Hivi Msumbiji na Comoro si waachane na Kireno na kifaransa tu?

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Hivi Msumbiji na Comoro si waachane na Kireno na kifaransa tu?

Kuna nchi nyingine ni za hovyo kweli?Hivi hao Wasumbiji kwanini wasiachane na kireno?Ureno yenyewe wapo hoi sikuhizi kingereza ndo lugha inafanya vyema ureno kuliko hata lugha yao

Lakini msumbiji wanaendelea kuwa nchi ya hovyo kwa kung'ang'ana na kireno

Wangefanya kingereza na kiswahili kiwe lugha kuu ya taifa waachane na huo ujinga unaoitwa kireno hivi jamani kireno kitakupeleka wapi tuseme ile kweli

Tumeshindwa kuchanganyika na kufanya maingiliano sana na wamsumbiji kwasababu ya kireno chao, lakini angalia tulivyo na maingiliano na rwanda, kenya,burundi, uganda kwasababu wanaongea lugha zinazoeleweka hawa watu wa msumbiji na.Comoro tunashindwa kwasababu ya malugha yao ya hovyo

Ukija.Comoro hawa ndo tulipaswa tuwe nao kabisa tena ikiwezekana tuungane nao na kuwavuta kama tulivyovuta ZANZIBAR kwanza tunafanana nao sana ila uchawi ni hicho kifaransa chao...wakati wenzao wanakimbilia kwenye kingereza na kukiacha kifaransa kama walivyofanya Rwanda na nchi nyingine wao wanazidi kujikomaza na hicho kifaransa chao.....Lugha ni kingereza tu bhana hizo nyingine kifaransa, kireno, kijerumani sijui kispaniola ni lugha za ajabu tu nashangaa mnaopoteza muda kujifunza hizo lugha sioni faida kwakweli bora ujifunze kichina kitakusaidia sio hizo lugha za hovyo
 
Hata sisi na hili likiswahili letu ni ujinga mkubwa sana kuling'ang'ania

Tena huwa napata hasira sana nikisikia mtu anasema sijui kiswahili kimekuwa sijui tujivunie lugha yetu,sijui nini
Kiswahili ni asili yetu na kimetusaidia sana kwenye utengamano wa kitaifa. Hakijaletwa na mkoloni kakisaidia kukua na kusambaa, hizo lugha nyingine sio zetu na kuzitumia kama kisingizio cha kutopata maendeleo ni uongo. Wachina, Wajapan, Wakorea wanaongea lugha zao nchi moja tu na lugha yake na wametoboa sisi hata kuunda chupa ya chai hatuwezi.
 
Hata sisi na hili likiswahili letu ni ujinga mkubwa sana kuling'ang'ania

Tena huwa napata hasira sana nikisikia mtu anasema sijui kiswahili kimekuwa sijui tujivunie lugha yetu,sijui nini
Naunga mkono hoja

Nikikikumbuka kipindi kile Airtel wameanzish yale mashindano ya vyuo vya Afrika Mashariki

Watanzania tulikuwa tunapelekeshwa aisee dah

Piga chini kishwahili,weka juu kiingereza
 
Hakuna lugha bora kuliko ingine ikiwa kila lugha inakidhi matakwa ya kimawasiliano ya watumiaji wake.

Ikiwa Kimang'ati kinakidhi matakwa ya kimawasiliano ya Wamang'ati,
ni lugha muhimu kwa watumiaji wake.
Kimang'ati kibaki majumbani Kwa wamang'ati,ila katika ngazi ya kitaifa na kikanda hakuna namna,kiingereza ndo njia ya kututoa
 
Kiswahili ni asili yetu na kimetusaidia sana kwenye utengamano wa kitaifa. Hakijaletwa na mkoloni kakisaidia kukua na kusambaa, hizo lugha nyingine sio zetu na kuzitumia kama kisingizio cha kutopata maendeleo ni uongo. Wachina, Wajapan, Wakorea wanaongea lugha zao nchi moja tu na lugha yake na wametoboa sisi hata kuunda chupa ya chai hatuwezi.
Jidanganye
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom