Hivi Mange ni tishio kuliko Snowden?

Hivi Mange ni tishio kuliko Snowden?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,852
Reaction score
831,131
Ni watu wawili tofauti kabisa kuanzia asili mpaka jinsia bila kusahau habari zao.. Labda kinachowakutanisha ni ule uthubutu wa kufunua ya sirini juu ya serikali zao... Lakini Snowden kampiku Mange yeye sio serikali yake tu bali serikali mbalimbali duniani... Huyu ni mdukuzi wa kimataifa, mjanja mwerevu na mchawi wa software.... Nywila gani imshinde Snowden? Kama kaziweza za marekani zile ambazo ni very sensitive atashindwa na ipi?
Snowden ni kitisho hasa kwa serikali ya nchi yake.... Kuna baadhi ya mambo hubaki kuwa siri za nchi na kuyatoa nje kabla ya muda wake kuwadia ni hatari sana.. Snowden anafurahiwa na mataifa adui wa marekani.... ANATOA SIRI ZA NCHI... hapa kuna kukosa uzalendo wa aina fulani... Hata kama jambo ni baya lakini kama linamaanisha kuilinda nchi kukaa kimya pia ni jambo la busara kuliko kupayuka.....!!!
Mange Kimambi mdogo wangu huyu... Sometimes ni kama chizi mropokaji lakini ana uthubutu ambao wengi hawana.... Wakosoaji aina yake wapo popote duniani na ni muhimu kuwa na watu wa kaliba yake.... Anakufanya uwe makini zaidi na utende kwa weledi zaidi.... Lakini tofauti na Snowden Mange habari zake sio za udukuzi bali na za kupewa na watanzania wenyewe walioko kwenye nafasi ya kuzipata habari husika.... Mange hana makosa analetewa HADUKUI.. HANA UWEZO HUO....!!!!
Sifurahishwi na baadhi ya post zake, zingine zina utoto mwingi, na baadhi ni mambo ya kike kuzodoana na kutambiana, kusemana vibaya na kutukanana... Lakini ukiondoa hayo makandokando kuna vitu makini anatuma japo naye anapelekewa.....
Ni aibu kwa serikali kuacha mambo muhimu na kuanza kuhangaika na mkosoaji wa mitandaoni... Ni aibu kwakuwa kama serikali ni safi basi haiwezi kuchafuliwa na post za kimbeambea... Ukiona serikali inaaza kuhangaika na kufanya figisu nyingi ili kummaliza Mange jua kuna kitu si bure... Kuna mambo yasiyo na faida kwa Taifa yanajaribu kufichwa.. Kuna kaliba inalindwa isiyo na faida yoyote kwa Taifa.....!!!
Watende kwa weledi, makosa yapo hatukatai... Hakuna mkamilifu hata mmoja akiwemo Mange mwenyewe lakini kutumia nguvu nyingi kuhangaika naye ni ishara tosha kuwa yuko sahihi na kuna tatizo kubwa mahali
 
Ccm kaz yake n kununua tu wanachama
IMG-20171203-WA0053.jpg
 
CCM haina sera tena imebaki kutumia dola kwa mambo ya kijinga kabisa, badala ya kuelekeza nguvu kwenye viwanda wameelekeza kwenye kesi.
IMG-20171203-WA0048.jpg
Mange kazi yake yeye ni kupokea habari kama zilivyo na kuzirusha.. Hahangaiki... Ukiona hivyo ujue system imejaa matobo... Hakuna kitu kinachoitwa tight mark... Hakivuji chochote
 
Ni watu wawili tofauti kabisa kuanzia asili mpaka jinsia bila kusahau habari zao.. Labda kinachowakutanisha ni ule uthubutu wa kufunua ya sirini juu ya serikali zao... Lakini Snowden kampiku Mange yeye sio serikali yake tu bali serikali mbalimbali duniani... Huyu ni mdukuzi wa kimataifa, mjanja mwerevu na mchawi wa software.... Nywila gani imshinde Snowden? Kama kaziweza za marekani zile ambazo ni very sensitive atashindwa na ipi?
Snowden ni kitisho hasa kwa serikali ya nchi yake.... Kuna baadhi ya mambo hubaki kuwa siri za nchi na kuyatoa nje kabla ya muda wake kuwadia ni hatari sana.. Snowden anafurahiwa na mataifa adui wa marekani.... ANATOA SIRI ZA NCHI... hapa kuna kukosa uzalendo wa aina fulani... Hata kama jambo ni baya lakini kama linamaanisha kuilinda nchi kukaa kimya pia ni jambo la busara kuliko kupayuka.....!!!
Mange Kimambi mdogo wangu huyu... Sometimes ni kama chizi mropokaji lakini ana uthubutu ambao wengi hawana.... Wakosoaji aina yake wapo popote duniani na ni muhimu kuwa na watu wa kaliba yake.... Anakufanya uwe makini zaidi na utende kwa weledi zaidi.... Lakini tofauti na Snowden Mange habari zake sio za udukuzi bali na za kupewa na watanzania wenyewe walioko kwenye nafasi ya kuzipata habari husika.... Mange hana makosa analetewa HADUKUI.. HANA UWEZO HUO....!!!!
Sifurahishwi na baadhi ya post zake, zingine zina utoto mwingi, na baadhi ni mambo ya kike kuzodoana na kutambiana, kusemana vibaya na kutukanana... Lakini ukiondoa hayo makandokando kuna vitu makini anatuma japo naye anapelekewa.....
Ni aibu kwa serikali kuacha mambo muhimu na kuanza kuhangaika na mkosoaji wa mitandaoni... Ni aibu kwakuwa kama serikali ni safi basi haiwezi kuchafuliwa na post za kimbeambea... Ukiona serikali inaaza kuhangaika na kufanya figisu nyingi ili kummaliza Mange jua kuna kitu si bure... Kuna mambo yasiyo na faida kwa Taifa yanajaribu kufichwa.. Kuna kaliba inalindwa isiyo na faida yoyote kwa Taifa.....!!!
Watende kwa weledi, makosa yapo hatukatai... Hakuna mkamilifu hata mmoja akiwemo Mange mwenyewe lakini kutumia nguvu nyingi kuhangaika naye ni ishara tosha kuwa yuko sahihi na kuna tatizo kubwa mahali

MSHANA NA WEWE WAKATI MWINGINE MMMMMMHHH !!!!! ACHA NIISHIE HAPO.
 
Je na Nyarandu alinunuliwa kwa sh ngapi ! Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu muchungu kwani matusi ya mange yanaisaidia nini nchi wewe kama ni jasiri fungus act ya matusi hatuna muda huo kwa sasa hapa ni kazi tu
 
View attachment 643152Mange kazi yake yeye ni kupokea habari kama zilivyo na kuzirusha.. Hahangaiki... Ukiona hivyo ujue system imejaa matobo... Hakuna kitu kinachoitwa tight mark... Hakivuji chochote

Mkuu, lakini hiyo kazi si rasmi ya Mange Kimambi kupokea habari zinazovuja na kuzirusha.

Pili, kama ni kazi yake rasmi si ingeeleweka tu na akatambulika rasmi?

Akitambulika rasmi basi anakuwa "responsible" na habari hizo.

Vinginevyo anakuwa mtu wa kati katika kusambaza habari zisizo rasmi na zilizovujishwa.

Kuna sheria ipo Tanzania ambayo yaitwa Access of Information Act ya mwaka 2016 ilosainiwa na Dr Mwakyembe , je unaifahamu?

Tatu, hakuna serikali yoyote ile duniani ambayo imefanikiwa kuzuia kuvuja kwa taarifa zake za siri ambazo haziruhusiwi kuonwa na umma, na mifano tunayo kama huo wa Snowden na wengine ambao walitoa hizo siri na leo ni maadui namba moja kwa nchi zao.

Ukiajiriwa serikalini na ukala kiapo ambacho kina kipengele cha kulinda siri za serikali basi baadae unapokiuka kiapo kicho unakuwa "responsible" yaani unawajibika.

Sasa kuwajibika kunategemea na mdhamini wako yaani mwajiri wako - serikali.

Lakini siyo ujidhamini mwenyewe kama mhalifu namba moja.
 
Back
Top Bottom