Hivi mtanzania bara unaweza kuomba uraia wa Zanzibar?.

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Kuna hii ishu ya watu wa bara kutoruhusiwa kumiliki ardhi Zanzibar. Je mtu wa bara anaweza kuomba uraia ili awe na haki kama mzanzibari mkazi?
 
Uzanzibar sio uraia ni uzawa tu au kama kabila vile. Wazanzibar ni Watanzania kiurai.. kuhusu kuomba Uzanzibar sijui
 
Uzanzibar sio uraia ni uzawa tu au kama kabila vile. Wazanzibar ni Watanzania kiurai.. kuhusu kuomba Uzanzibar sijui
Kusema ni kama kabila nakataa. kama ni mtanzania na hauna kusajili wa mzanzibari mkaazi kuna haki huwezi kuwa nazo Zanzibar.
 
Mm Nina ardhi na ni mtanzania bara na Sina kitambulisho Cha ukazi....watu wanawatafsiri vibaya wazanzibar.
 
Kuna hii ishu ya watu wa bara kutoruhusiwa kumiliki ardhi Zanzibar. Je mtu wa bara anaweza kuomba uraia ili awe na haki kama mzanzibari mkazi?
Umechanganya madawa! Uraia vs Ukaazi. Tanzania haina raia wa aina mbili. Wazanzibar na wabara wote ni watanzania. Kama unataka kuruhusiwa kumiliki ardhi Zanzibar basi unatakiwa kutimiza masharti ya kuwa mkaazi wa Zanzibar! Hizi ni moja ya sheria tata za muungano wetu lakini madhali zipo basi zifuatwe au zibadilishwe.
 
Wanacheza tu na lugha na technicalities za sheria. Kama mimi ni mtanzania na mzanzibari ni mtanzania. Na katibu inasema nina haki ya kwenda na kuishi kokote ikiwa nipamoja na kumiliki mali iweje nizuiliwe zanzibar?
Kitambulisho cha ukaazi ni uhuni wa lugha tu ila ni kitambulisho cha uraia wa zanzibar ukichukulia wenyewe wanasema Zanzibar ni nchi.
 
Mimi ni Mkenya ila nimewahi kuishi Zanzibar, kuna siku jamaa yangu wa kutokea Bara alihitaji kadi ya uraia ya Zanzibar, akapewa masharti kwamba lazima awe ameishi zaidi ya miaka mitano ndio aruhusiwe.
Japo suala la kununua ardhi ni tofauti maana kuna hata wageni nje ya nchi wasio hata Watanzania na wanamiliki ardhi. Kuna Waarabu wa Oman pia wazungu wengi tu wamejenga nyumba zao huko.
 
Back
Top Bottom