eti nilikuwa chumba cha jirani hapo pua na mdomo. Halafu unalalama eti mume anadharau, hataki kukufungulia mlango, saaaaad!

Alivyo kiburi karudi kwa rafiki yake kulala, yaani karudi kwenye party Halafu kwenye party yenyewe kuna madume wawili, mmoja bachela, mwingine hana time na familia, halafu wote unaambiwa ni wachakataji holela. Anyway hayo mengine tuyaache, turudi kwa huyu mwanamke

Hivi huu ni uungwana kweli? Mumeo katoka kazini, kachoka, kakuemelea kila kitu mpaka vya kesho chaini. Karudi akiwa amejaa upwiru, wewe unamuacha unakwenda kwenye soga. Inasikitisha sana

Siku mkisikia Bwana Melki anatangaza ndoa na Bi Dazeti Mweusi kutoka Mkulanga, naombeni mnikate mashine

Inasikitisha, badilikeni! Nitawaletea mrejesho wa kilichoendelea itakapitimu asubuhi
 
As long as Mwanaume ni POYOYO , mwanamke ,si tu kurudi saa Saba, atalala hukohuko alafu Kisha utaona wa saa Saba ana unafuu
 
Kama huyu mtu angemfungulia mkewe mlango muda huu, (1:17am), hapo ningeamini ule msemo wa wanazengo kuwa kawekewa Limbwata

Yaani mwanamke timamu, unamuacha mumeo saa nne usiku wakati tayari mlikuwa mmekwishapanda kitandani, unashawishika na mshika masikio mwenzio, mnaambatana kwenda kwa jirani kwa kile mnachokiita Friday Party. Kwa dharau unalewa mpaka saa 7 hii, halafu unabaki ukilalama eti nilikuwa chumba cha jirani hapo pua na mdomo. Halafu unalalama eti mume anadharau, hataki kukufungulia mlango, saaaaad!

Alivyo kiburi karudi kwa rafiki yake kulala, yaani karudi kwenye party Halafu kwenye party yenyewe kuna madume wawili, mmoja bachela, mwingine hana time na familia, halafu wote unaambiwa ni wachakataji holela. Anyway hayo mengine tuyaache, turudi kwa huyu mwanamke

Hivi huu ni uungwana kweli? Mumeo katoka kazini, kachoka, kakuemelea kila kitu mpaka vya kesho chaini. Karudi akiwa amejaa upwiru, wewe unamuacha unakwenda kwenye soga. Inasikitisha sana

Siku mkisikia Bwana Melki anatangaza ndoa na Bi Dazeti Mweusi kutoka Mkulanga, naombeni mnikate mashine

Inasikitisha, badilikeni! Nitawaletea mrejesho wa kilichoendelea itakapitimu asubuhi
Mawili mke hana adabu au mume hana msimamo. Mke kurudi nyumbani mwisho saa 8 usiku tena akiwa na kazi, zaidi ya hapo atafite pa kulala.
Huyo hana adabu kabisa. Mm ningekuwa jamaa ngekuta mabegi mlangoni
 
uku na uku kumbe mleta mada anazungumzia ivi videm vya kuvaa kobasi za manyoya na vimenyoa kiduku na kupaka rangi kichwani
20240307_170627.jpg
 
Pole sanaa lala tu mkuu.
Usija ua jela ikakukalia wanawake wako wengi tu..
Ila acheni kuoa walevi.
Sio mimi mkuu, ni mke wa jirani yangu hapa. Mimi sikupatw usingizi kutokana na kelele za huo muziki hivyo nilibaki nahesabu maua ya pazia

Baada ya hilo zondo ndo nikaamua kuandika uzi, maake nilisikia kila kitu, nikavaa kiatu cha jamaa
 
Back
Top Bottom