TihZ
Senior Member
- Jul 31, 2012
- 158
- 26
Nina mpenzi wangu tuna mwaka sasa katika penzi letu ingawa mwenzangu anaonekana kutonijali kama mimi ninavyomjali yeye ila miezi miwili iliyopita kuna msichana mmoja alitokea kunizoea sana kushinda hata huyu mpenzi wangu,alikuwa akinijulia hali kila inapowezakana kuzidi hata huyu mpenzi wangu Baada ya wiki kadhaa kupita binti huyu aliniambia kuwa angependa tuwe wapenzi kusema kweli hata mimi nilitamani iwe hivyo lakini sikuwa tayari kumuumiza kwani sikuwa na hisia kama zake hivyo basi niliamua kumkalia kimya maana sikupenda kumuumiza kwani alikuwa ananijali sana.Ila leo alinitafuta hewani hivyo sikuwa na jinsi ilibidi tu nimwambie hali halisi ingawa aliumia sana.Ninachojiuliza hapa hivi ni kwa nini mara kadhaa unampenda mtu lakini haonyeshi kukujali je ni kwamba inawezekana kuna mtu wa pembeni au ni hulka ya mtu tu kuwa hivyo?