Hivi mbunge kama huyu anafaa kuwa mbunge?

Chatumkali

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
2,037
458
Kituo cha TV cha TBC1 kimeonyesha shule ya msingi ya ajabu katika taarifa ya habari ya saa mbil usiku.Shule hiyo iliyopo mkoani Rukwa ina hali mbaya sana.

Watoto wamekaa kwenye mawe na magogo ya miti!Wlimu wanafundisha kwenye kipande cha bati kama ndio ubao!Madarasa yamejengwa kwa kuta za nyasi.

Cha kusikitisha mbunge wa eneo husika (jina sikulidaka vizuri) anamlaumu diwani wa eneo husika kwamba eti anafanya kazi gani! Halafu anasisitiza kwamba yeye binafsi hajawahi kuona shule kama hiyo katika maisha yake! Sasa yeye kama mbunge anafanya kazi gani?

Bungeni anamuwakilisha nani kama shule iliyopo ndani ya jimbo lake haijui? Ina maana wakati anapita huko kuomba kura hakuiona hiyo shule kituko? Hivi mbunge kama huyu anafaa kuwa mwakilishi wa watu kweli?

INASIKITISHA SANA!
 
Lawama ziende kwa serikali dhalimu ya CCM na siyo huyo mbunge ambaye kazi yake ni kuikumbusha serikali tu.

Kaka nakusalimu sana,
Huyo mbunge ni amenichekesha kweli leo. Hata sura yake ilikuwa inaonyesha hayupo serious na alichokuwa anajaribu kukipigia kelele
 
Mwita asante mkuu naona limbwata la ccm linaisha sasa. bado yule bi mkubwa
 
Majibu kama haya toka kwa viongozi wa ccm tumeyazoea kama JK mwenyewe anaulizwa kwanini nchi yako masikini anasema hata yeye hajui unategemea wabunge na madiwani wake watakua je?
 
Si maeneo yote ambayo wabunge wanafanikiwa kupita, Diwani anapaswa kuripoti kwa Mbunge then mbunge alipeleke serikalini. Mbunge ana haki ya kumlaumu Diwani.
 
Serikali ndiyo wana majukumu ya kujenga shule sababu wao ndiyo wakusanyaji kodi zetu..

Mbunge wala diwani hawana fungu lolote lakujenga shule
 
Lawama ziende kwa serikali dhalimu ya CCM na siyo huyo mbunge ambaye kazi yake ni kuikumbusha serikali tu.
Duh!!kweli Mungu mkubwa sana,nahisi leo umefunuliwa ufunuo wa yohana!!!!!!PAMOJA SANA MKUBWA!!!Tuungane pamoja kutetea maslahi ya taifa letu kwa maendeleo yetu
 
aliyewaambia mwita25 amezinduka kwa kuiponda CCM ni nani? huo ni sehemu wa mpango mkakati ili tuisambaratishe CHADEMA
 
Serikali ndiyo wana majukumu ya kujenga shule sababu wao ndiyo wakusanyaji kodi zetu..

Mbunge wala diwani hawana fungu lolote lakujenga shule

Hoja sio fungu mkuu!Hoja yeye kama kiungo kati ya serikali na wananchi anafanya nini ili matakwa ya wananchi yafike serikarini?Vinginevvyo basi kwa mtizamo wako tuseme hakuna haja ya kuwa na wabunge basi maana hawana maana yeyote!
 
Serikali ndiyo wana majukumu ya kujenga shule sababu wao ndiyo wakusanyaji kodi zetu..

Mbunge wala diwani hawana fungu lolote lakujenga shule

Si maeneo yote ambayo wabunge wanafanikiwa kupita, Diwani anapaswa kuripoti kwa Mbunge then mbunge alipeleke serikalini. Mbunge ana haki ya kumlaumu Diwani.

Mbunge ni mwakilishi wa watu na hivyo anatakiwa afanye kazi za kiuwakilishi na ndio maana kodi zetu zinamuwezesha ili aweze kuwafikia watu wake eneo lote!Tumemkopesha gari,tunamlipa posho ya mafuta nk kwa ajil ya kazi hiyo so hoja eti si maeneo yote wabunge wanafanikiwa kupita HAISHIKI MAJI!
 
Lawama ziende kwa serikali dhalimu ya CCM na siyo huyo mbunge ambaye kazi yake ni kuikumbusha serikali tu.
jirani tu hapa wilaya ya rufiji kulikuwa na shule ina mwalimu mmoja na darasa moja na ya nyasi na ni km 60 kutoka dar, ndo mazingira ya shule zetu za kitanzania na sera za magamba.ufisadi mtupu!!!!!!!!!!
 
Hawa ndiyo wale wabunge tunaowachagua kwa lazima na ccm ambao wanaishi mjini na wakati wa uchaguzi tu ndiyo wanaenda kwa wananchi; wakishinda basi kazi imekwisha wanaondoka... Mbuge kama huyu wananchi hawatakiwa wasubiri uchaguzi; wanatakiwa tu waandamande kumtoa kwa nguvu.
 
Back
Top Bottom