Hivi kwanini Bunge: "Wabunge wetu dhaifu na wanafiki hivi"

malisoka

JF-Expert Member
Jul 8, 2012
1,860
2,000
Nilishangaa sana nilipomuona Mwenyekiti wa Kamati ya PAC alipokuwa akitoa mashutuma kwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Hon Kangi Lugola, hivi huu ni udhaifu na unafiki aliokuwa akisema CAG Assad hapo kabla.

Ninajiuliza:

- Kwa nini wametoa shutuma hizo baada ya yeye kutumbuliwa?

- Hivi ni kwanini PAC ilishindwa kabisa kumhoji Kangi wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani?

- Hivi serikali ina nguvu kuliko Bunge? Kwa maana ya kuface mtu anapokuwa nje ya serikali kwa mbwembwe na bashasha.

- Hivi ni lini wabunge wa CCM wataacha unafiki huu wa kuwaogopa mawaziri wa serikali?

Kwa kweli hili limenipa mashaka sana kama Bunge linaweza kuiwajibisha serikali au serikali imeweza kuliwajibisha Bunge.
Ninachelea kusema Bunge letu linaiogopa serikali na ni dhaifu mno kwa serikali.

NB: Wajibu mkuu wa Bunge ni kuiwajibisha serikali, kama hilo halifanyiki basi kuna walakini na bunge letu.
 
malisoka

JF-Expert Member
Jul 8, 2012
1,860
2,000
Afadhali uchelee, kusema Bunge ni dhaifa ni kulitukana Bunge!.
Bunge liheshimiwe!.

Ila inauma sana . Tunawachagua watu kwa ajili ya kusimamia haki na maendeleo ya watanzanaia bungeni katika uwakilishi wa majimbo. Halafu wao ndio wanakuwa kikwazo na unafiki unafiki!

Hivi umeishafika dodoma hivi karibuni?

Serikali imehamia dodoma, panapokuwa na bunge hakuna tofauti, bunge ni kama serikali na serikali ni kama bunge.

Tena kuchanganya kwamba hakuna matangazo ya Bunge live ni wabunge wamekuwa ni kama wapo kwenye mkutanoi wa chama cha walimu vile.

Thamani yao mbele ya wananchi imeshuka sana. wamekuwa wakawaida sana kutokana na kutokuwajibika kukemea na kuishauri serikali.

Ukimuona Mch Msigwa watu watakodoa na kusema umemuona mbunge msigwa!
Ukimuona Zitto kila mtu atapenda amshike mkono.
Ukimuona Mbowe utatamani upigenaye selfii.

Sasa ukutane na Mh Livingston Lusinde -Kibajaji mipasho kwanza huwezi kumtambua hana mchango kwa wananchi zaidi ya kupinga kupinga kila kitu.
 
LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
6,514
2,000
Sijui kama hata wana angalia mabunge mengine yanavyo endeshwa.. Yaani ukiangalia mabunge ya wenzetu halafu ukija kuangalia bunge letu hasa akiwa ana changia mbunge wa Ccm utadhani ni kikao cha mazishi una angalia.. Ina tia aibu sana kuona kila jambo kwao ni ndiooooo... Hata kama halina tija.
 
Kabulala

JF-Expert Member
Oct 13, 2019
540
1,000
malisoka,
Correction: Chairman wa PAC ni mbunge kupitia CHADEMA na sidhani kama kuna mhimili upo Kwa ajili ya kuwajibisha mwingine, kilichopo ni kwamba Bunge Kwa kupitia Kamati linatuwekea macho na masikio Sisi wenye nchi yetu na serikali.. Chairman alitakiwa aseme yote waliyoyaona na kuyasikia ambayo ana amini sio Sawa na atoe maazimio Bungeni... wabunge wakae kama Kamati na watoe maazimio Kwa serikali Kwa kupitia Waziri Mkuu Kwa utekelezaji...na the way navyowajua wabunge wetu maazimio yangekua Waziri ajiuzuru.. guess what..Magu aliwawahi na PAC walikua wameshaandaa Hotuba Yao na kujipanga kuwasha Moto Bungeni...SIASA NI HESABU...Huu ni mwaka wa Uchaguzi..hakuna upande uko tayari kuupa mwingine political milage.
 
Ndio kisheria ni hivyo lazima mbunge dhaifu dhaifu awekwe hapo kama bendera.
 
Halaiser

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
2,537
2,000
Serikali ya ccm pamoja na Wabunge wake ni mali ya mtu mmoja. Yaani one man show. Ikitokea kesho Kangi akarejeshwa hao hao utaona wamebadili mwelekeo na kuanza kumsifia yy na mamlaka za teuzi. Mf hai ni kwa Bw Kicheere.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom