Hivi kwanini Ubunge usiwe na kikomo ili kupisha mawazo mapya?

Fohadi

JF-Expert Member
Jul 24, 2020
770
2,408
Binafsi sio mpenzi wa chama chochote cha siasa japo nafuatilia siasa kwa sababu siasa ina affect sekta zingine zote za kimaisha hivyo upatikanaji au uwepo wa viongozi bora ni kitu muhimu sana kwa maendeleo. Na ili tupate maendeleo, tunahitaji mawazo mbadala kila kukicha.

Inasikitisha kuona kuna watu wamekuwa 'Monopoly' wa majimbo yao miaka nenda rudi. Na kibaya zaidi kwa miaka yote waliyosimamia majimbo bado matatizo ni yaleyale. Kuna muda unashangaa kuona mbunge amekaaa kwenye hilo jimbo kwa zaidi ya miaka 20 lakini bado kila mwaka wa uchaguzi vipaumbele vyake ni vilevile. Hii ni kwa wabunge wote wa chama tawala na upinzani.

Unakuta mtu toka uchaguzi wa 2005 kwenye jimbo lake hoja zake kuu zilikuwa MAJI, AFYA NA ELIMU. Mtu huyo huyo ndani ya jimbo hilohilo mwaka 2020 anakuja na hoja zilezile na mbaya zaidi anakuwa na nguvu ya kushinda kwa sababu amesha monopolize ile nafasi. Na usishangae 2025 panapo uhai akaja kugombea na hoja zilezile.

Ni vema ukomo kwenye hizi nafasi ukaangaliwa ili kuleta mawazo mapya. Itapendeza kama mtu atakaa jimboni kwa mihula 2 tu kama ilivyo nafasi ya urais. Iwekwe sheria kuwa hairuhusiwi mtu ambae tayari ni mbunge kugombea ubunge zaidi ya mara 2. Hii itasaidia hata watu wengine wawe na access ya kula keki ya taifa na kuwatumikia wananchi. Hii itasaidia kuondoa ile dhana iliyojengeka kuwa jimbo fulani ni la fulani.

Nawasilisha.
 
Katika demokrasia, ubunge una kikomo. Kinaitwa kura za wananchi.
Itakuwaje pale ambapo kula za wananchi ni either haziheshimiwi au hazina nguvu. Hapa si ndipo mtu mmoja anaweza kukalia kiti hadi afariki? Rejea kura za maoni za ccm mwaka jana, kulikuwa na haja gani ya wajumbe kupiga kura ikiwa tu kura zao hazikuhesimiwa?
 
Itakuwaje pale ambapo kula za wananchi ni either haziheshimiwi au hazina nguvu...Hapa si ndipo mtu mmoja anaweza kukalia kiti hadi afariki?....Rejea kura za maoni za ccm mwaka jana, kulikuwa na haja gani ya wajumbe kupiga kura ikiwa tu kura zao hazikuhesimiwa?
Kama kura za wananchi haziheshimiwi hata hiyo term limits itabaki kuwa ni stories za kuchangamsha baraza JF.

Kama umeshindwa kudhibiti uchaguzi mmoja, huwezi kudhibiti process nzima ya uchaguzi inayoongoza uchaguzi wowote.

Hapo unachosema ni kama mtu anasema kashindwa kununua gari, anataka kununua kiwanda cha kutengeneza magari.
 
Kama kura za wananchi haziheshimiwi hata hiyo term limits itabaki kuwa ni stories za kuchangamsha baraza JF...
Huoni kama term limit ikiwekwa itasaidia kuziondoa sura zilezile kila mara? na kuleta sura zingine? Maana automatically yule aliyekaa bungeni mihula miwili hataruhusiwa kugombea.
 
Huoni kama term limit ikiwekwa itasaidia kuziondoa sura zilezile kila mara? na kuleta sura zingine?..Maana automatically yule aliyekaa bungeni mihula miwili hataruhusiwa kugombea..
Cha kufanya ni kuhakikisha kura za wananchi zinaheshimiwa.

Kwa sababu, wewe unaposema term limits itasaidia kuondoa sura zilezile, kuna watu wanawapenda wabunge wao wanataka waendelee zaidi ya mihula miwili, hao ukiwawekea term limits utakuwa umewakatili.

Na hakuna ushahidi wowote kwamba wabunge wapya wana ufanisi zaidi. Hata sasa kuna wabunge wapya, sijaona ushindanishi kati ya wabunge wa siku nyingi na wapya ulioonesha wapya wana ufanisi zaidi.

Hakikisha demokrasia ya kura za watu inaheshimiwa, unavyozidisha vikwazo kwenye masharti ya uongozi, ndivyo unazidisha kuibana demokrasia hii.

Hapa naona kama vile mnatafuta shortcut.

Kwa mujibu wako, tatizo ni hili.

Kura za watu haziheshimiwi.

Kama hujatatua tatizo la kura kutoheshiwa, kwanza hutaweza kuweka term limits. Hii itabaki kuwa hadithi ya kufurahimisha baraza JF.

Pia, hata kama ukiweza kubadilisha mambo na kuweka term limits kwa muujiza, bado utakuwa hujatatua tatizo la kura kutoheshimiwa.

Hao usiowataka wakiondoka na kuweka watoto wao utalalamika tena. Utasema tumeweka term limuts, sasa wanarithisha watoto wao.

Utakuwa mtu wa kulalamika kila siku.

Kwa sababu unataka shortcut zisizotatua matatizo ya msingi, wakati hutatui matatizo ya msingi.
 
Cha kufanya ni kuhakikisha kura za wananchi zinaheshimiwa.

Kwa sababu, wewe unaposema term limits itasaidia kuondoa sura zilezile, kuna watu wanawapenda wabunge wao wanataka waendelee zaidi ya mihula miwili, hao ukiwawekea term limits utakuwa umewakatili...
Hoja maridhawa sana mkuu.

Kwa uzoefu wako na ukongwe wako katika mambo ya siasa, unadhani nini kifanyike ili kula za wananchi ziheshmiwe kitu ambacho kwa Africa nakiona ni kigumu sana labda kwa miaka mingi ijayo.

Huku kwetu Afrika na Tanzania ikiwemo, aliyepo madarakani ana uhakika wa kushinda kwa 75%..Yaani akishinda mpinzani ni habari kubwa sana...nini kifanyike mkuu.
 
Hoja maridhawa sana mkuu.

Kwa uzoefu wako na ukongwe wako katika mambo ya siasa, unadhani nini kifanyike ili kula za wananchi ziheshmiwe kitu ambacho kwa Africa nakiona ni kigumu sana labda kwa miaka mingi ijayo. Huku kwetu Afrika na Tanzania ikiwemo, aliyepo madarakani ana uhakika wa kushinda kwa 75%..Yaani akishinda mpinzani ni habari kubwa sana...nini kifanyike mkuu.
Na je,katiba mpya inayoliliwa ndo itakuwa mwarobaini wa maamuzi ya wananchi kuheshimiwa kupitia sanduku la Kura?
 
Binafsi sio mpenzi wa chama chochote cha siasa japo nafuatilia siasa kwa sababu siasa ina affect sekta zingine zote za kimaisha hivyo upatikanaji au uwepo wa viongozi bora ni kitu muhimu sana kwa maendeleo. Na ili tupate maendeleo, tunahitaji mawazo mbadala kila kukich...
Mzee LUKUVI NI MBUNGE KWA MIAKA 30 utadhani Jimbo halina Watu wengine ila yeye
 
Ukitaka hayo mawazo yako yawezekane haraka wapunguzie ule mshahara na posho zao, wataondoka bungeni wenyewe.
 
Hilo litawezekana hadi pale katiba itaporekebishwa, lakini sasa warekebisha katiba si ajabu wakawa hao hao wabunge...
 
Binafsi sio mpenzi wa chama chochote cha siasa japo nafuatilia siasa kwa sababu siasa ina affect sekta zingine zote za kimaisha hivyo upatikanaji au uwepo wa viongozi bora ni kitu muhimu sana kwa maendeleo. Na ili tupate maendeleo, tunahitaji mawazo mbadala kila kukicha...
Ninapayuka tena: "Jawabu ni Katiba Mpya".
 
Back
Top Bottom