Hivi kweli tumefika huku??

Hivi kweli tumefika huku??

Salaam wanajukwaa!

Jana nikiwa safarini natoka mkoani kurejea Dar-es-salaam,tulisafiri watu kama wanne hivi,mdada mmoja wa makamo,na wanaume 3,wote hatukuwa tunafahamiana. Lakini kama ujuavyo safari ikiwa ndefu sana,story huwa kitu cha kawaida.

Basi baada ya kimya cha muda mrefu,dereva akaanzisha story za hapa na pale,akajikuta anasimulia habari ya maisha yake ya mahusiano,na kumtuhumu mkewe namna alivyokuwa akitoka na wanaume wengine,walivyoachana na baadaye kurudiana,(ni story ndefu sana ya huyu jamaa lakini sitaieleza sana hiyo,japo jamaa alipita nyakati ngumu sana)

Kilichonifanya niandike hii mada ni huyu dada abiria mwenzetu,alivyojiachia kusimulia mikasa yake na namna alivyomuanika mumewe (japo ni kweli hatumjui mume wake,lakini hapana...)

Anaanza kwa kulaumu wanaume namna tulivyo wadanganyifu,nikichoka alipokuwa akielezea udanganyifu huo, anaanza!

"Mimi nimeolewa miaka 9 iliyopita,mume wangu alikuwa na udhaifu sana kitandani,nilivumilia miaka 4 nikashindwa,nilitafuta mwanaume mwingine,hakuwa na kazi,nilimsaidia sana yule kaka, huwezi amini nilikuwa namuibia mume wangu pesa,nampelekea huyu mwanaume aanze biashara,wakati anatafuta kazi,maana alikuwa amesoma...

Nilichukua mkopo bila mume wangu kujua,milioni 25 nikamwambia tujenge nyumba mkoa jirani,ili ikiisha tuhamie huko,mimi nimuache mume wangu (hapo watu wote kwenye gari tupo kimya tunamsikiliza kwa makini,moyoni nikiwa najisemea,masikini dada anaonyesha namna alivyo mjinga)

Anasema jamaa akaenda kununua kiwanja na kujenga kingolwira Morogoro,jamaa akamwambia nyumba imefikia level nzuri tu,ila pesa imeisha,bado finishing na fensi. Bila aibu mdada anajisemea " Nilimzunguka mume wangu, saving account yangu ambayo mume alikuwa anaijua ulikuwa na milioni 18,nilichukua ile pesa yote nikampa mpnz wangu amalizie fensi.

"Cha ajabu baada ya nyumba kukamilika nilimwambia anipeleke niione ili nitafute namna ya kuachana na mume wangu,alianza kunipiga chenga,nilimuomba pesa mume wangu Milioni tano niende kijijini kwetu kwa ajili ya kumalizia nyumba ya wazazi,akanipa,tukaenda na mpnz wangu Zanzibar ili niongee naye vizuri,na nilijua ninachofanya makusudi ili mume wangu anifukuze"

"Basi mume wangu alivyojua kuwa sikwenda kijijini alikasirika sana,akaniambia niende kwetu nikapumzike,nikafurahi sana nikijua ndo tiketi ya kwenda kuanza maisha na mpnz wangu,maana nyumba tayari tulikuwa nayo na alikuwa ameshapata kazi..."

"Wanaume mlivyokuwa na roho mbaya,yule kaka kumbe alikuwa anajenga Dar,na alikuwa na mwanamke mwingine,anampeleka kumuonyesha nyumba hiyo hiyo na kumwambia wakioana ataishi naye hapo,haki ya Mungu nilisikia roho inatoka....(khaaaa)

Analalamika kuwa jamaa aliingia mitini,mdada mpaka sasa ameachana na mume wake,na mkopo bado anaendelea kulipa na amepanga kimara chumba na sebule,na anamlaani mpnz wake aliyemdanganya kuwa akiachana na mume wake yeye atamuoa...

Hakika maisha haya yana mengi,mahusiano na ndoa... Yamejaa visa na mikasa,mengi ya kujifunza. Baada ya dada kushuka kimara watu wakamsema sana kwa kumtukana "mpumbavu bora hata asisimulie" wasijue atakuwa mgonjwa mahututi kisaikolojia,kutokana na ulevi wa penzi...hivyo kusimulia kunamfanya angalau apate nafuu

Dada kama uko hapa jukwaani ninakupa pole,lakini pia samahani kwa kuweka story yako hapa,inaweza kuwasaidia wengine wanaotaka kukimbia ndoa zao ili wakaishi na wapenzi wao kwa kigezo cha waume kutowafikisha vileleni,tafuteni namna nyingine ili waume zenu wawe bora kuliko kukimbilia nje,kuna madhara makubwa sana.
Mwingine juzi tu kalizwa milioni 2 aliunda joint account na mchepuko na amezaa mtoto nje wa kiume mme naye kawadukua hivyo kwa sasa mke yupo kwao kaacha watoto watatu mme analea yeye yupo na kichanga cha mchepuko na ana maisha magumu mno.
Kweli wanaume macho mengi lakini kwa mwenendo wa sasa mtaachika sana kwa tamaa ya mapenzi.
 
jinga san ahilo...yani anatoana aache ndo kazame kwa vitu asivoweza...duh anafanya usaliti wa ndoa akidhani yuko salama n aujenzi huo bandia
 
Hizo million 25 alizokopa zingetosha kabisa kutibu tatizo la huyo mumewe na chenji ingebaki.
 
Huyo kidume KWELI Alijua kuna SIKU na Yeye atasalitiwa kama alvyosalituwa mwanaume mwenziwe mamaa sasa VUNA ulicho panda
 
Back
Top Bottom