ramadhani samizi
Member
- Jun 5, 2014
- 44
- 6
Piga MBA-procurement and logistics,nadhani ipo mlimani na udom kama ckosei.over
MBA ni nzuri, lakini jitahidi kufikiria nje ya box. Sio uzuri wake katika soko la ajira. Maana waajiri wazuri wakiajiri wewe utakuwa huna chako... Kuna kujiajiri pia...Habari zenu wana jf.. mimi nina bachelor (B.sc.ed), nafikiria kujiunga open university ..nataka kuchukua MBA mwaka huu..ila nahitaji-ushauri kwanza je chaguo langu ni sahihi kwa hali ya sasa?..maana siku za nyuma nlisikia watu wengi walikimbilia huko..ambaye amesoma hii master au ana uzoefu na hili anishauri..
Piga MBA-procurement and logistics,nadhani ipo mlimani na udom kama sikosei over
Ndugu yangu nivizuri kupata ushauri sahihi kuliko kupotoshwa tu hapa!
Binafsi nimesoma BBA,nimekaa mtaani nikisaka ajira kwa muda mrefu ....
Mwaka jana nikapata ushauri toka kwa Prof. flani wa Mzumbe alinishauri kwamba MBA ni nzuri kwa mtu aliye kazini (mfano mhasibu) anapotaka kuongeza maarifa zaidi yakiuongozi katika fani yake(eg:-uhasibu) basi mtu huyo anaweza akasoma MBA in Accountancy......
Au ni nzuri kwa mtu mwenye mtazamo wakujiajili na si kuajiliwa..
Kwa ushauri zaidi ni PM nikupe ushauri zaidi.
Na kwasasa MBA inatolewa na karibu vyuo vyote hapa Tz....
So MBA ni kozi iliyotema sana na inaendelea kutema zaidi hivyo ni vizuri ukawa makini kabla yakuchagua kitu cha kusoma.
hapa tunazungumzia masters
na kuhusu uzoefu masters yoyote inakuwa nzuri ukishakuwa kazn....
Ni nadra kukuta taasis inaajiri master amby ni fresh bila uzoefu.. Labda za kufundisha
Nashukuru tayari nimepata admission ya hii course...sasa kinachofuata ni kupata ushauri ktk specialization kati ya hzi..
1.finance
2.accounting
3.Marketing
4.human resource
5.logistics and transport
Ipi imetulia hapo?