Hivi kwanini tunakufa?

This is not fair aise!
Itoshe
Dah wakuu, sasaivi apa nlikuwa natembea tembea, mara ghafla nyumba jiran nasikia watu wazima wanalia kama watoto.

Haina hata haja ya kuuliza unajua tu nini kimetokea, Hivi kwanini tunakufa?
Yani unazaliwa ili ufe?

Mungu kwanini asingeweka hata alternative jamani? Mimi wazazi wote wapo ila huwa nawaza sana zamu yangu kuwalilia!

Kama sio mimi kuwalilia wao basi wao watanililia mimi, ila kulia haikwepeki.
Nini maana yake? Kwanini lakini?Aaaarghhhhhh Aaaaaaaaarggggh
This is not fair aise!
Tu kusema uzi tyr.......unauliza kwanini kuna kufa??
 
Sasa mtu kama Championship asipokufa kuzimu ataendaje?
Anahitajika sana akashughulikiwe
My Lord and saviour Jesus Christ went there for me. Kila mwanadamu anastahili kwenda kuzimu lakini ukombozi upo kwa kila atakayeamini kile Yesu alifanya msalabani.

My future is certain in Christ. Yesu alikufa na akafufuka ili mimi niweze kuishi. Siku inakuja ambapo sisi tulioweka imani na tumaini letu kwake tutakuwa na asubuhi iliyo njema, siku ya unyakuo.

Oh upendo wake ni wa milele na upo kwa ajili yako. Neema yake ipo kwasasa lakini siku inakuja itakuwa imepita. Njoo kwa Yesu njoo ili uwe kiumbe kipya, ya kale yote yatapita, tazama yatakuwa mapya.
 
Katika ndoto ambazo binadamu atatimiza kwa 100% basi kifo namba moja.Mkuu haipo nafsi duniani ambayo haigopi kifo na haipo nafsi ambayo itakikwepa kifo .Kifo ni kama kiumbe kimeumbwa kama sisi isipokuwa hakionekani na wala hakizai.
Kitampitia kila mmoja wetu aliye hai cha msingi kwa imani yako kumuomba Mungu kikukute mazingira salama.
 
Kunatisha zaidi kufukiwa ardhin halaf pumzi kukata ee Mola atusaidie tuwe na mwisho mwema vifo visiwe vya uchungu ,sipendi kufa au watu kufa
Ukiwa unatenda mema hapa duniani, huwezi kuogopa kifo; kifo utakichukilia kama kuhama sehemu moja na kwenda sehemu nyingine. Na huko unakohamia kuna maisha mazuri zaidi ya haya hapa duniani. Tunaogopa kifo kutokana na kutojiamini na maisha yetu hapa duniani na kutojua maisha ya kule tunakokwenda.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom