Hivi Mahakama ni Kisutu tu?

Hivi Mahakama ni Kisutu tu?

Cko deep sana na mifumo ya kimahakama bt what I'know ni Mahakama ya kinondoni ni ya wilaya Kinondoni same to Samora ambayo ni ya Ilala na mahakama ya Temeke ambayo ni ya wilaya ya Temeke.. Kisutu inapata Power ya kusikiliza kesi ambazo zingefaa kusikilizwa high court under extended jurisdiction sec 173 CPA(Nimeuliza wajuzi)
Hata hakimu wa Kinondoni anaweza kupata nguvu hiyo (Extended Jurisdiction) coz ni hakimu mkazi na yeye kama yule wa Kisutu. Hii nguvu haipewi MAHAKAMA anapewa HAKIMU mkazi anayekuwa akisikiliza shauri husika.
 
Ni hivi, mahakama ya Tanzania imegawanyika katika sehemu kuu 2, (nitaanzia ya juu kabisa)
1. Mahakama kuu ambayo inahusisha (a) Mahakama ya Rufani (Court of Appeal) na (b) Mahakama kuu (High court) hizi zote mbili zipo katika kundi la mahakama kuu, Mahakama ya Rufani in mamlaka bara na visiwani, lakini mahakama kuu ina mamlaka yote kwa Tz bara.

2. Mahakama za chini (subordinate courts)
i. Mahakama ya Hakimu mkazi wa mkoa
ii. Mahakama ya wilaya
iii. Mahakama ya mwanzo

I. MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI (COURT RESIDENT MAGISTRATE)
Hii ipo moja katika kila mkoa, kwa maana ya kuwa na mamlaka juu ya mashauri yote yanayotokea ndani ya mkoa katika kiwango (jurisdiction) kilichowekwa

II. MAHAKAMA YA WILAYA (DISTRICT COURT)
Hii ipo moja katika kila wilaya kusikiliza mashauri yanayoangukia katika mamlaka yake ndani ya wilaya hiyo

III. MAHAKAMA YA MWANZO (PRIMARY COURT)
Hizi zipo katika kila wilaya na zinaweza kuwa zaidi ya moja kulingana na ukubwa wa eneo husika, na husikiliza mashauri madogo (yaani kesi ndogondogo)

Linapotokea suala ambalo mtu atahitaji kwenda mahakamani, mtu huyo haamui tu kuchagua mahakama gani aende kufungua shauri (case) lake, kila kesi ina uzito wake iwe ya madai au ya jinai (isipokuwa masuala ya mirathi na ndoa za kiislam) mfano mtu anayekudai milioni 20 hawezi kwenda fungua shauri lake mahakama ya mwanzo, kwa kuwa haina nguvu ya kusikiliza kesi za madai zinazozidi millioni 10, hivyo mtu huyo atatakiwa kupeleka shauri lake mahakama ya wilaya ambayo makubaliano ya kupeana hizo hela yalifanyika, mkataba ukifanyikia Arusha, hamuwezi fungua kesi Iringa kwakuwa wote mnaishi Iringa, kesi itatakiwa ifunguliwe Arusha, hayo nayo ni mamlaka.

Kimsingi kuna vitu vingi vya kimamlaka vya kuangalia kabla hujafungua kesi katika mahakama fulani, na ukikosea ukafungua kesi kwenye mahakama isiyokuwa na mamlaka, basi kesi yako itatumbiliwa mbali.

Hivyo Kuona kisutu kunakuwa na kesi nyingi ni kutokana na ukubwa (siyo wa eneo) wa jiji wa Dar es salaam, ndiyo maana hujawahi sikia mbunge lema amepelekwa kisutu, au BUlaya amepelekwa kisutu.

so hili ni suala la kisheria
 
Hakuna mahakama ya mkoa kwenye muundo wa mahakama. Kuna mahakama ya wilaya ambayo ndiyo hiyo hiyo mahakama ya hakimu mkazi. So ukisikia mahakama ya wilaya basi ujue hakimu wake ni hakimu mkazi na anaweza kaa kwenye mahakama yoyote ya hakimu mkazi. Siku hizi hata mahakama za mwanzo wanaajiriwa mahakimu wakazi. So Kisutu na mahakama ya Wilaya Kinondoni zote zina mamlaka MOJA kisheria. Suala la kwanini kesi nyingi zinafunguliwa Kisutu ni masuala tu ya Kijiografia (Territorial jurisdiction) na Kisutu ndio ina territorial jurisdiction ya Dar (Ufafanuzi wa kina wahitajika so tafuta mjuzi akuelekeze)
Unataka kusema katika muundo wa mahakama Tanzania kuna ngazi nne tu
 
Unataka kusema katika muundo wa mahakama Tanzania kuna ngazi nne tu
Tukianzia chini:

Mahakama ya mwanzo

Mahakama ya Wilaya/Hakimu Mkazi

Mahakama kuu

Mahakama ya Rufaa

So umeuliza jibu tuna ngazi NNE, maana rufaa ikitoka mahakama ya wilaya haiendi hakimu mkazi inakwenda mahakama kuu. Ndio maana Kwenye muundo mahakama ya wilaya/hakimu mkazi huwekwa pamoja.
 
sawa nakubaliana na wewe kwenye issue ya appeals from DRM, lakini Je mahakama ya wilaya ya Temeke ina territorial jurisdiction kwa Dar es salaam?
 
Tukianzia chini:

Mahakama ya mwanzo

Mahakama ya Wilaya/Hakimu Mkazi

Mahakama kuu

Mahakama ya Rufaa

So umeuliza jibu tuna ngazi NNE, maana rufaa ikitoka mahakama ya wilaya haiendi hakimu mkazi inakwenda mahakama kuu. Ndio maana Kwenye muundo mahakama ya wilaya/hakimu mkazi huwekwa pamoja.
Kitu kinachochanganya hapa ni levels za mahakimu kwa wote ni RM hata Primary wapo, lakini haimaanishi kwamba mahakama hizi zinalingana nguvu absolutely, kuna issues huwezi zi institute wilayani na ni lazima ziende Kisutu, mfano mgogoro wa taasisi yoyote yenye ngazi ya mkoa, huwezi ipeleka wilayani.

so mfumo wa mahakama una ngazi 5, unaweza ni sahihisha pia
 
Huchelewi pia kuuliza kwanini Hosp. MHIMBILI tuu kwani hakuna zingine? Kwann isiitwe TAIFA? Maswali mengine huwa ni ya kitoto sana
 
Ni hivi, mahakama ya Tanzania imegawanyika katika sehemu kuu 2, (nitaanzia ya juu kabisa)
1. Mahakama kuu ambayo inahusisha (a) Mahakama ya Rufani (Court of Appeal) na (b) Mahakama kuu (High court) hizi zote mbili zipo katika kundi la mahakama kuu, Mahakama ya Rufani in mamlaka bara na visiwani, lakini mahakama kuu ina mamlaka yote kwa Tz bara.

2. Mahakama za chini (subordinate courts)
i. Mahakama ya Hakimu mkazi wa mkoa
ii. Mahakama ya wilaya
iii. Mahakama ya mwanzo

I. MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI (COURT RESIDENT MAGISTRATE)
Hii ipo moja katika kila mkoa, kwa maana ya kuwa na mamlaka juu ya mashauri yote yanayotokea ndani ya mkoa katika kiwango (jurisdiction) kilichowekwa

II. MAHAKAMA YA WILAYA (DISTRICT COURT)
Hii ipo moja katika kila wilaya kusikiliza mashauri yanayoangukia katika mamlaka yake ndani ya wilaya hiyo

III. MAHAKAMA YA MWANZO (PRIMARY COURT)
Hizi zipo katika kila wilaya na zinaweza kuwa zaidi ya moja kulingana na ukubwa wa eneo husika, na husikiliza mashauri madogo (yaani kesi ndogondogo)

Linapotokea suala ambalo mtu atahitaji kwenda mahakamani, mtu huyo haamui tu kuchagua mahakama gani aende kufungua shauri (case) lake, kila kesi ina uzito wake iwe ya madai au ya jinai (isipokuwa masuala ya mirathi na ndoa za kiislam) mfano mtu anayekudai milioni 20 hawezi kwenda fungua shauri lake mahakama ya mwanzo, kwa kuwa haina nguvu ya kusikiliza kesi za madai zinazozidi millioni 10, hivyo mtu huyo atatakiwa kupeleka shauri lake mahakama ya wilaya ambayo makubaliano ya kupeana hizo hela yalifanyika, mkataba ukifanyikia Arusha, hamuwezi fungua kesi Iringa kwakuwa wote mnaishi Iringa, kesi itatakiwa ifunguliwe Arusha, hayo nayo ni mamlaka.

Kimsingi kuna vitu vingi vya kimamlaka vya kuangalia kabla hujafungua kesi katika mahakama fulani, na ukikosea ukafungua kesi kwenye mahakama isiyokuwa na mamlaka, basi kesi yako itatumbiliwa mbali.

Hivyo Kuona kisutu kunakuwa na kesi nyingi ni kutokana na ukubwa (siyo wa eneo) wa jiji wa Dar es salaam, ndiyo maana hujawahi sikia mbunge lema amepelekwa kisutu, au BUlaya amepelekwa kisutu.

so hili ni suala la kisheria
nimekuelewa vizur kutoka juu mpaka chini sasa mwishoni cjakuelewa umetaja lema na bulaya vp yy tundu lissu alipelekwa mahakama gan
 
Hivyo Kuona kisutu kunakuwa na kesi nyingi ni kutokana na ukubwa (siyo wa eneo) wa jiji wa Dar es salaam, ndiyo maana hujawahi sikia mbunge lema amepelekwa kisutu, au BUlaya amepelekwa kisutu.

Vipi kuhusu Tundu Lissu mzee??? na yeye ni wa Dar es salaam..
Makosa alifanya mkutanoni Singida, kesi Kisutu... Unasemaje hapo

[HASHTAG]#Chief[/HASHTAG] Eng.
 
Vipi kuhusu Tundu Lissu mzee??? na yeye ni wa Dar es salaam..
Makosa alifanya mkutanoni Singida, kesi Kisutu... Unasemaje hapo

[HASHTAG]#Chief[/HASHTAG] Eng.
Lissu hakukamatwa kutokana Na issue yoyote Kama ilitokea pale Ikungi, kulikuwa Na RB ya kumkamata Lissu kwa makosa ya udhalilishaji ambayo 'inasemekana' aliyafanya pale Kisutu Dar.

kukamatwa kwake akiwa singida hakukumaanisha ametenda makosa hayo singida.
 
Lissu alipelekwa Kisutu kwa kosa alilolifanya "wanavyosema" palepale Kisutu, Na wala sigo Singida. Nilivyomtaja bulaya Na Lema nilimaanisha kesi za uchaguzi katika Kanda zao
nimekuelewa vizur kutoka juu mpaka chini sasa mwishoni cjakuelewa umetaja lema na bulaya vp yy tundu lissu alipelekwa mahakama gan
 
Dar Es Salaam kuna Mahakama mbili za Hakimu Mkazi (RMC) ambazo ni Kisutu na Kinondoni. Mahakama hii huanzishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania kwa kuzingatia Sheria ya Mahakama ya Hakimu Mkazi (Magistrates' Courts Act, Cap 11). Kuhusu uwezo wake (jurisdiction) wa eneo kijiografia huainishwa kwenye tamko la kuanzishwa kwake (Establishment Order).
Huweza kusikiliza rufaa toka katika Mahakama za Wilaya au za Hakimu Mkazi inapokasimiwa uwezo (Extended Jurisdiction).
 
Sasa kwa nini mahakimu wanaitwa mahakimu wakazi, kwani kuna mahakimu wageni
 
Mahakama ya Kinondoni ni ya mkoa wa Dar es salaam?? ..ulizia hata kwa wajuzi bac kabla hjaandika!
Anamaanisha Kinondoni kuna District court ambayo in charge wake ni Mhe Moshi na kuna Resident Magistrates' Court sasa hapo umemchanganya uliposema Mahakama ya mkoa ndo kuna RM's tu. Ni maamuzi tu Jamhuri kupeleka mashauri Kisutu na hakuna sababu maalum labda tuseme ukipeleka shauri Mahakama ya Mkoa inakusaidia kukuondolea mashaka ya kama umepeleka mshtakiwa katika Mahakama sahihi (Territorial jurisdiction) maana ni ngumu kwa Dar kujua mtuhumiwa ni mkazi wa Ilala au Kinondoni au temeke. Hivyo kuondoa usumbufu wa kujua ni mkazi wa wapi unapeleka shauri Mahakama ya mkoa.
 
Kisutu ndo mahakama ya mkoa wa Dar es salaam kila mkoa una mahakama yake na mahakimu wake huitwa hakimu mkazi rejea muundo wa mahakama ile kuanzia mahakama ya mwanzo mpaka ya rufani...nijuavyo mimi ni hivyo nitasahihishwa nilipokosea maana sio mwanasheria mimi
Hakuna mahakama ya mkoa bali mahakama ya hakimu mkazi(resident magistrate's courts).Zinaweza kuwa zaidi ya moja ndani ya mkoa au mji mmoja.
 
kisutu ndo yenye territorial jurisdiction over dar es salaam

ikumbukwe pia kuwa mahakama sio jengo bali ni hakimu/jaji

kwa mfano judge wa high court akikaa kisutu on record itaandikwa "in the high court of ..... sitting at kisutu" (emphasis is mine)
Wear mweredi
 
Back
Top Bottom