Hivi kwanini matajiri wakubwa hapa Tanzania ni wahindi na waarabu tu?

Trump anayo jawabu....tuwache ngono..
Uzinzi wa hovyo kws kuona ukiwa na mademu ndo utajiri.
Pia tuwache ulevi...ulevi ni umasikini
Kitu kingine tujifunzee savings..
Ukiwa na malengo basi utafika tu.
Wapo vijana wa kichaga wamepiga sana...wana malengo....
 
Wahindi walevi wachache sana na wapenda bata wachache bongo hii mtu anakamshahara ka Laki Nane anajiona biingwa na altezza yake akija gereji anakuoneni nyie mlo na maoili mapimbi tu...mademu kwa sana tunapenda sana ngono hachanani (ushahidi umo humu kwenye sledi zetu nyingi). ..hatupendi kuweka akiba ukiuliza jibu ni "niweke akiba kwa pesa ipi"....tunakimbilia vitu visivyozalisha pesa kv kujenga vijumba ilhali huna kipato kinachoeleweka (uoga wa maisha).

hatuna nidhamu ya matumizi (eti fasheni mtu mwenyewe kula yako ya tabu unapotezea hela huko)...hatuwekezi...wanaofanya biashara akipata faida anaitumia yote.

elimu elimu elimu. ..

customer care ya hovyo kabisa kwa wengi wetu nenda kwa kanjibai ukaribisho tu unakufanya usalie kwake, sie huku ndo yale ya (lile pangaboi! kwani we umejipangaje! ) au 'kwani lazima ununue kwangu ' ,,,,unakoroga sumu kisha unajinywesha ushasikia chai hiyo :mad:

tunapenda sana udaku aka umbeambea wa kufuatilia individual issues na kuacha kazi.

tuko too selective, hatutaki kazi za suluba eg kilimo,mining,logging ambazo kwa hapa Tanzania ndo zina pesa.
Acha hao kina kanjibai waendelee,,,waiterrr kuja leta tano hapa wape hao kreti dadeki zangu mi sio muhindi :confused:
 
wahindi waliozaliwa mtwara na waarabu wa rukwa.......
⛽ mtoa post kaongea menge kw yale anayoyafaham ila ukwe wa kumiliki mali ni mgumu sn, japo siri ya mafanikio nikujituma, nikweli tunajituma sana, pia maandiko yamesaidia ktk ufafanuz kwamba TAJIRI KUINGIA PEPONI NI SAWA NA NGAMIA KUPENYA KTK TUNDU LA SINDANO,, pia unapo taka kucbakata hoja na kupata majibu ya mingi soma andiko hilo,, mimi naamini hakuna rundo la Mali linalokosa ushirikina ndani yake, wa hindi na waabu hawa viumbe wana miliki majin, chumaulete, ,makafara, kiujumla hayo ni mambo magumu sana kwetu cc, japo wapo wachache wenye mioyo hio ya ujasiri
 
hii ishu watu wanasema ni uchawi lakini so kweli watoto wakihind wanafungiwa ndani mda mwingi hiyo inapelekea kushindwa kucheza na wenzao so wanakuwa hawachangamki kama mataila hivi
Mkuu sijui una umri gani ,ila kama una miaka 25 kurudi chini, usibishe nyamaza, kwakua bado unakua utayakuta huko mbeleni
 
Sisi tumekimbilia kujenga nyumba mbali wao wanaishi mjini nyumba za kupanga
Sisi tunaendekeza starehe wao wanawekeza
Sisi tuna lugha mbaya kwa wateja wao wanamjali mteja
Sisi tunaibiana wao ni ngumu sana kuibiana
Sisi tunadharauriana yaani kama Bosi ni Mwafrika unamuona ndio sivyo ila wao wanaheshimu Bosi wao
Sisi tunapoteza muda mwingi kupiga picha insta na fb wao wanatumia muda mwingi madukani wakiuza bidhaa
Sisi hatupendani hata ndugu kwa ndugu wao wanapendana na ndio maana picnic zao unakuta wanaenda wengi sana
 
Trump anayo jawabu....tuwache ngono..
Uzinzi wa hovyo kws kuona ukiwa na mademu ndo utajiri.
Pia tuwache ulevi...ulevi ni umasikini
Kitu kingine tujifunzee savings..
Ukiwa na malengo basi utafika tu.
Wapo vijana wa kichaga wamepiga sana...wana malengo....
Upo sahihi mkuu, wengi hatuna nidhamu ya matumizi na tumekosa maono na shida inakuja pale unapopata mke asiye na future inakuwa ni shida juu ya shida na ndugu nao kila kukicha wao ni mizinga wakiwa na imani kuwa mtaji wako au mshahara wako unaweza ukawahudumia wotewote. Pongezi kwa Wachaga&Wakinga walau wanajitaidi ktk ilo.
 
Sio kweli wako watanzania weusi wengi ni matajiri sana,ila utajiri wetu uko kwenye mifugo mashamba makubwa, nyumba na viwanja.Na wengi wanaishi maisha ya kawaida,na wengine wanafukia pesa haweki Benki.Akifa PESA ndio imepoteam
Sio utajir huo sasa
 
Imekuwa hivyo ni kwa sababu wanatumiwa na viongozi waliopo serikalini. Wao (viongozi) wanaiba na kuwekeza kwenye kampuni zao na kuwatumia waarab/wahindi kuendesha shughuli zao.
 
Wahindi wajanja. Mfano hapa kazini kwangu. Manunuzi kwa muhindi.. Gereji pia. Bima pia. It support pia. Mswahili kapata tenda ya usafi na dereva tu. Vingine wamewapa wahindi wenzao
 
Mhindi anaishi Kariakoo
Sisi Tunajenga Mbweni au Bunju na gari la thamani sawa na nyumba ya kariakoo (apartmetn) wao wananunua na kupunguza zile fujo za kusafiri kila siku kutoka mbali
mh hawa majamaa kitu kinachoitwa shida hawakitaki kabisa na elimu mwisho form 4 dukani dah..
 
Sio utajir huo sasa
Huo pia ni utajiri,ukiuza mifugo unapata pesa,ukivuna mazao unapata pesa,ukiwa na nyumba za wageni(guest house)unapata pesa,ila sisi pesa zetu hatuweki benki,tunafukia.Na pia hatutengenezi ajira endelevu.Kwa hiyo kuonekana tuna pesa inakuwa ngumu sana.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
nadhani hilo swali ulitakiwa kumuliza baba na babu yako ,hawakuweka juudi katika kuwekeza ili ww uje uendereza mali walizo tafuta wazazi wako na hilo swali iko siku mwanao atakuja uliza tena kama usipo jishughulisha kwa bidii zaidi
 
Biashara za waafrika walio wengi hazisomeki. Pesa wanazungusha kwenye biashara in cash zikizidi wanachimbia chini, records hawaweki, biashara hawaweki kwenye mitandao, wapo simple hawataki kujionyesha, wanaishi kama middle class lakini wako worth billions. Akishtukizia anaenda dukani ananunua VX ya 300m cash. Wapo wengi sana Tanzania. Forbes hawawezi kuwafaamu. Subiria watoto wao wakiridhi hizo Mali uone mlipuko wa mabilionea waafrika kwenye Forbes sababu hawa wengi watatamba sana nakujionyesha alafu watafilisika
 
Soma historia vzr utapata jibu mdau. Slave trade in east and central Africa......"Tipu Tipu" wengi wao wamerithi mali toka kwa wazee wao ambao kwa njia moja au nyingine walishiriki ktk biashara ya utumwa hii ni kwa upande wa Waarabu. Wahindi wao walikuwa mawakala wa Waarabu ktk biashara zao mbali mbali utumwa ukiwa miongoni. Hii ndy sababu kubwa ya Waarabu kuwa matajiri husani ktk nchi nyingi za Africa ambazo ziliathirika na utumwa.
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Back
Top Bottom