Hivi Malezi yamenishinda?

Hivi Malezi yamenishinda?

Pole sana baba yake ni Afande nini?
hatakiwi kuwa mkali sana kwa mtoto kuna stage ambazo mtoto anapitia hizo za kulisha midoli na kusambaza vitambaa ni mambo madogo kwa mtoto katika ukuaji
Saidianeni kumfundisha na sio kamwaga maji kibao cha kushitukiza ..Mwisho mtamkomaza mtoto na viboko.
sipati picha dogo na makofi ya baba daaah
nadhani kanatamani kuhama mtaa
 
Pole sana baba yake ni Afande nini?
hatakiwi kuwa mkali sana kwa mtoto kuna stage ambazo mtoto anapitia hizo za kulisha midoli na kusambaza vitambaa ni mambo madogo kwa mtoto katika ukuaji
Saidianeni kumfundisha na sio kamwaga maji kibao cha kushitukiza ..Mwisho mtamkomaza mtoto na viboko.

hello!
 
sipati picha dogo na makofi ya baba daaah
nadhani kanatamani kuhama mtaa

kofi la baba linauma, hasa kama kofi limebeba uchungu wa kukosa hela, kisa dili halijatiki....mtoto lazima aone maruweruwe
 
Naanimi adhabu iendane na umri wa mtoto na uzito wa kosa lenyewe.
Vinginevyo atakuwa sugu(anaamua kuwa rebellious)

Ikifikia point hii huwa ni mbaya sana kwa mtoto na mzazi mwenyewe
Hakuna anayemsikiliza mwenzie.


Unataka kusema mtoto wa miaka mingapi ndo anafaa kuchapwamaana enzi zetu ilikuwa sio kuchapwa tu,mtu ulikuwa unakimbizwa na panga kabisa
Mimi mapanga yalishanikosa kosa sana
Sijui ningekuwa nauzaje sura mjini hapa loh
 
kofi la baba linauma, hasa kama kofi limebeba uchungu wa kukosa hela, kisa dili halijatiki....mtoto lazima aone maruweruwe
je hasira ya kunyimwa unyumba ? ukute tena kanafanana na mamake
 
salama Husninyo ...? jifunze malezi ya katoto hapa kasije kukuletea mambo ya smile D for dushelele

ndio najifunza hapa fl, nisije kutaabika na malezi. Mi huyo mme ningekuwa namdunda. Hawezi kumpga mpga mtoto kizembe.
 
sipati picha dogo na makofi ya baba daaah
nadhani kanatamani kuhama mtaa

Hahaha
balaa hapo baba ana hasira za kukosa deal hapo hasira lazima ziishie kwa mtoto
Au anaangalia mechi timu yake imefungwa hapo lazima hasira kwa mtoto
 
Mtoto ni halali yake kupata MKATE na KIBOKO

Lakini sitegemei mpaka mtoto akuone mbaya kiasi cha kukuogopa

Hapo pana shida, Baba ni Lazima abadirike

Na isije kuwa Baba anahasira zake Labda anavidalili mtoto si wake, Mama kuwa mwangalifu kusije tokea yasiyotegemewa
 
Ila mie naona asilimia kubwa ya wababa huwa wanapenda kupiga watoto bila kujali umri wa mtoto! Afu pia hawaangalii sehemu ya kupiga, kichwani, vibao ndio wanapendelea.

Sasa mtoto wa 4yrs wamchapa makofi huyo mamake je utamfanyaje? Sipendi yaani najisikiaga kuchezwa na utumbo kama sio chango.
 
Huyo Baba asijeakawa na frustration zake halafu anazimalizia kwa mtoto anaweza akamuaribu mtoto sehemu za mwili wake. Mtoto wa miaka minne ni wa kufinywa tu kama anarudia rudia kosa, lakini sio kuchapwa. Makosa mengine mtoto kama huyo anatakiwa kuonywa kwa mdomo tu wala sio kipigo. Watoto wote wanapitia stage kama hizo, wao wakijua ni michezo kumbe ni uharibifu. Huyo Baba ajue watoto kuna umri wa kufundishwa na kuonywa kwa mdomo tena kwa upole na kuna umri wa kufinya kidogo na kuna umri wa adhabu kali zaidi. Huyo mtoto yupo stage ya kuonywa kwa kufinywa kidogo. Mshauri huyo Baba ajirudi na ajitaidi kutafuta ukaribu wa kuwa na mtoto maana kinachotokea sasa ni kibaya sana kwa mahusiano yake na mtoto.
 
Hahaha
balaa hapo baba ana hasira za kukosa deal hapo hasira lazima ziishie kwa mtoto
Au anaangalia mechi timu yake imefungwa hapo lazima hasira kwa mtoto
Akiguswa tu na mtoto utasikia ondoka hapa, hebu kalale wakati mtoto ndio katoka kuamka mda huo lol. Wamama tuna kazi..
 
ndio najifunza hapa fl, nisije kutaabika na malezi. Mi huyo mme ningekuwa namdunda. Hawezi kumpga mpga mtoto kizembe.
Hahahaha! Unamdunda??? Swahiba unaringa vile una manyama eeh?
 
Mtoto wa miaka minne siyo mdogo kihivoy ila haihalalishishi eti pigwe kikamilifu. Kuna makosa mengine ni minor hata akirudia mara nyingi kwa umri huo anaweza samehewa. Lakini wakati mwingine kosa la kwanza anapigwa ili kustrengthen karipio! Shida ipo kama leo unamuona mdogo humpigi kabisaa hutajua kamwe kama kakua na anastahili kupigwa sababu transition haiji overnight!
Tatizo lingine wanawake mnadhani watoto ni wenu peke yenu baba hahusiki! Afu mtoto wa miaka minne mkubwa bwana si anatakiwa aanze nasare huyo! Sasa kama hasikii akiambiwa atakuwa mjeuri mwalimu akisema kelele hata sikia
 
sijui nani aliwaambia wazazi wengine kupiga au kutukana ndo kulea jamani agrrrrrrrrrrrrrr!!!

sasa hako kamalaika miaka minne unakapiga wapi hasa? mtoto anahitaji upendo wa hali ya juu ili ajifunze kinyume na hapo mnamjengea hofu isyokuwa na mantiki yeyeote na mtashangaa hata shuleni mnaweza kuwa mnamuathiri katika kujifunza kwake.

mmenikumbusha jirani yangu, hapa namvutia kasi kuna siku ntamwambia ukweli, anamtukana mjukuu wake matusi ya nguoni, binti ninavomuona ni kama anakuwa sugu na ana tabia za ajabu ajabu sana. yeye kuitwa mbwa ni kawaida sana tena kwa kosa hata la kuvaa sandals za bibi yake...
 
Dada umesahau enzi zile baba akikohoa tu watu wote mpo uvunguni
lakini baba kuwa mkali sometimes inasaidia
wengine tungekuwa neti humu

Smile nadhani kuna makosa ambayo baba yake anaweza kumchapa..kweli la kumwaga maji mezani ama sahani ya chakula imedondoka ndo unamchapa kibao utadhani mtu mzima ..
 
Back
Top Bottom