Hivi kweli kuna watu wanapona kwa maombi?

my name is my name

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
1,644
2,000
Mimi naamini uwepo wa Mungu namuabudu pia mfuasi wa dini fulani. Lakin kwa haya mambo ya mtu kupona kwa maombi au dua tu huwa siamini.

Inaezekana kweli zamani enzi za manabii watu walikuwa wanapona kweli kwa maombi/ dua lakin kwa dunia ya sasa sidhani kama kuna hki kitu. Yani mtu kupona ugonjwa kwa maombi tu bila kutumia dawa au vtu kama hivi.

Ulishwahi kushuhudia mtu aliepona kwa maombi tu? Sio kushuhudia kwnye tv au kuhadithiwa namaanisha kushuhudia kwa macho yko mgonjwa/ mtu alikuwa na matatizo akawa sawa kwa maombi tu?

Hapa namaanisha labda mtu ulikuwa unamuona ana struggle kwa muda mrefu baadae akaenda kwenye maombi akawa sawa. Umewai shuhudia ktu km hii?
 

Karaoke

Senior Member
Nov 22, 2019
117
250
Kama hoja ni kushuhudia wapo wengi wanaopona, lakini ni wagonjwa walioandaliwa, kiukweli labda uwe na mapepo au stress ndio maombi yanaweza kukuponyesha lakini kama ugonjwa wako ni ugonjwa halisi,hata waombeaji wote duniani wakuombee hutapona ni mpaka utumie njia halisi kama hospitali au dawa za kienyeji
 

my name is my name

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
1,644
2,000
Kama hoja ni kushuhudia wapo wengi wanaopona, lakini ni wagonjwa walioandaliwa, kiukweli labda uwe na mapepo au stress ndio maombi yanaweza kukuponyesha lakini kama ugonjwa wako ni ugonjwa halisi,hata waombeaji wote duniani wakuombee hutapona ni mpaka utumie njia halisi kama hospitali au dawa za kienyeji
So maombi yanaweza kupona mgonjwa ya saikolojia tu lakini sio magonjwa mengine?
 

chivala

Senior Member
Apr 13, 2021
101
250
Mimi naamini uwepo wa Mungu namuabudu pia mfuasi wa dini fulani. Lakin kwa haya mambo ya mtu kupona kwa maombi au dua tu huwa siamini. Inaezekana kweli zamani enzi za manabii watu walikuwa wanapona kweli kwa maombi/ dua lakin kwa dunia ya sasa sidhani kama kuna hki kitu. Yani mtu kupona ugonjwa kwa maombi tu bila kutumia dawa au vtu kama ivi. Ulishwahi kushuhudia mtu aliepona kwa maombi tu? Sio kushuhudia kwnye tv au kuhadithiwa namaanisha kushuhudia kwa macho yko mgonjwa/ mtu alikuwa na matatizo akawa sawa kwa maombi tu? Hpa namaanisha labda mtu ulikuwa unamuona ana struggle kwa muda mrefu baadae akaenda kwenye maombi akawa sawa. Umewai shuhudia ktu km hii?
Maombi yanaponesha magonjwa yale yanayoweza kutoweka bila kutibiwa
 

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
30,094
2,000
Duh! Alichukua muda kiasi gani kupona wakati akitumia maombi kama dawa? Alikuwa hatumii dawa yoyote zaidi ya maombi?
Alitumia maombi tu, Kila kitu kinawezekana kama ututumia nguvu za kiroho kupambana na nguvu za mwilini.
Unachotakiwa kuanacho ni imani, Commitment na Subira
 

airwing

JF-Expert Member
Dec 8, 2017
214
500
Wengi tu Kuna jamaa alikuwa dereva na muislamu aliletwa kanisani akiwa hawez kuamka, kuongea Wala kusikia na hajitambui hata mke wake na watoto hawajui na hajui watt Ni Nini na maana ya mke!!!
alipigwa fire maombi ya Siku 14 Tena kambi, na akaanza kupona taratibu Sasa hivi mzima anafanya Kazi Yap merkez Morogoro...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom