Kwanini Waarabu na Wahindi Tanzania ni matajiri?

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
Hivi ni kwa nini Waarabu na Wahindi hapa kwetu ni matajiri sana ingawaje Shule hawajaenda?
Ukizunguka TZ Mikoa kama Shy, KG, mpka Iringa na MT na LN kote huko unakutana na Waarabu matajiri wa kufa mtu wkt hata Shule hawajaenda? Kuna Waarabu hukoo Bukoba au Shy hata kusoma ni ishu lkn anamiliki malori hata 40 sasa huu utajiri ulikujaje kujaje? Sasa ni kwa nini?

Mbona sisi siyo Matajiri? Na kama ukiuliza unaambiwa ni utajiri wa kurithi lkn walirithi ktk kwa nani huwo utajiri?

Mtu kama mwenye mabasi ya Abood huyu Mwarabu/Muhindi wa Moro utajiri aliupataje? Ukienda stendi ya Ubungo kila baada ya saa moja basi linaondoka kwenda Moro na ktk Moro ni hivyo kila siku, hiyo fedha aliipata wapi?

Ukimuuliza Manji atakwambia alirithi ktk kwa baba yake na baba yake alirithi ktk kwa babu yake, sasa babu yake Manji utajiri aliupatia wapi?

Mbona sisi hatuna mahali pa kurithi?
Na hiyo biashara akina babu yake Manji, Rostam &Co. walikuwa wanafanya ni ipi na na nani?


Nauliza haya maswali kwa maana leo hii ukimchukuwa Mtz wa kawaida ambaye hajasoma kama walivyo Waarabu ninaweza kusema kwamba ni karibu na haiwezekani yeye aje kumiliki mabasi mengi kama Abood au Shabiby yaani sioni ni jinsi gani hilo linawezekana sasa kwa nini kwa hawa Waarabu/Wahindi wanaweza na wakati hawajasoma?

Je kuna kitu labda Mlm.Nyerere alikiona ambacho sisi wengi wetu labda hatukifahamu khs utajiri wa Waarabu na Wahindi mpaka akaamua kuwataifisha hasa nyumba zao?
 
Mkuu kwanza kusoma na utajiri havina uhusiano wowote

Pili unawazungumzia wahindi kachori,wahindi pasi au wahindi pilipili?


Lkn swali langu fedha wanapata wapi ya kununua malori 40 au kumilikia mabasi 50 na zaidi kama Shabiby au Mohamedi trans?
 
jeikei kwenye hotuba yake moja alisema ''''''''''kwenye utawala wake anapenda tanzania iwe na mabilione wengi'''''''''......lakini hao mabiliaone wengi ni wale ndugu zetu wa kieshia sie weusi sidhani tumo....
 
Wana akili ya biashara na wazuri kwenye Ku budget hela yao hawana matumizi ya hovyo..hela haitumiki kirahic hadi iwe inatumika kwa sababu yenye umuhimu au ya msingi na wamejikita kwenye biashara zaidi na wepec wa kuhifadhi Wa hela bank. Akiwa ana vision au goal ya kufikia hapumziki hadi aipate huku kufanya vyote kwa umakini Wa hali ya juu
 
Kwasababu wabongo NI AKILI NDOGOOOOOOOOOOOOOOO Usiku kucha wako mitandaoni WANATUKANANA Weeeeeee

Sasa wewe uko wapi hapa?. Jibu hoja kwa pointi na sio mihemuko ya kushindwa na Lema ama mambo ya siasa.
 
Lkn swali langu fedha wanapata wapi ya kununua malori 40 au kumilikia mabasi 50 na zaidi kama Shabiby au Mohamedi trans?
Nenda bandarini mkuu hapo ndipo utajifunza utajiri wao au ukaunganishe na wewe bomba la mafuta lisilo na mita.
 
Warabu wengi matajiri unaona leo ni mali za urithi. Miaka ya zamani Wakati huo sisi bado tuna mawazo ya ujamaa ya nyerere kila kitu tuli zoea kupewa na serekali wenzetu walikua wanatumia fursa kufungua maduka kununua magari nk. Ndomana warabu almost wote leo utajiri wao upo kwenye magari au vituo vya mafuta coz wamerithishwa na huwez kuta mwarabu anamilikoli mall kubwa au supermarket coz vitu hivi zamani havikuepo...wahindi ni watu wa dili na ujanja ujanja kama kina manji ni asili yao kutafuta pesa wanajua
 
Sasa wewe umeshasema kabisa wanarithi kutoka kwa mababu zao halafu unatuuliza tena.. Hujaona wachaga wanaoanza na kuuza chips/ Karanga na sasa ni matajiri wakufa mtu hata hao wahindi/waarabu hawakamati? Hao ndio tungejiuliza wanafikaje hapo kwa sababu hawajarithi..they made it on their own
 
Majibu yako yote,yako kwenye kitabu kinaitwa,MASTER OF THE GAME .......by Sidney Sheldon,

ndo utapata jibu kwanini baadhi ya family zinaweza miliki utajiri hata kwa miaka 200
 
WANAKWEPA KODI na KUHUJUMU UCHUMI wa NCHI. Hamna kumung'unya maneno. Ngoja hii miaka mitano ya kwanza ya awamu hii iishe uone kutakuwa na magari mangapi ya kifahari bado barabarani. Kuna Mpuuzi mmoja alikamatwa juzi juzi tu ana Merc Benz 2015 s550 eti Ina namba T 234 A...watu wakasema nae ikagundulika ushuru Stahiki ulitiwa kapuni. Gari ipo yard mpaka hivi sasa tunavyoongea.
 
Back
Top Bottom