Wanajeshi wengi hasa wale wastaafu na ambao walipigana vita vya Idd Amin hawampendi kabisa Nyerere,nilisikia kwamba baada ya ile vita,serikali ya Marekani ilitoa fedha(baada ya kuona JW wamepigana usiku na mchana hadi wakashinda) kila askari aliyepigana ile vita apewe gari,ila Nyerere akataifisha hela yote kwenye bank moja iliyopo kule South Afrika,je hii ndiyo yaweza kuwa sababu haswa ya jamaa kutopendwa au kuna nyingine???mwenye details amwage hapa...@!!!
nyerere angekuwa na tamaa nahisi angekuwa milionea. Watanzania kipindi kile walikuwa hawana jeuri wala access to information kama sasa; kila kitu ni "kidumu fikra.....". Nyerere alikuwa na power ya kuwaamuru watu na wakatii..but jamaa hakuwahi kutake advantage kwa kupewa heshima kiasi kile (unless kuna ambayo siyajui).
Ila in short hilo swala kwa nyerere linanipa ugumu kidogo kulikubali. Hata swala la kupanda cheo, watu kibao wamekuwa wakubwa wa jeshi katika kipindi chake. Sema alikuwa strict na uchapaji kazi sasa hapo ndio nahisi chujio lilikuwa kali kwa mtu kupanda cheo.