Hivi kwanini mpenzi wangu hanipendi?

Hivi kwanini mpenzi wangu hanipendi?

Wandugu nimekuja hapa mnipe ushauri kidogo

Nilikuwaga na demu wangu she is so cute kwa kweli ila tatizo lake alikuwa ananipiga mizinga sana

Huyu demu nilikutana nae kipindi fulani alikuwa boy wake sema huyo boy wake alikuwa bahili sana yani hata vocha alikuwa hamtumii ,demu alimpenda mshikaji sema mshikaji alikuwa hana time nae kabisa

Baadaye demu akaamua aachie ngazi, mwanzoni tulikuwa washkaji sana na huyo demu sema baada ya kuachana na mtu wake akaamua anitamkie ananipenda mimi na angependa niwe mpenzi wake ,mm nikaona poa tu pia sikushangaa kunitongoza kwa kuwa mimi nina mwili uliojengeka kimazoezi pia nina sura yenye kuzuzua mademu so suala la kunitongoza sikuona la ajabu sana


Sema tatizo lilikuja kuanza pale nillipogundua huyu demu ni mtu wa mizinga sana pia ni muongo muongo sana na mbaya zaidi uongo wake anawashirikisha rafiki zake ili iwe rahisi kunidanganya


Huyu demu ilikuwa nikitoka nae nijipange haswa ,chini ya laki 3 lazima niaibike kabisa kwa kuwa kila kizuri atachokiona lazima atake nimnunulie nisipo fanya hivyo anakasirika na haongei na mimi wiki nzima akipiga simu lazima atake pesa



Pia alikuwa na tabia ya kuwalingishia wenzake kuhusu mimi ,ilikuwa nikimnunulia kitu cha gharama lazima akawatambie wenzake


Sitasahau siku moja nimetoka nae kwenda MCity kwa gari la kwao mfukoni nilikuwa na laki 5 ,unaambiwa siku hiyo laki 5 yote iliishia hapo hapo mcity mbaya zaidi sikuwa na nauli ya kurudia home na akakataa kabisa kunipeleka home nilijuta sana kwa nini sikwenda na gari kwa kweli,sema kwa bahati nzuri bro wangu alikuwa kaenda tegeta nikampigia simu akirudi anipitie turudi wote nyumbani kwa kuwa sina nauli ,aisee alinicheka sana kwa kuwa kipindi natoka aliniona nazo pesa zote



Yote tisa kumi suala la yeye kuninyima penzi aisee linaniuma sana alikuwa ananionjesha mara chache chache sana tena sio bure bure mpaka nimpe hela


Baadaye nikawaza nikaona nimpigie simu nimwambie tuachane ila tubaki kuwa marafiki tu kama zamani cha ajabu alichonijibu kilinishangaza sana alinijibu ndio amekubali tuachane na akasema nifute namba yake kabisa na hataki kabisa hata urafiki na mimi

Mwanzoni nilijua anatania maana lugha aliyokuwa anatumia ilikuwa laini sana baadaye siku zilivyozidi kukatika ndo nikaamini alichokuwa anamaanisha


Yaani mpaka sasa sielewi kwa nini huyu msichana alikuwa hanipendi maana kwetu ni matajiri kama kwao na vitu vingi nilikuwa namnunulia kwa kifupi alinifanya kama baba yake ingawa mimi ni mwanafunzi wa chuo tena mwaka wa kwanza kama yeye


Sielewi kwa kweli yani ,naombeni ushauri wenu pia nataka madada wa humu waseme vitu gani wanampendea mwanaume maana sielewi kwa kweli yani
Msomi ambae ajaelimik pole naendlea kuwa kweny giza ilooo ...it so gentlemen nasio boy ...jitambue
 
Haipendwi ATM zinapendwa HELA zilizomo. Kilichokuponza ni wewe kujifanya ATM.
 
pole sana jamaa....mademu wanaotongoza wakimbie km ukoma joh...dem mwenye upendo lazima ww ndo utongoze na usote sana ukija kumpata ndo mtapendana kweli lakini ukiona umetongozwa ww ujue umekutana na mkosi mzee...fid q anakwambia money makes money bt love is hustling....kumbuka easy comes easy go....vitu vinavyokuja bila kuhaso vina walakini uvikataage joh...ila usijilaumu sana coz umejifunza kitu maana wahenga wanasema..funzo la mjinga ni tabu.
 
Mapenzi hayalazimishwi,embe likishaiva lzm lianguke,na tunda likianguka arirudi mtini,Hakupendi kaona ATM haisomi network not rechargeable
 
Mtafute mtoto wa maskini mana wakishua mwenzako hakuelewi.... Endelea kutumbua tu majasho ya wazee wako walichuma kwa shida walijinyima ndio mana ukajiita wakitajiri
 
ushafika mwaka wa tatu kweli au ndo ulishadicso?
 
Huyo ndo wale wale mumy am cuming dad am going,
Halaf toto la kiume mzma eti unajisifia kwenu kuna pesa inaonekana hata kujitegemea wew bdo sana manake hauna hata uchungu na nidhamu ya pesa
 
Kwa akili yako tu hata mimi ningekuchuna na kukupiga chini..kwenu matajiri ndio nini sasa..nikwambie kitu..sisi wanawake tunapenda mwanaume mtafutaji,anayejiamini, na mwenye future..hayo yako ya bby yes bby no peleka green hekas huko ndio utakutana na wenzako ila nao wakivuka tu umri fulani lazima utombewe.
 
Yan hapa tena umeongea pumba mkuu, nan kakwmbia mtu anakupendea utajiri....

"""Yaani mpaka sasa sielewi kwa nini huyu msichana alikuwa hanipendi maana kwetu ni matajiri"""
Imagine..*** dis shit..utajiri utadhani anaujua..Yani kanichefua
 


Inabidi nicheke kwanza
Maana thread yako
Imenifurahisha mno.

Pole kwa yaliyo kukuta
Huyo jamaa wa kwanza wa huyo demu
Alikuwa sahihi ila sio sana.

Pesa mpe mwanamke ila isizidi kiwango

Na nimechukizwa na wewe kushindwa
Kuonesha msimamo dhabiti kwa
Huyo demu, atakuendeshaje
Huyo mwanamke,

You have to be a gangsta
You have to act like a gangsta...

Watoto wakishua mnalia lia kila siku
Kuhusu kuumizwa na mademu...

Huyo demu kwa kuwa alikuwa rafiki
Yako ndio maana amejua udhaifu wako

Ndio maana anakufanyia vituko

Your a man
Be strong like a man
Act like real men....
Be a gangsta.....
Come here
 
sasa kama ungekuwa wewe unge weza kumnyima?
Nenda katafute chumba uswahilini hlf anza kuishi km wao na usijioneshe una hela kwa sbb kwanza huna hela..
Pili zingatia masomo yako sana..utaenjoy life..
Acha kutegemea vitu vya babako utakufa masikini.
 
Back
Top Bottom