Hivi Msumbiji na Comoro si waachane na Kireno na kifaransa tu?

Ku-master lugha tatu nne au tano ni bora kuliko moja au mbili; badala ya kuwaambia waache hii au ile ni bora waongeze nyingine na nyingine...., ni nyenzo za ziada katika mawasiliano
 
Nchi zinazoongea kireno Afrika ni tano
1. Angola
2. Cape verde
3. Guiné Bissau
4. Msumbiji
5. São Tomé e príncipe
Wana umoja wao na wanaelewana na hali zao
Nalog off
 
..Lugha ni kingereza tu bhana hizo nyingine kifaransa, kireno, kijerumani sijui kispaniola ni lugha za ajabu tu nashangaa mnaopoteza muda kujifunza hizo lugha sioni faida kwakweli bora ujifunze kichina kitakusaidia sio hizo lugha za hovyo
Mtumwa wa fikra
 
Hivi Msumbiji na Comoro si waachane na Kireno na kifaransa tu?

Kuna nchi nyingine ni za hovyo kweli?Hivi hao Wasumbiji kwanini wasiachane na kireno?Ureno yenyewe wapo hoi sikuhizi kingereza ndo lugha inafanya vyema ureno kuliko hata lugha yao

Lakini msumbiji wanaendelea kuwa nchi ya hovyo kwa kung'ang'ana na kireno

Wangefanya kingereza na kiswahili kiwe lugha kuu ya taifa waachane na huo ujinga unaoitwa kireno hivi jamani kireno kitakupeleka wapi tuseme ile kweli

Tumeshindwa kuchanganyika na kufanya maingiliano sana na wamsumbiji kwasababu ya kireno chao, lakini angalia tulivyo na maingiliano na rwanda, kenya,burundi, uganda kwasababu wanaongea lugha zinazoeleweka hawa watu wa msumbiji na.Comoro tunashindwa kwasababu ya malugha yao ya hovyo

Ukija.Comoro hawa ndo tulipaswa tuwe nao kabisa tena ikiwezekana tuungane nao na kuwavuta kama tulivyovuta ZANZIBAR kwanza tunafanana nao sana ila uchawi ni hicho kifaransa chao...wakati wenzao wanakimbilia kwenye kingereza na kukiacha kifaransa kama walivyofanya Rwanda na nchi nyingine wao wanazidi kujikomaza na hicho kifaransa chao.....Lugha ni kingereza tu bhana hizo nyingine kifaransa, kireno, kijerumani sijui kispaniola ni lugha za ajabu tu nashangaa mnaopoteza muda kujifunza hizo lugha sioni faida kwakweli bora ujifunze kichina kitakusaidia sio hizo lugha za hovyo
Hivi mleta maada ulifikiria nini mpaka kuandika huu upuuzi? Unajua maana lugha? Inachukua miaka mingapi mpaka iweze kuongelewa na wahusika,

mwaka 1498 Vasco dagama ndiyo alikuwa anaingia Msumbiji kwa mara ya kwanza, jiulize wewe unayetukana lugha za watu babu zako walikuwa wapi ndiyo utajijibu,

Mozambique walizindua bwawa la umeme wa maji mwaka 1905 linaitwa kabora basa, wewe unayeongea kiswahili babu zako walikuwa wanapigana vita vya majimaji,

askari wa Tanzani wanapokuja kuwasaidia kupigana vita vya ukombozi wa uhuru, waliwakuta kunaViwanda vya watu binafsi majumbani mwao,
Maputo au Rolenco marcus kipindi hicho ilikuwa na mvuto kuliko johnsburg, ngoja niishie hapa usilolijua sawa na usiku wa giza
 
Hata sisi na hili likiswahili letu ni ujinga mkubwa sana kuling'ang'ania

Tena huwa napata hasira sana nikisikia mtu anasema sijui kiswahili kimekuwa sijui tujivunie lugha yetu,sijui nini
Ungejua wazungu wanashangaa sana sisi kuwa na lugha yetu ya kiswahili na siyo lugha ya kikoloni, wanafunzi wengi kutoka Ulaya wanakuja Tanzania kujifunza lugha ya kiswahili ndugu yangu tembea utajifunza mambo mengi kuhusu jamii za nje zinavyo ipenda lugha yetu, kule Zanzibar kuna shule ya kimataifa ya kufundisha lugha ya kiswahili inaitwa Adventure, wanafunzi wanatokea Ulaya.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Kiswahili ni asili yetu na kimetusaidia sana kwenye utengamano wa kitaifa. Hakijaletwa na mkoloni kakisaidia kukua na kusambaa, hizo lugha nyingine sio zetu na kuzitumia kama kisingizio cha kutopata maendeleo ni uongo. Wachina, Wajapan, Wakorea wanaongea lugha zao nchi moja tu na lugha yake na wametoboa sisi hata kuunda chupa ya chai hatuwezi.
Huyo hawezi kujua umuhimu wa lugha yetu na hawezi kujua kama lugha yetu inapendwa sana na wageni na wageni wanapenda sana kuijua, huyo anatakiwa atambee ili apate marafiki kutoka nchi za Ulaya ndiyo atakuja kujua kiswahili kina heshima kiasi gani, lakin kama anaishi na jamii ya aina moja hawezi kujua kiswahili kina sambaa kwa ukubwa gani kwasababu rafiki zake wote ni jamii ya kiswahili.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna lugha bora kuliko ingine ikiwa kila lugha inakidhi matakwa ya kimawasiliano ya watumiaji wake.

Ikiwa Kimang'ati kinakidhi matakwa ya kimawasiliano ya Wamang'ati,
ni lugha muhimu kwa watumiaji wake.
Natamani kila mtu angeelewa mantiki ya hii comment yako. Bahati mbaya wengine hawawezi kuelewa.
 
Kuendelea kuzifanya official rugha za walio watawara nikuendelea kuutukuza kuukubari nakuuheshimu utawara wao huu niupuuzi mwingine wa watu weusi
 
Ungejua wazungu wanashangaa sana sisi kuwa na lugha yetu ya kiswahili na siyo lugha ya kikoloni, wanafunzi wengi kutoka Ulaya wanakuja Tanzania kujifunza lugha ya kiswahili ndugu yangu tembea utajifunza mambo mengi kuhusu jamii za nje zinavyo ipenda lugha yetu, kule Zanzibar kuna shule ya kimataifa ya kufundisha lugha ya kiswahili inaitwa Adventure, wanafunzi wanatokea Ulaya.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
Unaniandikia yale yale ambayo sitaki kuyaona na kuyasikia,hii lugha haina faida ni hasara tu kwa taifa hili
 
Hivi mleta maada ulifikiria nini mpaka kuandika huu upuuzi? Unajua maana lugha? Inachukua miaka mingapi mpaka iweze kuongelewa na wahusika,

mwaka 1498 Vasco dagama ndiyo alikuwa anaingia Msumbiji kwa mara ya kwanza, jiulize wewe unayetukana lugha za watu babu zako walikuwa wapi ndiyo utajijibu,

Mozambique walizindua bwawa la umeme wa maji mwaka 1905 linaitwa kabora basa, wewe unayeongea kiswahili babu zako walikuwa wanapigana vita vya majimaji,

askari wa Tanzani wanapokuja kuwasaidia kupigana vita vya ukombozi wa uhuru, waliwakuta kunaViwanda vya watu binafsi majumbani mwao,
Maputo au Rolenco marcus kipindi hicho ilikuwa na mvuto kuliko johnsburg, ngoja niishie hapa usilolijua sawa na usiku wa giza
Waliojenga ni wazawa au mabeberu wa kireno?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom