malisoka
JF-Expert Member
- Jul 8, 2012
- 1,860
- 2,638
Nilishangaa sana nilipomuona Mwenyekiti wa Kamati ya PAC alipokuwa akitoa mashutuma kwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Hon Kangi Lugola, hivi huu ni udhaifu na unafiki aliokuwa akisema CAG Assad hapo kabla.
Ninajiuliza:
- Kwa nini wametoa shutuma hizo baada ya yeye kutumbuliwa?
- Hivi ni kwanini PAC ilishindwa kabisa kumhoji Kangi wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani?
- Hivi serikali ina nguvu kuliko Bunge? Kwa maana ya kuface mtu anapokuwa nje ya serikali kwa mbwembwe na bashasha.
- Hivi ni lini wabunge wa CCM wataacha unafiki huu wa kuwaogopa mawaziri wa serikali?
Kwa kweli hili limenipa mashaka sana kama Bunge linaweza kuiwajibisha serikali au serikali imeweza kuliwajibisha Bunge.
Ninachelea kusema Bunge letu linaiogopa serikali na ni dhaifu mno kwa serikali.
NB: Wajibu mkuu wa Bunge ni kuiwajibisha serikali, kama hilo halifanyiki basi kuna walakini na bunge letu.