Ni hivi, mahakama ya Tanzania imegawanyika katika sehemu kuu 2, (nitaanzia ya juu kabisa)
1. Mahakama kuu ambayo inahusisha (a) Mahakama ya Rufani (Court of Appeal) na (b) Mahakama kuu (High court) hizi zote mbili zipo katika kundi la mahakama kuu, Mahakama ya Rufani in mamlaka bara na visiwani, lakini mahakama kuu ina mamlaka yote kwa Tz bara.
2. Mahakama za chini (subordinate courts)
i. Mahakama ya Hakimu mkazi wa mkoa
ii. Mahakama ya wilaya
iii. Mahakama ya mwanzo
I. MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI (COURT RESIDENT MAGISTRATE)
Hii ipo moja katika kila mkoa, kwa maana ya kuwa na mamlaka juu ya mashauri yote yanayotokea ndani ya mkoa katika kiwango (jurisdiction) kilichowekwa
II. MAHAKAMA YA WILAYA (DISTRICT COURT)
Hii ipo moja katika kila wilaya kusikiliza mashauri yanayoangukia katika mamlaka yake ndani ya wilaya hiyo
III. MAHAKAMA YA MWANZO (PRIMARY COURT)
Hizi zipo katika kila wilaya na zinaweza kuwa zaidi ya moja kulingana na ukubwa wa eneo husika, na husikiliza mashauri madogo (yaani kesi ndogondogo)
Linapotokea suala ambalo mtu atahitaji kwenda mahakamani, mtu huyo haamui tu kuchagua mahakama gani aende kufungua shauri (case) lake, kila kesi ina uzito wake iwe ya madai au ya jinai (isipokuwa masuala ya mirathi na ndoa za kiislam) mfano mtu anayekudai milioni 20 hawezi kwenda fungua shauri lake mahakama ya mwanzo, kwa kuwa haina nguvu ya kusikiliza kesi za madai zinazozidi millioni 10, hivyo mtu huyo atatakiwa kupeleka shauri lake mahakama ya wilaya ambayo makubaliano ya kupeana hizo hela yalifanyika, mkataba ukifanyikia Arusha, hamuwezi fungua kesi Iringa kwakuwa wote mnaishi Iringa, kesi itatakiwa ifunguliwe Arusha, hayo nayo ni mamlaka.
Kimsingi kuna vitu vingi vya kimamlaka vya kuangalia kabla hujafungua kesi katika mahakama fulani, na ukikosea ukafungua kesi kwenye mahakama isiyokuwa na mamlaka, basi kesi yako itatumbiliwa mbali.
Hivyo Kuona kisutu kunakuwa na kesi nyingi ni kutokana na ukubwa (siyo wa eneo) wa jiji wa Dar es salaam, ndiyo maana hujawahi sikia mbunge lema amepelekwa kisutu, au BUlaya amepelekwa kisutu.
so hili ni suala la kisheria