Mbunge Abood azungumza na Wananchi kata ya Chamwino mtaa wa Maelewano eneo la Pombe shop

Oct 8, 2023
37
17
MHE. ABOOD AZUNGUMZA NA WANANCHI KATA YA CHAMWINO MTAA WA MAELEWANO ENEO LA POMBE SHOP .

Mnamo Majira ya saa kumi tarehe 24.10.2023, Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe. Abdulaziz M. Abood amefika katika Kata ya Chamwino Mtaa wa Maelewano baada ya wito wa Wananchi takribani 70 kwa minajri ya kusikiliza kero na changamo za Wananchi hao waliobomolewa Nyumba zao kwa kupisha Ujenzi wa Shule ya Msingi ndani ya Kata hiyo na wengi kuachwa bila matumaini ya uhakika wa kuishi.

Mhe.Mbunge akapata wasaa wa kusikiliza na kufanya majadiliano ya kina na Wananchi hao hasa wale husika wanaosadikika kuwa kwenye mzunguko wa ilipokuwa Pombe Shop,

MADAI/MALALA MIKO YA WAHUSIKA.
Wananchi hao, wakaelezea masikitiko makubwa na maumivu wanayopitia hasa familia zao nyingi kukosa makazi mara baada ya kubomolewa na aidha wakaelezea Matamanio yao mbele ya Mhe. Mbunge, huku wakimuomba haki itendeke na kubainisha kuwa mchakato wa ubomoaji na uamisho haukuzingatia haki vilevile wakimuomba Mhe.Mbunge, suala lao la kupatiwa viwanja na fidia ya ujenzi liwe la uhakika ili wapishe ujenzi wa Shule bila vinyongo.

NENO LA MBUNGE
Mbunge akizungumza na Wananchi hao akasema kuwa amesikia kila aina ya maoni na mapendekezo ya Wananchi hao na ya kwamba atafikisha suala hilo katika ngazi zake za juu hasa akitoa mapendekezo ushauri na maombi ya wananchi hao kwa wakubwa zake hasa akizingatia mambo mawili

a) Kuhakikisha upatikanaji wa Maeneo waliopewa yanapatikana kama ilivyo hakika
b) Kuona kuwa Suala lao la Pili linazingatiwa.

Sambamba na hilo Mhe. Mbunge aliuliza kama kuna anayepinga shule kujengwa katika eneo hilo na Wananchi wote walilidhia ila dukuduku yao ikawa namna ya kuama

HITIMISHO
Baada ya majibu hayo, Wananchi wakafurahi na kuona faraja ya kuwa na Mhe. Mbunge na hasa alivyoitikia wito wao, na kuhaidi kusubili wakati Mhe. Mbunge akiendelea kulifanyia kazi
 
Back
Top Bottom