Hivi kweli tumefika huku??

Like seriously. .waweza kukuta jamaa alikuwa na business ideas. .Lakini ikawa ana kwama kupata capital. ..so imejitokeza opportunity kama hiyo Unadhani angeiacha Thubutu '' Hata wewe usingediriki kufanya hivyo' .....

Ila kumuacha dahh!!! Hakufanya vyema amemkatili sana ''Ijapokuwa huyo dada Alifanya unyama mkubwa sana kwa mumewe. ...so let's assume kuwa hayo ni maamuzi ya Fate ''so Pali kuwa hakuna namna ya kuepusha hayo yasiweze kujiri
Angemuacha tu,bila kumdhulumu pesa zake nyingi....
 
Unaweza kuta huyo dada kajitungia tu story ili safari iwe fupi au ili msimtongoze mpaka amefika mwisho wa safari yake kawaacha madume matatu bado mnafikiria hadithi yake...yeye kaenda zake kwa mumewe.
 
Kabisa ni Ujinga mkubwa ...imagine hapo kama alizaa na mumewe. ..wakati huu itakuwa ana wa pitisha watoto wake kwenye hali ngumu kwaajili ya Ujinga wake ...
Yawezekana hata wa darasa la saba asifanye alichofanya yeye
 
Ujue namfahamu vizuri huyo dada. Ni kweli yupo humu na ni mchangiaji mzuri wa JLW. Na mimi ni yule dereva wa lile gari ulilopanda.

Sema nini mwanangu hujafanya poa kusimulia hiyo story humu jukwaani. Hapa mabaharia wote waliosoma hiyo simulizi wameazimia kukuvua vyeo vyote vya kibaharia.
 
Unaweza kuta huyo dada kajitungia tu story ili safari iwe fupi au ili msimtongoze mpaka amefika mwisho wa safari yake kawaacha madume matatu bado mnafikiria hadithi yake...yeye kaenda zake kwa mumewe.
Noup,kwa saikolojia ndogo sana unamjua mtu anayesimilia hadithi ya kusadikika na anayeeleza uhalisia,ukienda msibani hauhitaji kuelekezwa wafiwa,(utawajua tu)

Huyu dada alichokuwa anatafuta ni huruma tu,kwa sababu dereva alikuwa anaelezea yaliyompata kwenye ndoa yake (ya kusikitisha sana)

Dada akaanza kufunguka kuwa wanaume ni mashetani zaidi,kufuatia kudhulumiwa na mtu aliyedai "alimpenda sana" akisahau kuwa yeye alikuwa shetani zaidi kwa mume wake!

Na "facial expression" yake unagundua ni mtu anayepitia majuto sana kutokana pengine na akiyofanya,angekuwa anasogeza story ilikuwa easy sana kujua!

Lakini kubwa zaidi,hakuna hata mmoja aliyekuwa na mambo ya kihuni mle ndani,sikuona hata jicho la kukonyeza hata dereva alionekana wazi kuwa mwenye busara zake

Hivyo mdada hakuwa hata na sababu za kujihami kiasi cha kufikiria story kama hivi
 
Bahati nzuri ni kwamba mimi sio mwanachama wa hiyo kitu mnaita "baharia" kwa sababu sijawahi hata kuelewa mnamaanisha nini?

Pili kusimulia ni kuwafanya wengine wajifunze, (wanawake wenye hulka kama ya yule dada) wasije sema hatukuwaambia,wanaweza kujitoa kwa wapenzi wao na kuwapa kadi zao za bank,lakini matokeo yake ni kama hayo...

Yaani in short ni kwamba tunajifunza kutokana na makosa ya wengine,kama kweli ni wewe dereva basi utakubaliana nami kwamba kwa hali ile mdada anahitaji kufanyiwa counseling ya nguvu sana ili aishi miaka aliyopangiwa na Mungu wake,vinginevyo atakufa siku si zake...
 
Kuna siku jilikuwa natoka dodoma, nikachukua abiria wanne waliokuwa wanaenda moro, wakaka 3 na mdada mmoja, ile safari ilikuwa fupi sana,tulijikuta kila mtu akihadithia matatizo yake ya mahusiano, yaani asilimia kubwa ya watu wana matatizo sana kwenye mahusiano japo tunatofautiana sana katika kuyakabili
 
Jamabi Mungu kama ameamua kumpa fundisho huyo dada aliyekuwa anasaliti ndoa yake jamaa (mzinzi mwenzake) angeweza kupinga mpango wa Mungu kweli???

Maana mimi najiuliza maswali mengi sana lwenye hilo
Ni mduara, huyo nae zamu yake itafika ya kupewa fundisho..
To every action there is a reaction.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…