Hivi kwanini Serikali na wabunge wa CCM mliamua kutukatili wafanyakazi suala la mafao?

Ni kupoteza muda kuwategemea wabunge wa ccm (ambao ndio wengi) usitarijie lolote la maana. Kumbuka ndio waliopitisha sheria kandamizi za mifuko kulipa kwa mkupuo 33% kabla Raisi hajaingilia kati!
Kuwategemea hawa wabunge wa ccm ni kupoteza muda na wakati.

Dawa hapa ni TUCTA kwenda mahakamani kudai haki za wafanayakzi ktk mafao, sema na TUCTA yenyewe hakuna viongozi bali siku hizi kuna wachumia tumbo!
Haya ndiyo mapumbavu kabisa, yaani hii nchi ukifikiria sana unaweza ukapiga watu risasi, mimi napambana nihamie Canada
 
Leo nimemsikia Mheshimiwa Rais akitoa maelekezo kuwa watumishi wa halmashauri wilaya ya mpya ya Kigamboni wapewe nyumba za NSSF na wakae bure mwaka mzima! Zile sio nyumba za Serikali na kwa kweli wafanyakazi wa nchi hii hawana mtetezi

Sent using Jamii Forums mobile app
Na NSSF nao walikuwa malofa, wankubalije kutoa nyumba ambazo sio serikali kutumiwa na watumishi wa serikali ilhali serikali ina hela za kuchezea kwanini isiwalipie watumishi kodi ya pango ?, hizo nyumba ni jasho letu sisi
 
Kuja kulalamikia humu Jf n buree tuu Mana Hawa jf walau Jambo ambalo n muhimu na linahitaji solution n Bora wangekuwa wanawatafuta hata wausika na kuwabana kiunagaubaga hapa.

Pili watu wanatukana tuu bila kuleta hoja saa zingine n Bora kumpa elimu yule amabae Hana ili ajifunze hvyo n Bora kuleta mawazo mazuri huenda wanaohusika wakapitia hapa kimyakimya.

Michango wangu kuhusu hili NSSF ibadili utaratibu wa mafao Mana haya mafao sio kila mtanzania anachangia bal n mtu anaefanya Kaz kwa mkataba ndio huchangia na wachache wa hiyari hvyo Kama likivyooanza na liiishe Kama litakavyomalizika kwamba pale ajira yako inapofikia ukomo Basi uchukue Chako.

Hii inawezekana kwa NSSF kupunguza matumizi yasikuwa ya lazima mfano NSSF inamajengo mengi Sana kila mkoa na baadhi ya wilaya Cha ajabu unakuta jengo la NSSF lipo Waz lakin ofisi za NSSF za mkoa husika wamepanga mfano NSSF Kilimanjaro.

Pili NSSF kulipia wanachama matibabu naona hili NSSF wangeachana nalo tuu na jukumu hili tayar NHIF wanalimudu na wao NSSF n wababaishaji kwenye kutoa matibabu kwa mwanachama Yan utazunguka mpaka pia n selective kwa baadhi ya hospital hapa Tanzania.

Tatu nyumba za kuishi walizojenga Mana zile nyumba zimekosa wapangaji Basi waseme Kama n mwanachama wa NSSF unaruhusiwa kupanga na kulipa 50% huku hyo 50% itakatwa kupitia michango ya mwanachama husika hvyohvyo hata kwenye kuuza pia.

Nne NSSF wanaweza kubadilisha hifadhi ya pesa ya mwanachama kuwa hisa za mwanachama hvyo kuumpa Uhuru wa kuamua kuziuza au kuendelea kuwa nazo pindi atakapokosa sifa za kuwa mwanacha hii itapunguza malalamiko mengi na matatizo na wanachama Kwan mtaji wa NSSF unakuwa palepale na kinachobadilika n mmiliki tuu wa kiasi flan za hisa.

N hayo tuu kwaleo NSSF nawakaribisha kuchukua mawazo yangu bure mkihitaji ushauri Zaid karibun
 
Back
Top Bottom