Hivi kweli inaingia akilini.....

TANMO

Platinum Member
Joined
Apr 12, 2008
Posts
12,145
Reaction score
12,875
kusalimiana na mtu huku macho umeyaelekeza mahali pengine?


Pichani: JK akisalimiana na Dkt Rachel Mhaville ambaye ni daktari bingwa wa meno ya watoto.
Picha: kwa hisani ya Mjengwa Blog.
 
Unaonekana hauko serious kwa huyo unayesalimiana. Inapaswa umpe tu attention yote ajue kweli unamaanisha katika salamu hizo. Sasa kama unaangalia pembeni esp kama ni mtu ambaye hamfahamiani na ndo mmeonana kwa mara ya kwanza inaleta picha mbaya kwake.
 
Unaonekana hauko serious kwa huyo unayesalimiana. Inapaswa umpe tu attention yote ajue kweli unamaanisha katika salamu hizo. Sasa kama unaangalia pembeni esp kama ni mtu ambaye hamfahamiani na ndo mmeonana kwa mara ya kwanza inaleta picha mbaya kwake.
 
naona dada wa watu amemkodolea macho Jeikei lakini mwenzake wala hana taim naye, anatimiza tu Protokali ya kuwapa mkono watu...
 
...Sioni tatizo; jamani sasa kila analofanya kikwete ni habari? hao nao wamejipanga msururu wote wa nini;It is boring to shake hands of score of people for absolute no good reason and they all expect you to give a smile si utalala na headache kila siku.....
 

Mkuu, kuwa kiongozi mzuri inabidi uwe unaweza sana ku-pretend.... Body language yako inabeba ujumbe mzito sana, Kiufupi Mhishimiwa Rahisi hakutimiza kile alichopaswa kutimiza na kwa mantiki hiyo tuna haki ya kumjadili.
 
yaani yupo mbaaali kabisa.
 
Hapana huwezi jua alichokuwa akiangalia huko pembeni!!!! Huenda aliangalia maramoja tu!!!! Tumsamehe leo mkuu wa kaya.......!!!
 
naona dada wa watu amemkodolea macho Jeikei lakini mwenzake wala hana taim naye, anatimiza tu Protokali ya kuwapa mkono watu...
hapo usikute kuna kifaa jk alikiona pembeni ndio maana alikuwa anakikodolea macho na kuwapa ishara wapambe wake wakiwinde ili akatindue amri ya 6. si mchezo jk...
 
Kwenye hii picha hakuna tatizo lolote jamani Jk yuko kawaida kabisa na tabasamu lake
 
Wakubwa hebu tuwe siriaz kidogo,tunakosoa vitu vidogo dogo sana.
Angekuwa anasalimiana nae na yupo peke yake hapo sawa ila hapo ni msururu wa watu.........na picha hii yaonesha kuwa imepigwa mwishoni mwa kusalimiana kwao na JK anamwangalia mtu anaefuata.
Maana na alieleta picha hii anataka kutuaminisha kuwa JK alimpa mkono bila hata kumwangalia.This is too much
 
Jasiri....................!
<br />
<br />
 
labda ndio kwanza anasikiliza utambulisho kisha aligeuka kumwangalia.

Picha moja tu haiwezi kueleza hali halisi ilivyokuwa
 


Sidhani kama "this is too much" kama unavyosema mkuu labda kama ingekuwa ni picha hii peke yake. Jaribu kufutailia picha zilizo nyingi huyu baba huwa hafocus kwenye yule anayemsalimia, kwa wataalamu wa Psychology hili ni tatizo na si jambo dogo kama unavyotaka kutuaminisha wewe mkuu. I respectfully disagree with you kwamba alikuwa anamwangalia anayefuata kwanini asimwangalie mtu mmoja anayesalimiana naye at a time hao wanafuata si atawaangalia anaposalimiana nao? Imagine dada wa watu kayakaza kweli macho lakini jamaa wala hayupo hapo. Tabasamu lina maana gani kama hakuna eye contact maana hilo tabasamu ni la nani sasa? Moja ya tafsiri ya kutomwangalia mtu unayesalimiana naye ni dharau na mimi sishangai kwani aina ya watu wenye uwezo kama jk wengi wana dharau sana.
 
ni daktari bingwa wa meno ya watoto..kwa hiyo ni sawa kabisa macho yalegezwe ili meno ya watoto yasilegezwe...huoni kuwa kuna link hapo?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…