Muundo wa mahakama kwa upande wa Zanzibar wanaye Regiona Resident Magistrate (RRM).Bara kuna RM.Ikumbukwe huko nyuma kwa ukosefu wa wasomi wa kutosha,mahakama za mwanzo zilisimamiwa na mahakimu wenye Certificate ya Sheria, Wilaya Diploma na mahakimu wenye shahada ya Sheria walikuwa wanavalishwa kofia za kuwa mahakimu wa kazi.Hawa walikaa mijini na walisimamia mahakama na kuendesha mashauri yenye taswira zilizoainishwa na sheria.Ilizoeleka kuzikuta mahakama hizi na mahakimu hawa maeneo ya mijini.
Mpaka leo bado ipo hivyo lakini siku hizi kwa mfano hapa Dar wapo mahakimu wakazi wanafanya kazi mahakama za mwanzo na ninadhani muda so mrefu muundo utaenda kubadilishwa kuwe na mahakma maalumu kwa ngazi ya mkoa ambayo itakuwa na mamlaka ya rufani toka wilayani. Kwa sasa mahakama ya hakimu mkazi haina tafsiri ya kuwa mahakama ya mkoa bali yenye mamlaka ya kusikiliza kesi za thamani na taswira flani zikisimamiwa na mahakimu wenye elimu kuanzia shahada moja kwenda juu . Zinaweza kuwa zaidi ya moja ndani ya jiji, mji au manispaa moja.