Hivi kweli TRA wana nia njema na nchi yetu?

Kaduguda

JF-Expert Member
Aug 1, 2008
724
641
Kampuni za mizigo bandarini Dar zalalamikia ushuru mpya

Na Leon Bahati

KAMPUNI zinazotoa huduma ya kupakua na kupakia mizigo (forwarding and Clearing) Bandari ya Dar es Salaam zimegoma na kusababisha hofu ya kuzuka kwa mkanganyiko wa uchumi nchini

Pamoja na kugoma, kampuni hizo zimedai zinafikiria kuitumia Bandari ya Mombasa nchini Kenya katika kupakua na kupakia mizigo ya kibiashara.

Habari zilizolifikia gazeti hili zilisema baadhi ya kampuni hizo zinatishia kuondoka Dar es Salaam baada ya Serikali kupandisha ushuru kwa karibu asilimia 50 tangu Jumatano iliyopita.

Baadhi ya wamiliki wa kampuni hizo , waliliambia Mwananchi Jumapili kuwa serikali imebadili mfumo wake wa kutoza ushuru wa forodha ambapo kila kontena linatozwa kati ya Sh20 milioni na 40 milioni, bila kujali aina ya mzigo uliopo ndani.

Lakini mchumi mmoja , alisema jana kwamba wakati wote mfanyabiashara akiongezewa gharama, basi atakayeumia ni mlaji (wananchi).

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Hamfrey Mushi alisema katika mazingira hayo, ni vigumu kupambana na mfumuko wa bei.

Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina gazetini, baadhi ya wenye kampuni walidai, awali walikuwa wanalipa ushuru kulingana na thamani ya bidhaa zilizopo ndani ya kontena.

Lakini mfumo mpya, uliobuniwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) unatoza Sh 20 milioni kwa kila kontena lenye urefu wa futi 20 na Sh.40 milioni kwa kila kontena lenye futi 40.

Bila kuangalia thamani.

Mwananchi Jumapili lilipowasiliana na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo alisema kuwa yupo safari ya kikazi, Kilosa Morogoro, na kushauri kuwasiliana na Katibu Mkuu wa Wizara, Ramadhan Kijja.

Hata hivyo, Kijja hakupatikana kupitia simu yake ya mkononi na hata ile ya ofisini kwake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

Mkurugenzi wa Elimu kwa walipa Kodi na Uhusiano wa TRA, Protas Mmanda naye hakupatikana ili kufafanua juu ya jambo hilo baada ya simu yake nayo kutopokelewa.

Pamoja na hali hiyo, habari zilizolifikia gazeti hili zilieleza kuwa baadhi ya watendaji wakuu wa TRA walikuwa kwenye vikao mwishoni mwa wiki ili kujadili hatma ya mgogoro huo.

Bandari ya Dar es Salaam imekuwa ikishutumiwa kutokana na utendaji usioridhisha wa Ticts, ambao unasababisha foleni kubwa ya meli zinazosubiri kupakuliwa.

Waziri wa Miundombinu, Dk. Shukuru Kawamba alisema kuwa hali hiyo imekuwa ikisababishia serikali hasara ya Sh20, milioni kila siku kwa kila meli.

Wakizungumzia juu ya utendaji mbovu wa bandari hiyo pamoja na kuongezeka kwa gharama pamoja na ushuru wa forodha, wataalam kadhaa wa uchumi walisema athari zake ni kubwa kwa uchumi na kwamba zitaongeza ugumu wa maisha hasa kwa wananchi wa kipato cha chini.

Aliitaka serikali kuchukua hatua za haraka za kupambana na hali hiyo vingionevyo, hali ya uchumi wa nchi itaendele kudorora na hali ya maisha itazidi kuwaendea vibaya watu wa kipato cha chini.


SOURCE: MWANANCHI - 2/21/2009

My take: Naomba wadau mnieleweshe hivi inakuwaje container lilipiwe ushuru flat rate, maana hata maji ya DAWASCO siku hizi kuna meter unalipa kwa kadri unavyotumia. Sasa mtu kaleta container kisha unasema ni flat rate hii wadau imekaaje? JF kuna wadau wa aina zote hebu ,lio TRA mtuambie kulikoni hata mkafikia maamuzi hayo?
 
Kaduguda, ukisikia hii ni serikali ya vihio ndio hiyo. Mi nadhani wakapimwe akili tunaweza walaumu kumbe baadha ya fyuzi vichwani mwao zilishakatika. Nimeshawahi changia sana juu ya mfumuko wa bei Tanzania, malengo na mikakati ya kufanikisha malengo hayo. Serikali hii inalengo la kushusha mfumko wa bei kuwa 7.5% by jun 2009 pia malengo yaliyopo ni kwamba uchumi utakuwa (of course najua wanafanya finacial engineering hatakama mambo hayapo hivyo basi dada tutakazo pewa ni kwamba uchumi umekua hata kama kuna recession).

Kwakifupi hii inaitwa 'import tariff restriction', hata hivyo haina basis (crazily done). Kama tunataka kuzuia uagizaji bidhaa nje ya nchi tunatakiwa kuwa na alternative domestic supply ya bidhaa hizo. Hata hivyo huwezi kuwa na flat rate bali kupandisha rate kwa kiasi fulani kwa aina fulani ya bidhaa unazotaka kuzuia uagizaji wake toka nji ili kulinda soko la ndani. Sasa sisi tunabidhaa gani hapo kama mbadala?. Au ndio wanatekeleza agizo la mwanye nyumba sikasha watembelea hao au bado?.
 
Mara nyingi tasisi zetu huususan TRA huwa wanatangaza viwango vipya kupitia kwenye bajeti sasa hii mbona haiko sawa? Kuweka tarifss haphazard namna hii ni uvurugaji wa uchumi. Hakika lazima TRA na Wizara ya Fedha iwaeleze wananchi kuhusu hali hii. Mimi inanipa wasiwasi kuwa uchaguzi unakuja mambo kama haya utayasikia sana. Ingawa kweli ataumia mlaji wa mwisho lakini "wao" watakuwa wamepata wanachokitaka irrespective of the fact anaeumia ni mwananchi wa hali ya chini. Hakuna mantiki ni WIZI MTUPU!!!!!
 
Walipa kodi wakubwa Tz ni walewale wakianzia wafanyakazi ambao hutozwa kodi kubwa kuliko. TRA wanajidai eti wanajiwekea malengo ya ukusanyaji wa kodi kumbe wanachokifanya ni kuwabambikia watu kodi . Hawana tofauti sana na baadhi ya Polisi . Wakesha kubambikia wanakuamuru ulipe 1/3 ya hiyo amount kwanza ndio maelezo au makubaliano yafuate. Wanaangalia upande mmoja tu kama nyati wakasahau efeect yake kwa uchumi in general.

Halafu nijuavyo mimi kodi nyingi huongezwa wakati wa bajeti. Je kuweka viwango vipya bandarini imezingatia hilo? Nani ana aprove mambo hayo. Kama ni bunge basi linapaswa kuact.
 
Jamani;

Kabla ya kulaumu tuangalie sana... Yawezekana haya ni maagizo ya wakubwa kutokana na hali ya uchumi au maandalizi ya uchaguzi

The bottom line ni kwamba - kuna viazi katika level zote hapa nchini ambao wanaweza kuamua chochote popote bila kujali yeyote... hadi yaharibike ndio watengue maamuzi

Watch this one
 
Jamani;

Kabla ya kulaumu tuangalie sana... Yawezekana haya ni maagizo ya wakubwa kutokana na hali ya uchumi au maandalizi ya uchaguzi

The bottom line ni kwamba - kuna viazi katika level zote hapa nchini ambao wanaweza kuamua chochote popote bila kujali yeyote... hadi yaharibike ndio watengue maamuzi

Watch this one
 
Kama ni kweli basi Tanzania sasa inaendeshwa kama Somalia(kwa style ya ransom), hawa watu wanaojiita wachumi na wamebobea katika masula haya inakuwaje leo hawazingatii kanuni walizojifunza darasani?.

Unapofanya flat rate katika kulipia container kwanza ni kinyume cha sheria za kodi zilizopo kwa sasa, labda watuambie kuna sheria mpya imepitishwa na bunge. Japo sheria zinampa uwezo Commissioner of Domestic revenue kutumia uwezo wake katika kufikia kadirio analodhani yeye kuwa ni thamani ya mzigo, bado flat rate ni misuse of that clause na anatakiwa kupimwa akili kama kweli ana sound mind katika kufikia maamuzi.

Mtu amekaa marekani miaka 20 anaamua kurudi nyumbani na kuchukua container anaweka makochi yake, jiko na gari alilotumia miaka kumi vyote havizidi $10,000 unamwambia alipe million 40? kweli wewe unaakili kweli?. Ok utasema ni returning resident atakuwa na exemption ila kama anataka kuja na mitambo yake ya kuanzisha biashara atafikiria hilo?. Huku ni kudidimiza uchumi mchana kweupe.

Nafikiri kuweka malengo isiwe ni kwa cost ya wananchi, waweke mazingira mazuri ya kukuza biashara na uchumi kwani ng'ombe usipomlisha hatatoa maziwa, sasa hawa jamaa wao wanataka kukamua tu kulisha hawataki sasa si wataua?. Hii ndiyo Bongo "on your own"
 
Back
Top Bottom