Hivi kwanini BOT Tanzania uwa inakwamisha mambo mengi?

kwa-muda

JF-Expert Member
Sep 5, 2018
1,163
2,223
Kuna huduma nyingi sana za kifedha uwa zinakosa vibari kufanya kazi hapa nchini na hii inakwamisha watu wanaofanya kazi na biashara mtandaoni na ukiuliza wahusika watakwambia ni kwasababu ya sheria za kifedha Tanzania. Wenzetu kenya mambo safi na karibia nyingi Africa sijui kwanini sisi hatuendi na kasi ya mabadiriko/
Mifano
Paypal mpaka leo Tanzania huwezi pokea ela sijui wanabana kwasababu gani sijui kwanini BOT wanabana.
Skrill waliapply ili iwezekani mtu kutuma ela kutoka account yake ya skrill kuja mpesa na tigo pesa wameomba waruhusiwe toka mwaka 2015 mpaka leo hakuna wakati kenya unaweza tuma ela toa skrill ikaingia mpesa. Na sababu wanazotoa hao skrill ni kwamba BOT hawajapitisha ombi lao.
Haya mambo yanakwamisha sana hasa watu wanaolipwa kutoka nje bank wire ni expensive na inachukua muda wakati mobile wallet ni cheap na zinasave muda.
BOT kama mko humu jaribuni kuangalia hili jambo maana kama mnataka kwenda na kasi ya mabadiriko angalieni upande wa pili wa shilingi watu wengi wanashindwa kupata vipato vyao on time.
 
Sheria nyingi karibu kila sekta ni za kuwafanya watu walioko nje ya siasa ya Chama Tawala wawe ma hofu ,maskini,wanyonge na wasiojitambua. Sheria zenye ladha ya kikoloni. Mpaka sasa ndani ya nchi moja ya kiafrika Kuna mabwana na watwana. Kuna watu hata akiongea huruhusiwi kumjibu. Ukimjibu au kujitetea unatishwa na kuambiwa utashughulikiwa mana unacheza na mtu hatari sana.
IMG-20180923-WA0010.jpg
 
Nishafikiria kuandika uzi kama huu good thing umeniwahi lakini watanzania sisi tuna ujinga.

Paypal wanasema ukiona huwezi kupokea pesa ni kwa ajili ya sheria za benki kuu yenu siyo wao. Sasa kwa ujinga wetu wa kutojua huko online maisha yanaendaje tumejikaliza kimya tu.
Wale wachache ambao wamejua kuwaambia wenzao ili wajue wanahisi watafaidi sana.

Dunia iko kasi Tz yetu inatakiwa iende kasi pia, huwezi amini hata kusign up for payoneer bila kua na akaunti ya benki kwa Tz ni haiwezekani, halafu Pakistan eti wanaweza.

Ujinga wetu unatuangamiza.
 
Tanzania ili uishi kwa amani inakubidi kuwa ZWAZWA FULANI, ZOBE ZOBE na KULA KULALA YES MAN - DREAMLESS !

Ukijishughulisha tu kidogo UTAKWAMA.

Ukifuatilia wenzio nchi nyingine wanaishije UTAPATA STRESS BURE !

Ukitaka hata kufanya kiujasiriamali UTAKWAMISHWA NA SHERIA KOKO kama SIYO KWENDA JELA.

Tanzania ndio Taifa lenye MADOCTOR + MAPROF MAZWAZWA EVER
 
Kwanza watanzania wenyewe hawako ready kwa mambo ya business, hata kama B.O.T wanakwamisha lakin watanzania wengi hawajui business , hata hiyo PayPal uliyosema ni asilimia moja tu ya watanzania wanaijua,

Bado Tanzania tunahitaji mwalimu mzuri wa ubepari baada ya kumpata mwalimu mzuri wa ujamaa(Nyerere)
Hatuko katika dunia ya sasa, mambo mengi yanafanyika kizamani
 
Kwa sasa hivi vijana wengi tungekua tuna uwezo wa kujiajiri online. Kulaumu ujamaa na hizo online platiform kutambulika na 1% ya watu siyo kigezo cha kutozifanya hizo huduma kuwepo nchini.

Unataka kusema Kenya nzima inaijua Paypal?
 
Ila asilimia kubwa wanajua
So kama watanzania
 
Binafsi siamini kama wananchi kujua au kutojua ni sababu isipokua viongozi wenyewe wanatakiwa kujua dunia inaendaje na waendane nayo.
Force ya wananchi kujua ndo inasukuma watu kushinikiza huduma hizo kuwa allowed na B.O.T ,mfano we umeijua ndo maana ukaanzisha uzi huu usingejua usingekuwa interested na kuwasema B.O.t wajiangalie upya
 
ujamaa umetudumaza, nchi imejaa watu waoga waoga na wenye hofu na mambo mapya. na ndio maana hata wanausalama wa nchi hii wanakikumbatia sana kile chama cha kijani na cha zamani, wana hofu na mabadiliko!!
 
Ujamaa upi unaozungumzia?
 
Kuna huduma nyingi sana za kifedha uwa zinakosa vibari kufanya kazi hapa nchini na hii inakwamisha watu wanaofanya kazi na biashara mtandaoni na ukiuliza wahusika watakwambia ni kwasababu ya sheria za kifedha Tanzania. Wenzetu kenya mambo safi na karibia nyingi Africa sijui kwanini sisi hatuendi na kasi ya mabadiriko/
Mifano
Paypal mpaka leo Tanzania huwezi pokea ela sijui wanabana kwasababu gani sijui kwanini BOT wanabana.
Skrill waliapply ili iwezekani mtu kutuma ela kutoka account yake ya skrill kuja mpesa na tigo pesa wameomba waruhusiwe toka mwaka 2015 mpaka leo hakuna wakati kenya unaweza tuma ela toa skrill ikaingia mpesa. Na sababu wanazotoa hao skrill ni kwamba BOT hawajapitisha ombi lao.
Haya mambo yanakwamisha sana hasa watu wanaolipwa kutoka nje bank wire ni expensive na inachukua muda wakati mobile wallet ni cheap na zinasave muda.
BOT kama mko humu jaribuni kuangalia hili jambo maana kama mnataka kwenda na kasi ya mabadiriko angalieni upande wa pili wa shilingi watu wengi wanashindwa kupata vipato vyao on time.
Mbona wazungu hawajaruhusu mpesa?
 
Ukiwauliza!! Sababu watakazotoa ndyo zile zile za kuwakatalia diaspora kuwa na uraia wa nchi mbili.... Ni uoga uoga mpaka basi naskia hta m pesa ilikubaliwa kwa mbinde tena baada ya mabepari kuweka presha
 
Tanzania ili uishi kwa amani inakubidi kuwa ZWAZWA FULANI, ZOBE ZOBE na KULA KULALA YES MAN - DREAMLESS !

Ukijishughulisha tu kidogo UTAKWAMA.

Ukifuatilia wenzio nchi nyingine wanaishije UTAPATA STRESS BURE !

Ukitaka hata kufanya kiujasiriamali UTAKWAMISHWA NA SHERIA KOKO kama SIYO KWENDA JELA.

Tanzania ndio Taifa lenye MADOCTOR + MAPROF MAZWAZWA EVER
Umemaliza. Over!
 
ujamaa umetudumaza, nchi imejaa watu waoga waoga na wenye hofu na mambo mapya. na ndio maana hata wanausalama wa nchi hii wanakikumbatia sana kile chama cha kijani na cha zamani, wana hofu na mabadiliko!!
I said it
 
Ukiwauliza!! Sababu watakazotoa ndyo zile zile za kuwakatalia diaspora kuwa na uraia wa nchi mbili.... Ni uoga uoga mpaka basi naskia hta m pesa ilikubaliwa kwa mbinde tena baada ya mabepari kuweka presha
Hata pass za kusafiri utasikia ni za kufuata nyumbani hata kama uko peru
 
Simba na yanga zilikataliwa kumilikiwa kwa zaidi ya 50% na mtu binafsi kwa sababu ya UOGA wa serikali same na hii ishu ya pay pal unaweza kuta wanaogopa pay pal kutumika kukusanya michango ya vyama vya upinzani....kwa kifupi jambo lolote linalotishia uwepo wa chama tawala lazima litawekewa vikwazo hta km lina manufaa kwa nchi
 
Mbona wazungu hawajaruhusu mpesa?
Wazungu hawahangaiki kutuma ela kama sisi, tunahitaji nunua vitu kutoka kwao tunahitaji kulipwa kwa kazi tunazofanya world wide fikiria nje ya box kuwa tatizo siyo kuruhusu mpesa kwao tatizo ni kuruhusu interaction uweze pokea ela kwenye mpesa kutoka platform mbalimbali uweze pokea ela kwenye akaunti ya bank kutoka paypal.
Kama wanahisi hatufai kutumia hivyo vya wazungu basi watengeneze mfumo wa pesa unaofanya kazi karibu dunia nzima kama ilivyo paypal
 
Back
Top Bottom