Hivi kwanini Tanzania hatunaga Postal Codes?

LUBEDE

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
4,322
Reaction score
6,700
Wakuu hivi kwanini Tanzania hatunaga anuani za uhakika za miji yetu na majumbani mwetu zaidi ya namba za simu tu?

Hivi Serikali haioni kama inatucheleweshea maendeleo na kutupa ugumu wa kufanya biashara kimataifa?

Wanatuzidi hadi Uganda jamani. Kama nchi ifike kipindi tubadilike, kununua kitu mtandaoni Tanzania unatumia nguvu nyingi sana, lazima uwe mjanja mjanja sana, kinyume na hapo utaambulia kucheza na bidhaa za kichaga tu, smh!
 
Nani kasema hazipo? Kama huijui post code yako basi ingia kwenye tovuti ya TCRA utaipata.

Pia kuna kitu kinaitwa Plus code (hii ni google location code)
 
Tanzania tumekataa kupima miji na makazi na kuacha ujenzi holela.

Bila kuwa na mipango miji katika makazi hatuta songa mbele kimaendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Mfano,Miji ikiwa imejengwa kwa kufuata ramani ya mji inakuwa rahisi kusambaza huduma za maji,umeme, kuwezesha ardhi kuwa dhamana ya kukopea benki.

Usichangae kwa makazi holela inakuwa ngumu kutengeneza anuani za mitaa"postal code"

Tatizo viongozi wanajua umuhimu wa kuwa na upimaji, lakini wameacha ujenzi wa makazi holela kwa sababu wananchi ni " wapiga kura",yaani kwa mitazamo hii tutachelewa sana.
 
Kuna baadhi ya maeneo Tanzania yenye Postal Codes e.g Arusha (23100) ,Dar es Salaam(537) ya Arusha ilizinduliwa toka 2010
 
Tanzania tumekataa kupima miji na makazi na kuacha ujenzi holela.

Bila kuwa na mipango miji katika makazi hatuta songa mbele kimaendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Mfano,Miji ikiwa imejengwa kwa kufuata ramani ya mji inakuwa rahisi kusambaza huduma za maji,umeme, kuwezesha ardhi kuwa dhamana ya kukopea benki.

Usichangae kwa makazi holela inakuwa ngumu kutengeneza anuani za mitaa"postal code"

Tatizo viongozi wanajua umuhimu wa kuwa na upimaji, lakini wameacha ujenzi wa makazi holela kwa sababu wananchi ni " wapiga kura",yaani kwa mitazamo hii tutachelewa sana.
Kila sehemu Tanzania ina post code hadi eneo la kata unayoishi. Tumia simu yako kujua hilo. *152*00#
 
Wakuu hivi kwanini Tanzania hatunaga anuani za uhakika za miji yetu na majumbani mwetu zaidi ya namba za simu tu?
hivi serikali haioni kama inatucheleweshea maendeleo na kutupa ugumu wa kufanya biashara kimataifa?
wanatuzidi hadi Uganda jamani..kama nchi ifike kipindi tubadilike,kununua kitu mtandaoni Tanzania unatumia nguvu nyingi sana,lazima uwe mjanja mjanja sana,kinyume na hapo utaambulia kucheza na bidhaa za kichaga tu,smh!
Tatizo lako hausikilizi taarifa za habari na haufuatilii matangazo yanayotolewa na serikali. Wakati mchakato wa Post Code unaanzishwa namba za nyumba zote zilibadilishwa na mitaa iliwekwa majina pia isiyokuwa na majina wananchi tuliombwa tupeleke majina tunayotaka ya mitaa yetu.

Bahati mbaya hatukujali hivyo tumebaki na mitaa isiyo na majina! Bila jina la mtaa Post Code haifanyi kazi, na mbaya zaidi mitaa iliyowekwa majina watu waling'oa vibao. Nakushauri kabla ya kuweka Post jitahidi kupeleleza kuhusu unachotaka kuandika.
 
Tatizo lako hausikilizi taarifa za habari na haufuatilii matangazo yanayotolewa na serikali. Wakati mchakato wa Post Code unaanzishwa namba za nyumba zote zilibadilishwa na mitaa iliwekwa majina pia isiyokuwa na majina wananchi tuliombwa tupeleke majina tunayotaka ya mitaa yetu, bahati mbaya hatukujali hivyo tumebaki na mitaa isiyo na majina! Bila jina la mtaa Post Code haifanyi kazi, na mbaya zaidi mitaa iliyowekwa majina watu waling'oa vibao. Nakushauri kabla ya kuweka Post jitahidi kupeleleza kuhusu unachotaka kuandika.
Binafsi sijaelewa
 
Nitajie post code ya Buza kwa Mpalange

1608091534032.png
 
Binafsi sijaelewa
Hautaelewa kwa sababu haukutaka kufuatilia matangazo ya TCRA, TCRA ilitoa matangazo na barua kwa wamiliki wa majengo kushiriki mchakato wa kuboresha mitaa kwa kushauri majina ya mitaa yao, wapo walioshiriki lakini wengi hatukutaka kushiriki, sasa nani alaumiwe!
 
[emoji848][emoji848][emoji848] hii habari mpya kwangu.
 
Tanzania tumekataa kupima miji na makazi na kuacha ujenzi holela.

Bila kuwa na mipango miji katika makazi hatuta songa mbele kimaendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Mfano,Miji ikiwa imejengwa kwa kufuata ramani ya mji inakuwa rahisi kusambaza huduma za maji,umeme, kuwezesha ardhi kuwa dhamana ya kukopea benki.

Usichangae kwa makazi holela inakuwa ngumu kutengeneza anuani za mitaa"postal code"

Tatizo viongozi wanajua umuhimu wa kuwa na upimaji, lakini wameacha ujenzi wa makazi holela kwa sababu wananchi ni " wapiga kura",yaani kwa mitazamo hii tutachelewa sana.
Hata kuboresha huduma za afya, zahanati zikiwa mtaani au kwenye kitongoji zitasaidia wagonjwa wenye magonjwa sugu kwenda hospitali kubwa. Wanaweza kuhudumiwa katika zahanati kwa dawa za marudio.

Watoto kutokusafiri mbali kufuata elimu kama shule zitawekwa karibu na wananch. Wafanya biashara pia watasogeza huduma karibu na wananchi.

Ni rahisi kufahamu kila mtu anaishi wapi. Hata polisi itawasaidia kukamata wahalifu ki rahisi.
 
Hautaelewa kwa sababu haukutaka kufuatilia matangazo ya TCRA, TCRA ilitoa matangazo na barua kwa wamiliki wa majengo kushiriki mchakato wa kuboresha mitaa kwa kushauri majina ya mitaa yao, wapo walioshiriki lakini wengi hatukutaka kushiriki, sasa nani alaumiwe!
Zoezi hili linatakiwa kuwa endelevu
 
Sijui anamanisha nini ili kama post code nayo ifahanu zipo sana maeneo yote mpaka ngazi ya kata
 
Sasa hapo ni Buza. Yeye anataka "Kwa Mpalange"
Kwa Mpalange sio mtaa, ni kituo cha daladala kilicho ndani ya Mtaa wa buza, Kata ya Buza. Kwa hiyo hapo Kwa Mpalange anatumia msimbo wa posta huo wa 15125
 
Back
Top Bottom