Hivi kwanini Mungu ana wivu?

Hivi kwanini Mungu ana wivu?

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,652
Reaction score
5,134
Wataalamu wa bibilia, nakumbuka kuna siku nilisoma hicho kitabu nikaona historia ya mnara wa babeli Mungu aliposhuka na kuwakuta binadamu wanatengeza ule mnara alishtuka na kuwatenganisha kwa lugha pamoja na maeneo ndiyo yakazaliwa mataifa mengine.

Tukio la pili kwenye sura ya mwanzo Mungu baada ya adamu kula ule mti ambao alikatazwa inaonekana ibilisi alikuwa anajua siri ya mti huo wa uzima japo hakuufahamu haswa ni upi ila baada ya Mungu kuona binadamu na jeshi lake watapanga kuutafuta ndiyo akauficha, nimesahau exactly ni wapi.

Case ya tatu, baada ya kuwatoa Wanaisraeli kupitia Mtume wake Musa aliwaambia kuwa yeye ni Mungu mkuu na anawivu hivyo wasiabudu mwengine isipoikuwa yeye.

Je, kwa kauli ya kusema kuna miungu mengine anafahamu kuwa kuna nguvu nyengine tofauti na yeye?

Je, hajiamini na nguvu zake?

Je, Mungu huyu ni tunayemuabudia wakristo na waislamu?

Je, ni binadamu wa mwanzo ambaye aliwahi kutambua siri za ulimwengu na akajitahidi kuzificha na hatimaye akajitolea taji la uungu?

Nawasilisha.
 
Ni sawa na wewe na mke wako then aanzishe uhusiano uliosawa na wa kwako kwa mwanaume mwingine.

Tafsiri utayoipata moyoni mwako ndio hiyo iliyomaanishwa kwenye hayo maandiko, halafu upime mwenyewe kama ni sawa au si sawa.
 
Mungu alimuumba mtu kwa sura na mfano wake.
kwani ukichukua sura yangu,yako na wengineo unaweza kujua au kufahamu ukubwa,rangi,nafasi,idadi ya SURA yake?

me najua kuwa kasema hivyo kwa sababu hafananii kwa mfano wetu wa sura wala tabia ila mungu labda tuawmw ni nguvu untouchable,invisible,unseen but you can feel it by your subconscious mind.
 
Mungu wa kwenye biblia na Quran hayupo, laiti kama angekuwepo asingekuwa na madhaifu makubwa kiasi hicho.

Huo mnara kabla haujajengwa, Mungu ajuae kesho yetu na ajuae kila kitu kuhusu sisi angeshatambua mawazo ya binadamu kutaka kujenga mnara na angesitisha hilo zoezi mapema.

Huyo shetani ambae alimdanganya adam na hawa kula tunda, angeshamuua zamani sana, Mungu muweza wa yote, mwenye upendo wote asingeruhusu tuishi na shetani wakati anajua shetani ana nguvu kuliko sisi.
 
Mungu wa kwenye biblia na Quran hayupo, laiti kama angekuwepo asingekuwa na madhaifu makubwa kiasi hicho.

Huo mnara kabla haujajengwa angeshatambu mawazo ya binadamu kutaka kujenga mnara na angesitisha hilo zoezi mapema.

Huyo shetani ambae alimdanganya adam na hawa kula tunda, angeshamuua zamani sana, Mungu muweza wa yote, mwenye upendo wote asingeruhusu tuishi na shetani wakati anajua shetani ana nguvu kuliko sisi.
nashangaa sana bibilia inavyomuelezea mungu as if binadamu utakuta andiko linasema upon wapi wewe adamu,na adamu akaitika niko hapa mungu wangu.

mda mwengine wanasema mungu alikuwa anatembelea bustani...this is human behaviours
 
FB_IMG_1712176443286.jpg
 
Back
Top Bottom