Hivi kwanini mtu akishaoa au kuolewa ndo yanaanza kuja mazari ya kukutana na wapenzi wengine wazuri zaidi?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Kusema ukweli; Mitihani mingine hii ni majaribu! (LAKINI SIYO KWA WOTE BUT MOSTLY HUTOKEA)

Mtu anaweza komaa miaka kadhaa kutafta mpenzi wa maana kwa taabu sana lakini punde tu akishaoa au kuolewa ndo mazari yanaanza!

Mfano; Kwa upande wetu wanaume; Kuna wakati unakutana na mwanamke hadi unajiuliza hivi huyu alikuwa wapi siku zote hizo? Mwanamke halazimishi kuolewa, mwanamke mwenye akili zake katika kushauri, Muelewa, Mrembo kila idara n.k Kiufupi matendo yake yanakufanya uone sifa zake adimu bila shuruti; Unajaribu kumchimba uone kama maisha ana pretend lakini unagundua ni real kabisa! But Tayali unakuwa ushaoa!

Hivi ni kwanini Mazari kama hayo huwa hayatokei mwanzo kabisa hadi yasubili mtu afunge ndoa?

Au ukishafunga ndoa ndipo huwa inakuja nyota ya ndoa?
 
Ni kweli mkuu hili lipo na tulichukulie km mtihani yapaswa tuushinde tu.


Sent from my iPhone using JamiiForums
Hapo ndipo huwa naamini kumbe wanawake Wa kariba ya mama zetu kumbe bado wapo!

Ukiachilia mbali wale wanaolazimisha kuolewa, ambao kila mda wanaulizia mwanaume kujitambulisha achumbiwe
 
Km ww ni muislamu hiyo Ina maana unaletewa wanawake na Allah ili ukamilishe zile nne bila Ila km ni Mkristo hayo ni majaribu/vishawishi unavyotakiwa kuvishinda kwa nguvu zote ili Yesu/Mungu adhihirike ndani yako....

NADHANI NIMESOMEKA
 
Huyo anaitwa shetani. Remeber baada ya kula tunda pale bustanini adam ndipo aligundua yuko uchi. Siku zote hizo hakujua.
Ni kuwa makini.. and remember mke wako ni mke wako.. unaweza mtenheneza akawa mzuri zaid au mbaya zaid. It all up to you

Sent using Jamii Forums mobile app
Brother una umri gani kwenye ndoa?
Isije ukawa unashauri hivi kumbe bado uko Honeymoon
 
Huyo ni shetani kaja kukutoa katika ndoa. Shetani hapendi agano la ndoa sababu ndoa ni kanisa, ambapo utukufu wa MUNGU huimarika ndani yake.


Sasa usiite zali hilo bali ni majaribu. Kama hawakukuona kabla ya ndoa wasikuone baada ya ndoa. Mpende ulie nae sababu alikukubali katika wakati kilaa mtu alikuona mikosi na nuksi.

Mwanaume aliye ndani ya ndoa huwa anakuwa na mvuto sana. Wanawake hawa wa mjini wasiojielewa na watangaji wa mitaa huwa wanavutiwa na wanaume walio ndani ya ndoa sababu huona commitment yao katika mahusiano ile hali wao hawana commitment. Mwanamke anae mpata mwanaume mwenye nia ya ndoa ndie mwanamke mwenye bahati katika jamii, sababu ndoa humkinga na uasi wa dunia na kumpatia ulinzi.


So ushauri wangu kwako, ukiona kuna kadada kanajileta kwako then jua ni muda wa kuongeza mahaba kwa mke wako na kumfanyia mazuri zaidi. Kupenda mwanamke wako aliyekuibaliana na wewe katika shida na raha kuna raha yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shetani huyo. Anakujaribu maana hapendi familia. Familia ndio msingi mzuri wa kila kitu, akivuruga hapo basi kazi yake inakuwa rahisiiiiii.

Hata huyo ulomuoa ulimuona ni mzuri,mwenye akili na sifa zote uzitakazo. Ukaamua muoane muanzishe familia yenu.
 
haya majarbu ndo huleta mtifuano ktk ndoa, yaani anavokusumbua mwenza then unahsi ulikosea njia na yule wa njian ndo mtu sahh, wakat huu ndoa nyingi hua mashakani
 
Hiyo ni kawaida mkuu. Hata simu ukinunua simu kali leo linakuja toleo jipya kali zaidi inabidi ufanye update, nikama mambo ya software ukiwa na old version ambayo ilikuwa nzuri wakati huo developers wanakuletea version iliyoboreshwa zaidi kwahyo uamuzi ni wako kustick na na oldest version au kufanya updates to the latest version
 
haya majarbu ndo huleta mtifuano ktk ndoa, yaani anavokusumbua mwenza then unahsi ulikosea njia na yule wa njian ndo mtu sahh, wakat huu ndoa nyingi hua mashakani
Halafu ukitoka huko ndo unapewa tulizo LA nafsi
 
Back
Top Bottom