Hivi Mahakama ni Kisutu tu?

Hivi Mahakama ni Kisutu tu?

structuralist

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,230
Reaction score
909
Wakuu adhani wengi wetu tumekuwa tukishuhudia kesi nyingi zikifunguliwa Mahakama ya kisutu.

Kila wakati unasikia kesi iwe ya kisiasa au vinginevyo hasa inapohusisha watu "maarufu" lazima ifunguliwe Mahakama ya kisutu.

Naomba kujuzwa hivi hakuna Mahaska zingine Dar es Salam zenyewe uwezo wakusikiliza hizo kesi?

Hivi mawakili,karani nk wa Maha kama hiyo si wanazidiwa na kazi? Na je wale wa Mahakama zingine wanapumzika sana au inakuwaje? Tusaidiane hapo wasau.
 
Kisutu ndo mahakama ya mkoa wa Dar es salaam kila mkoa una mahakama yake na mahakimu wake huitwa hakimu mkazi rejea muundo wa mahakama ile kuanzia mahakama ya mwanzo mpaka ya rufani...nijuavyo mimi ni hivyo nitasahihishwa nilipokosea maana sio mwanasheria mimi
 
Hata Kinondoni ni Mahakama ya Mkoa wa Dar es salaam na kuna mahakimu wakazi wengi tu (RM,SRM) lakini mbona bado hawaendi huko?
 
Kisutu ndo mahakama ya mkoa wa Dar es salaam kila mkoa una mahakama yake na mahakimu wake huitwa hakimu mkazi rejea muundo wa mahakama ile kuanzia mahakama ya mwanzo mpaka ya rufani...nijuavyo mimi ni hivyo nitasahihishwa nilipokosea maana sio mwanasheria mimi

Tumia kiingereza kueleza muundo wa mahakama italeta kuelewa
 
Sasa si ndio ueleweshe?Hakuna anayejua kila kitu!
Cko deep sana na mifumo ya kimahakama bt what I'know ni Mahakama ya kinondoni ni ya wilaya Kinondoni same to Samora ambayo ni ya Ilala na mahakama ya Temeke ambayo ni ya wilaya ya Temeke.. Kisutu inapata Power ya kusikiliza kesi ambazo zingefaa kusikilizwa high court under extended jurisdiction sec 173 CPA(Nimeuliza wajuzi)
 
Umejibu vizuri sana
 
kisutu ndo yenye territorial jurisdiction over dar es salaam

ikumbukwe pia kuwa mahakama sio jengo bali ni hakimu/jaji

kwa mfano judge wa high court akikaa kisutu on record itaandikwa "in the high court of ..... sitting at kisutu" (emphasis is mine)
 
Na kwa nini inaitwa kisutu,kwa nin isiitwe mahakama ya mkoa wa dar es salaam?
 
Swalo halijajijibwa kwaninia wanafungua kisutu badala ya hakimu mkazi kinondoni, mfano swala la uchaguzi limetokea kinondoni na kinondoni mahakama ipo kwanini waende kisutu....
 
Kisutu ndo mahakama ya mkoa wa Dar es salaam kila mkoa una mahakama yake na mahakimu wake huitwa hakimu mkazi rejea muundo wa mahakama ile kuanzia mahakama ya mwanzo mpaka ya rufani...nijuavyo mimi ni hivyo nitasahihishwa nilipokosea maana sio mwanasheria mimi
Katika mfumo wa mahakama hatuna kitu kinaitwa mahakama ya Mkoa. Tuna Mahakama ya Hakimu mkazi (Resident Magistrate Court). Kuna historia ndefu ambayo ilipelekea kuwa na mahakama hiyo but before that tulikuwa na mahakama ya wilaya ambayo mpaka sasa bado ipo. Kwa hapa Dar kuna mahakama za hakimu mkazi mbili na pia sio lazima mahakama ya hakimu mkazi iwe katika mkoa. Zamani wakati Njombe ikiwa ni sehemu ya mkoa wa Iringa, pale Njombe kulikuwa na mahakama ya hakimu mkazi of which kwa mkoa wa Iringa by then kulikuwa na mahakama za hakimu mkazi 2. Nadhani kidogo naweza kuwa nimechangia kufafanua pale ulipoomba masahihisho
 
Kisutu ndo mahakama ya mkoa wa Dar es salaam kila mkoa una mahakama yake na mahakimu wake huitwa hakimu mkazi rejea muundo wa mahakama ile kuanzia mahakama ya mwanzo mpaka ya rufani...nijuavyo mimi ni hivyo nitasahihishwa nilipokosea maana sio mwanasheria mimi
Hakuna mahakama ya mkoa kwenye muundo wa mahakama. Kuna mahakama ya wilaya ambayo ndiyo hiyo hiyo mahakama ya hakimu mkazi. So ukisikia mahakama ya wilaya basi ujue hakimu wake ni hakimu mkazi na anaweza kaa kwenye mahakama yoyote ya hakimu mkazi. Siku hizi hata mahakama za mwanzo wanaajiriwa mahakimu wakazi. So Kisutu na mahakama ya Wilaya Kinondoni zote zina mamlaka MOJA kisheria. Suala la kwanini kesi nyingi zinafunguliwa Kisutu ni masuala tu ya Kijiografia (Territorial jurisdiction) na Kisutu ndio ina territorial jurisdiction ya Dar (Ufafanuzi wa kina wahitajika so tafuta mjuzi akuelekeze)
 
Back
Top Bottom