Hivi kweli uchawi upo?


Tatizo mkuu hatuelewani kwa sababu unanipeleka ambapo mie sipo. Haya madai ya kuwepo uchawi tumezaliwa na kuyakuta,sasa wewe pia unadai kuwa hakuna huo uchawi ambao watu wanadai kuwa upo.

Kwahiyo mie nilichotaka kwako ni sababu zilizokufanya kuona hili jambo la kuwepo uchawi si la kweli na ndiyo maana ukasema hakuna uchawi,maana umepinga madai ya kuwepo uchawi hivyo lazima utakuwa na sababu zilizokufanya ukatae hayo madai ya kuwepo uchawi na ndiyo hicho nachotaka.

Hivyo sio kwamba mie nataka ueleze kwanini hakuna uchawi kama ulivyosema.
 
Mkuu, embu nieleweshe,
Hivi? 'kuelezea sababu zinazofanya kwamba jambo la uchawi sio kweli' na 'kuelezea kwanini hakuna uchawi' ni mambo mawili tofauti?

"Kwanini" "kwasababu"
 
kwani wewe unadhani uchawi ni nini... ili tueleweshane
 
Mbona hatuuoni
Kwani akili zipo? Mbona hatuzioni?
[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]

nafight with my weather[emoji23][emoji23]
 
Mkuu, embu nieleweshe,
Hivi? 'kuelezea sababu zinazofanya kwamba jambo la uchawi sio kweli' na 'kuelezea kwanini hakuna uchawi' ni mambo mawili tofauti?

"Kwanini" "kwasababu"
Unapaswa ufahamu kuwa anachokifanya yeye hapa ni kupinga madai ya kuwepo uchawi hivyo lazima atakuwa na sababu zilizofanya apinge kuwepo huo uchawi ambao watu wanadai kuwa upo, sasa mie nataka kuzijua hizo sababu zilizofanya apinge kuwepo huo uchawi ambao watu wanadai kuwa upo.

Sasa yeye anaposema kuwa hawezi kueleza sababu za kutokuwepo uchawi inakuwa kama anamaanisha kuwa mie nimeibuka tu na kuanza kumwambia aeleze sababu za kutokuwepo kitu ambachohata hata yeye hakijui,si hivyo bali mie nimemuomba aeleze sababu za kupinga madai kuwa hakuna uchawi.
 
Facts [emoji115] [emoji106] [emoji106]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bufa, sio vitu vya kusadikika, kama haujapatwa tafuta mtu aliyelogwa akueleze. Sasa unapingana na Biblia na Msahafu? Yesu hakuondoa mapepo? Umeshawahi kufanya biashara kwa kuzingatia kanuni zote lakini pesa haionekani? Uchawi upo sema watu wanautumia vibaya badala ya kujilinda. Ukiambiwa utalogwa kimbia haraka kajilinde kulingana na imani yako. Nimeshapatwa hivyo naongea kwa kujiamini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nenda misungwi ukaone fisi wanabatizwa nahisi utapata kwa kuanzia utafiti wako
 
Kuna mtu kasema haamini huu upuuzi! Basi ukiamini Mungu yupo ni upuuzi, haonekani na uchawi hauonekani. Uchawi ni ushetani wa aina yake, kwa kua unaamini Mungu yupo na shetani yupo basi uchawi ni sehemu ya shetani, kwa hiyo uchawi upo. Labda unaekataa ujaribiwe kidogo tu usipotamani ardhi ipasuke uingie humo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…