Hivi kwanini?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,239
113,612
Miaka takribani arubatashara iliyopita tukakutana pale uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ivato, jijini Antananarivo kisiwani Malagasi.

Wote bado tulikuwa washababi na watanashati wenye nyuso zilizojaa furaha na bashasha.

Wewe hukuwa na shaka na usharafu wangu nami vivyo hivyo sikuwa na shaka na wa kwako.

Tumepitia mengi, njia tambarare, milima, pamoja na mabonde.

Nini kilichokusibu ghafla umebadilika? Wewe hutaki kuambiwa. Hutaki kusemwa.

Unashawishika na mambo madogo. Unashawishika na vitu vidogo.

Hivi kwa nini? Kwa nini watu hubadilika na kuwa kama siyo wao tena?
 
Miaka takribani arubatashara iliyopita tukakutana pale uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ivato, jijini Antananarivo kisiwani Malagasi.

Wote bado tulikuwa washababi na watanashati wenye nyuso zilizojaa furaha na bashasha.

Wewe hukuwa na shaka na ufarashi wangu nami vivyo hivyo sikuwa na shaka na wa kwako.

Tumepitia mengi, njia tambarare, milima, pamoja na mabonde.

Nini kilichokusibu ghafla umebadilika? Wewe hutaki kuambiwa. Hutaki kusemwa.

Unashawishika na mambo madogo. Unashawishika na vitu vidogo.

Hivi kwa nini? Kwa nini watu hubadilika na kuwa kama siyo wao tena?

kwenye bold maana yake nini?

By the way, malagasy ni lugha nchi ni madagasikara
 
Dah huwa inauma sana,ila sababu kuu ni kuwa wanakua wamechoka......wanahitaji changamoto mpya!
changamoto hizo ndo zinazoumiza mioyo yetu...wakati tunashangaa imekuaje,wao hata hawajali...
 
Sasa lipi ni lipi? Ni kwamba watu hubadilika tabia zao au mlipokutana walificha tu rangi zao?

Mtu utajuaje kuwa lipi ni lipi?

Wengi kujificha tabia zao, na kuwa vile ambavyo anafikiri unapenda awe. Ni vigumu sana kuwa mtu mwingine kwa muda mrefu.
 
Dah huwa inauma sana,ila sababu kuu ni kuwa wanakua wamechoka......wanahitaji changamoto mpya!
changamoto hizo ndo zinazoumiza mioyo yetu...wakati tunashangaa imekuaje,wao hata hawajali...

Je, ni sawa tukiyaita hayo mabadiliko kuwa ni utapeli wa kimapenzi?
 
If you feel that God is so far away, guess who moved?
My favourite quote.
Relevance yake hapa ni kuwa, huenda wewe ndo umebadilika. NN, signature yangu unaweza kuitafsiri vipi kwenye ulimwengu wa mahusiano?
 
Binadamu habadiliki, ila huficha makucha yake mwanzoni.
Watu tunapenda tujulikane kwa mazuri yetu na si mapungufu yetu.

Tukiwa wapya, naficha yote mabaya hadi nikuzowee.
 
Kwa hiyo mie nime-move???

Nadhani umetumia handheld device kubandika hili bandiko kwa sababu halina hiyo signature yako.
 
Binadamu habadiliki, ila huficha makucha yake mwanzoni.
Watu tunapenda tujulikane kwa mazuri yetu na si mapungufu yetu.

Tukiwa wapya, naficha yote mabaya hadi nikuzowee.

Ukishanizoea unaficha mazuri. Kongosho bana! Khaa!
 
Nilikuwa madagascar 1999, na hiyo ni 13 yrs ago .......

Nilifikiri ulitaka kuita jinsi wao wanavyoita nchi yao ndio maana nikakukosoa, by the way it would ave felt better kama ningekunail hata once. LOL

Hahahaaaaa huwa ni ngumu sana kuni-pin down kwenye kona maana huwa najiandaa haswa!!

Nakupa homework. Tafuta maana ya 'mfarashi'.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom