Mbunge Daniel Awack anahujumu mradi wa Wananchi ulioletwa na Serikali Mang'ola

Tizzo G

Member
Jun 9, 2012
24
14
Kumekuwa na tetesi kutoka kwa wananchi na watu wa karibu sana na palipotakiwa kuanzishwa mradi wa bwawa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji kwa wananchi wa Mang'ola barazani Wilaya ya Karatu. Cha kushangazi mbunge huyu wa CCM amewadanganya wananchi kwamba eti bwawa likijengwa litasababisha mafuriko na kuharibu mashamba yao kumbe lengo lake ni ili mradi wa bwawa usifanyike ili alinde mashamba yake aliyonayo eneo la mang'ola barazani.

Pia kuwepo kwa bwawa hilo kutapunguza soko la mazao ya mbunge huyo kwani wananchi wengi watakuwa na uwezo wa kulima kwa kutumia maji ya bwawa hilo.

Kulikuwa na tetesi za Rais kuja kuzindua uanzishwaji wa mradi huo lakini hakuweza kuja sababu ya mgogoro uliopo ambao chanzo chake ni mbunge huyo.

Tungependekeza waandishi wa habari ambao ni wabobezi wangechunguza hili jambo na pia uongozi wa mkoa wa Arusha walitazame hili.

Mbunge huyu alishawahi kuweka mashine za umwagiliaji kwenye chanzo cha maji hali iliyosababisha mgogoro na kamati ya maji Kijiji cha mang'ola barazani hali iliyopelekea mashine hizo kuchomwa moto na watu wasiojulikana.

Hali hiyo ilipelekea mbunge huyo kutuhumu na kuushtaki uongozi wa katika ya maji kwamba ndio waliohusika kuchoma mashine zake na kesi iliendeshwa Arusha mjini kwa muda wa miezi kumi, mwishowe mbunge huyo alikosa ushahidi na akashindwa kuwatia hatiani aliowashtaki.

Pia mbunge huyu anaendesha mashamba ya kilimo karibu na shule ya sekondari ya Domel iliyopo mang'ola barazani Karatu, wakati wa kupulizia dawa mazao yake haswa vitunguu, maeneo ya shule yanakuwa sio rafiki kwa sababu ya ile harufu kali ya dawa kwa wanafunzi na wafanyakazi wa shule hiyo.

Rais
ccm
Liangalieni hili Kwa sababu mbunge huyu anahujumu maendeleo ya wananchi.
 
Ingawa hizi ni tetesi kuna uwezekano mkubwa zikawa ni za kweli kwasababu huyu mbunge ni mkulima mkubwa wa vitunguu na huenda miradi kama hiyo ikayumbisha maslahi yake.

Awaki ni miongoni mwa wabunge wa CCM walioingia bungeni kwa kubebwa kwenye uchaguzi haramu wa 2020. Kuna kashfa inamwandama yeye na aliyekuwa katibu mwenezi enzi za mwendazake kupeana rushwa ya mamilioni ili kupitisha jina lake.

Ninaisihi CCM isirudie tena kosa lililofanyika 2020. Majina ya watu wengi waliopaswa kuwa wabunge kupitia CCM yalikatwa na kuwekwa vilaza kama huyu Awaki, Tale na Shigongo.
 
Uzuri ni kwamba awakii ana Hela amefanikiwa Sana kwenye kilimo, sioni la kushangaza akiyumbisha mradi kama huo akishirikiana na viongozi Wala rushwa waliopo kwenye selikali ya mang'ola
 
Back
Top Bottom