Hivi kwanini viongozi na wabunge kupitia CCm hupinga jambo,halafu baadae wanakifanya?

selenga

New Member
Mar 17, 2011
2
0
Nimeshangazwa sana na viongozi na waheshimiwa wabunge kupitia CCM kupinga kwa nguvu zote suala la maandamano, lakini siku za karibuni imeriotiwa kwamba katika mkutano utakao fanyika mjini Mbeya utatanguluwa na maandamano kwa madai kuwa maandamano ni haki ya mwanachi/mwanachama.
Kinachonishangaza ni hiki kwamba, nakumbuka wakati viongozi na wabunge kptia chama cha Chadema walipokuwa wakifanya mikutano na maandamano halali kumekuwa na kelele nyingi kwamba ni uvunjifu wa amani, sasa najiuliza je huo wa Mbeya ni Uvunjifu wa kitu gani au ni nini? naomba kusaidiwa katika hili.
 
Ukiumiza sana kichwa na hawa jamaaa pasua kichwa utafa cku c zako hawanaga cha kupinga kiukweli,Mfano mzur Mansoor alichangia bajet ya Ngeleja na kuunga hoja kwa % mia then akaanza kusema ktk jimbo lake kati ya kata 13 ni kata 1 tu ndo ina umeme asa utasema timamu huyo.Kweli hii ndo TZ yetu
 
Wabunge wa magamba wako zaidi kwa maslahi yao kuliko wanachama wao wanavyofikiria. Mifano hai ipo. Wamejilundikia maposho na mishahara minene minene na bado ulafi wao unafukuta kwa kutaka kuongezewa zaidi. Kwa hiyo wanapofikia wakati wa kufanya maamuzi siku zote wataangalia maslahi yao kwanza. Na hili la umeme subiri uone litapita kiulaini kama vile sio wenyewe waliosema tofauti mwanzoni kwa sababu wana sera ya kulindana na ile wanaita "collective responsibility". Si umeona mchana wa leo wameitana??? subiri jioni hii uone kioja
 
Nimeshangazwa sana na viongozi na waheshimiwa wabunge kupitia CCM kupinga kwa nguvu zote suala la maandamano, lakini siku za karibuni imeriotiwa kwamba katika mkutano utakao fanyika mjini Mbeya utatanguluwa na maandamano kwa madai kuwa maandamano ni haki ya mwanachi/mwanachama.
Kinachonishangaza ni hiki kwamba, nakumbuka wakati viongozi na wabunge kptia chama cha Chadema walipokuwa wakifanya mikutano na maandamano halali kumekuwa na kelele nyingi kwamba ni uvunjifu wa amani, sasa najiuliza je huo wa Mbeya ni Uvunjifu wa kitu gani au ni nini? naomba kusaidiwa katika hili.
UNAFIKI UNAFIKI wao wanachukiwa waandamanaji kwenye malori na kuwapa fedha na chakula. CDM wanafuatwa na waandamanaji kwa miguu na gharama zao. The difference is clear!!
 
Hawa jamaa wanakasumba ya kuwa wao ndio wanajua tu na wao ndio waanzirishi,hawataki mwingine awe na umaarufu kuwazidi wao,hawapendi kukosolewa kabisa.
 
Chadema wanaongoza CCM inafuata

Wanasahau kwamba jana yake walipinga kitu wanachokifanya leo
 
CCM always ni ndumilakuwili, maskini hawajui wafanyalo! yaani bora pazia kuliko bendera CCM hufuata upepo tuu
 
Back
Top Bottom