Hivi Madaktari wetu huwa wanashindwa kutafsiri matokeo ya vipimo?

Madaktari ni binadamu na kila mmoja ana uelewa wake anapokuwa Darasani.

Siyo kila daktari anajua, wengine ni vilaza tu.

Ila tatizo kubwa kwetu kama watanzania ni ugumu wa kukiri jambo fulani silijui au nimeshindwa.

Hali hii imesababisha wagonjwa wengi kufariki au kutafutiwa matibabu sahihi when it's too late.

Yaani unakuta mtumishi wa afya huko zahanati badala ya kumfanyia referral mgonjwa ambaye anaona kabisa ameshashindwa, lakini anajifanya yuko nondo, mwishowe anakuja kumfanyia referral mgonjwa akiwa kwenye hali tete.

Na hali hii siyo kwa madaktari pekee, ni karibia sekta nzima ya afya. Maabara ndio kabisa, yale maparasites wanaoyakariri huwa ni wachache sana.

Wajanja huwa wanafanya team up ikionekana hawaelewi elewi.

Unaweza kuambiwa una ugonjwa fulani kumbe siyo.

Ukiona unatibiwa hupati unafuu ujue kabisa you're treating the wrong case.

Fanya vipimo maabara hata 5 ili uwe na uhakika.

Na madaktari walivyo, unakuta mtu kakariri tu cases ambazo ni common eneo husika kama Maralia, Typhoid, UTI,

Ikitokea rare disease tayari anakuwa hajui chochote cha kufanya. Ndio maana unakuta mtu ana dengue fever kawa diagnosed ana Maralia.

Mpaka ihe kujulikana haikuwa Maralia it's too late.
Yaani acha tu, umeandika kama umewahi kupitia hii misukosuko

Kuna kipind kidogo nimpoteze mana kwa huu ujinga
 
Ungetoa na mfano wa hospitali tujue ukubwa wake..

Maana kuna vihospitali vya mitaani tabibu(Clinical Officer) anaachwa kama ndo final say huku elimu yake ikiwa ndogo,na watu huwa wanawaita ni madaktari..matatizo kama haya lazima yatokee..

Note:I don't mean to offend those clinical officers
 
Msi-generalize jamani. Not all. Kuna madaktari wanabaka fani. Mf mtu hajasomea Radiolojia Ila anajifanya kutafasiri Sono au picha za MRI, tegemea anguko na ramri za kipuuzi.

Dr hajasomea Pharmacy vzr Ila anajifanya anajua dawa zote duniani. Medical field is too wide, let us accept our niches where we are expert at!
 
Sitetei ujinga mkuu.
Hizo case hutokea Mara chache hata Mimi imewahi nitokea daktari alikosea kung'oa jino..akang'oa lisilo na tatizo lenye tatizo likaachwa..lakini huyo ni daktari bingwa anayewang'oa watu vizuri miaka na miaka..daktari ni binadamu pia,hayupo perfect muda wote.
Narudia tena acha kutetea upumbavu.
 
Madaktari ni binadamu na kila mmoja ana uelewa wake anapokuwa Darasani.

Siyo kila daktari anajua, wengine ni vilaza tu.

Ila tatizo kubwa kwetu kama watanzania ni ugumu wa kukiri jambo fulani silijui au nimeshindwa.

Hali hii imesababisha wagonjwa wengi kufariki au kutafutiwa matibabu sahihi when it's too late.

Yaani unakuta mtumishi wa afya huko zahanati badala ya kumfanyia referral mgonjwa ambaye anaona kabisa ameshashindwa, lakini anajifanya yuko nondo, mwishowe anakuja kumfanyia referral mgonjwa akiwa kwenye hali tete.

Na hali hii siyo kwa madaktari pekee, ni karibia sekta nzima ya afya. Maabara ndio kabisa, yale maparasites wanaoyakariri huwa ni wachache sana.

Wajanja huwa wanafanya team up ikionekana hawaelewi elewi.

Unaweza kuambiwa una ugonjwa fulani kumbe siyo.

Ukiona unatibiwa hupati unafuu ujue kabisa you're treating the wrong case.

Fanya vipimo maabara hata 5 ili uwe na uhakika.

Na madaktari walivyo, unakuta mtu kakariri tu cases ambazo ni common eneo husika kama Maralia, Typhoid, UTI,

Ikitokea rare disease tayari anakuwa hajui chochote cha kufanya. Ndio maana unakuta mtu ana dengue fever kawa diagnosed ana Maralia.

Mpaka ihe kujulikana haikuwa Maralia it's too late.

Good answer.
 
Upo sawa sawa nishapigwa wrong treatments mara nyingi sana nikaja kugundua ninachoumwa google huko, hapo nishapigwa pesa almost miezi 9 halafu siponi.
 
Dah. Yani kuna shida kubwa sana kwenye idara ya afya. Dada yangu alikua akilalamika sana maumivu ya tumbo..

Nikamshauri aende kwenye vipimo
vya ultrasound, sasa alivyoenda kwa maelezo yake , yule aliyekuwa anamchukua video alimchukua muda mrefu sana akawa anasema mbona kila kitu kipo sawa.

Sasa kwenda kwa daktari, anamwambia eti umeonekana una maji kwenye kizazi inabidi ulipie dawa za 70,000 ukatumie.

Sasa alivyoniletea taarifa mimi nikashangaa, inakuaje mchukua video asione kitu halafu doctor aseme una maji kwenye kizazi.

Mwisho wa siku, tuliongea na dr mwingine akamshauri sister aache kutumia vidonge vya majira. Mpaka leo miaka 3 sister hajawahi kulalamika tena. Kumbe yule Dr alitaka kutulia 70,000 zetu.
 
Hata mimi siku hizi uwa nikipata tatizo ninaanzia google au hata nikienda hospital nikiambiwa kitu narudi pia google kujisomea
 
Dah. Yani kuna shida kubwa sana kwenye idara ya afya. Dada yangu alikua akilalamika sana maumivu ya tumbo..

Nikamshauri aende kwenye vipimo
vya ultrasound, sasa alivyoenda kwa maelezo yake , yule aliyekuwa anamchukua video alimchukua muda mrefu sana akawa anasema mbona kila kitu kipo sawa.

Sasa kwenda kwa daktari, anamwambia eti umeonekana una maji kwenye kizazi inabidi ulipie dawa za 70,000 ukatumie.

Sasa alivyoniletea taarifa mimi nikashangaa, inakuaje mchukua video asione kitu halafu doctor aseme una maji kwenye kizazi.

Mwisho wa siku, tuliongea na dr mwingine akamshauri sister aache kutumia vidonge vya majira. Mpaka leo miaka 3 sister hajawahi kulalamika tena. Kumbe yule Dr alitaka kutulia 70,000 zetu.
Duh ni hatari kwakweli
 
Kuna jamaa aliwahi kuugua na kutafuta suluhisho zaidi ya hospitali 10.alinzia hospitali kubwa kushuka chini

1.Kila hospitali haikubali vipimo vya hospitali nyingine ulioanzia lazima wakupime upya na majibu yanakuwa tofauti

2.Alikuja kupata suluhisho kwenye hospitali mdogo kabisa

3.Unashauriwa uwe unacheki afya yako mara kwa mara lakini ukienda hospitali ukakuta foleni ya wagonjwa na matatizo makubwa walionao utapanga foleni wewe mzima kweli?
 
Usomaji wetu ni shida eti unapewa picha ya tatizo hata haina muonekano mzuri afu unaambiwa huyo sijui ni parasite gani wakati picha inaonesha ukungu tu,mwisho wa siku tunaishia kukariri
Umeongea Cha maana Sana, elimu yetu ni ya kukariri hata waliotufundisha walikaririshwa
 
Kuna jamaa tumekua nae mtaani babake alikuwa anamiliki duka la madawa,basi yuke mzee akawa anatamani mwanae aje kuwa daktari ingawa mwanae ni kilaza na masomo ya sayansi yalikuwa hayapandi.

Jamaa akawa ana shughuli ya kurisiti ili aendane na ndoto za mzee wake.

Mwishowe jamaa nasikia alifanikiwa kuwa daktari kwa njia walizozijua wao.

Nawasalimu wagonjwa wote wanaoendelea kukutana na daktari huyu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom