Perry
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 10,082
- 2,358
Wakuu,kuna jambo linanitatza..kuna binti mmoja namfukuzia hapa chuo,huyu binti niseme tu kuwa yeye ndie aliyechochea hadi mie kuanza kumfukuzia kwa sababu kabla ya yote nilikua namchukulia kama binti wa kawaida tu ambapo tulikua tunaweza tukapishana mahali hata bila kusemeshana wala kusalimiana,sasa ilitokea tukawa tumepangwa seminar moja{kwa wale mliopitia vyuo vikuu mtakua mnanielewa}tangu hapo akawa kila nikikutana nae njiani ananisalimia fresh tu,asa me nikaona nijaribu kumpiga sound kama kujaribu bahati yangu tu,kuna siku nikakutana nae angle flani tukiwa tunasubiri kipindi,nikamwomba number zake,nae bila hiyana akanipa,tukawa tumekubaliana kuwa jioni ya siku hiyo mara baada ya muda wa masomo kuisha nitamtafuta tukutane mahali,well,muda ulivofika nikamcoll kumkumbushia kuhusu miadi yetu,alipokuja nikampiga sound nae akawa amenielewa,lakin akawa ananiambia kua,yeye hana mtu but vile vile haitaji kuwa na mtu tena kwa sasa,katika kutaka kumdadis zaidi,akawa mkali,me nkaona isiwe tabu,nikamwambia basi ka vipi tuwe marafiki wa kawaida tu,sasa tangu pale huyu mmanzi ananishangaza,nikimpigia cmu anapokea na kuongea vizuri tu,nikimwambia tuonane muda wowote yuko tayari but nikimkumbushia ombi langu anabadilika na kusema tuyaache hayo coz moyo wake haujaamua kumpenda mwanaume yeyote tena..nikimtext message zinazohusu mambo mengne ya kimaisha anajibu ila zile zinazohusu mapenzi huwa hajibu..ebu wakuu nisaidieni kumdadavua huyu binti,kwamba ni binti wa namna gani na anaitaji kufanyiwa kitu gani ili kuweza kuwin her heart?