Hivi kwa nini hatuna ajira? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kwa nini hatuna ajira?

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Mr.creative, Sep 8, 2011.

 1. M

  Mr.creative JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2011
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 504
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Mwana jf unaweza kutoa sababu ya vijana wengu wa tz kukosa ajira ijapokuwa wengine wamesoma lakini hawana ajira?
   
 2. Straddler

  Straddler JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2011
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Waulize Idara ya uhamiaji.
  Kuna wimbi kubwa sana la Makaburu wanashikilia ajira pasipokuwa na utaalam wowote.
   
 3. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ajira zipo nyingi sana ila tatizo la vijana wetu wamezidi usharobaro wa kuchagua kazi. Waache wapigike tu ili wapate akili
   
 4. Amyner

  Amyner JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 2,404
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Kwanini uajiriwe.. Ever thought of kujiajiri?!
   
 5. Wang'wise

  Wang'wise JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 273
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa sababu employers ni wachache ku accomodate graduates wote. We need to think of creating employment than b employed
   
 6. MkimbizwaMbio

  MkimbizwaMbio JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hivi lazima kila mara uropoke???
   
 7. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,370
  Trophy Points: 280
  mkuu, katika hii post wakati ninaisoma mwanzoni nilisema 'huyu ameropoka tu' lakini baada ya kutafakari kidogo, nimegundua kuna ukweli ndani yake, vijana wanataka kazi za kupata pesa haraka haraka, hawataki kazi ambazo hawatakaa ofisini. Kweli bhana, tz kuna kazi sema tu vijana wa sasa hawajitumi kibishi, hawajui ku-hustle!
   
 8. l

  lulu chodota New Member

  #8
  Sep 8, 2011
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tatizo ni kwamba tumejengwa na dhana kwamba watu weupe ni bora kuliko wazawa na kwasababu hiyo wanapata nafasi kubwa katika ajira mfano katika tenda za ukandarasi wazawa wanasahaulika na kuona kuwa hawawezi kumbe wana uwezo mkubwa tu ila hawajapewa nafasi waonyeshe uwezo wao.
   
 9. N

  Ndaga Senior Member

  #9
  Sep 8, 2011
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 164
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  Ingekuwa wote watanzania wana ufahamu huu nitakaoelezea hapa, basi Tanzania ingekuwa hazina ya Africka kama si dunia yote;

  Kwanza, katika nchi inayotaka kuendelea kiuchumi haitegemei ajira za serikali ndo ziwawezeshe watu kufanikiwa kiuchumi na kuinua uchumi wa nchi yao, rahasha;bali hutegemea sector binafsi ya ubunifu na ujasiri wa kuanzisha kazi au kampuni zitakazoibua uwekezaji katika nyanja mbalimbali siyo kutegemea kuajiriwa na serikali.

  Ukitazama Nchi zilizoendelea sector binafsi ndizo zinazoongoza si tu kuingiza kipato kikubwa cha kodi serikalini bali kulipa mishahara mikubwa kwa watendaji wake aidha wawe ndo waanzilishi au wale wanaopenda kuajiriwa kwalo ilimradi wakidhi vigezo vya ubunifu na ujasiri katika nafasi zao.

  Pili, Vijana tuache uvivu na uharaka wa kuwa na kipato kikubwa kwa wakati mfupi ' haiwezekani' na hakuna principle yoyote itakayokupa nafasi ya kufanikiwa kwa muda mfupi labda uwe jambazi au muuza madawa ya kulevya nako kuna risk zake ambako maisha yako yatakuwa hatarini kila sekunde.

  Nakumbuka nilipokuwa namaliza degree yangu ya kwanza, cha kwanza niliangalia mahitaji ya jamii yangu yaani nchi yangu kwe elimu niliyopata, nikaona fursa ni nyingi sana hasa huko wilayani, nikaanzisha kampuni nikavumilia mwanzoni mwa kazi zangu za awali, kadri miaka ilivyokuwa inasonga ndivyo nilivyozidi kupata uzoefu na wigo mpana zaidi, nikaungana na wenzagu tukapata miradi mingi na tukaajiri wenzetu ambao hawako tayari kuwa wabunifu tukawapa TOR (miongozo) yetu ya utendaji; kwanza wawe tayari kufanya kazi wakati wote ufaao na usiofaa, usiku na mchana kwa muda wa miaka mitatu na baada ya hapo watapata share katika kampuni, wengi walikataa, wachache wakakubali wastrive na tukawapa share, sasa wale waliokataa hadi huvi leo wanahaha wanagonga nauli za daladala kila kukicha, wenzao tuko ndani ya viyoyozi hata kama ni Vitz lakini tunamiliki kihalali kupitia ubunifu wetu.

  Tatu,Tuache kulalamika na kuinung'unikia serikali ingawa inastahili kupigiwa kelele kwa kuwa na Viongozi wanaoibeza nchi yao kuwa ni masikini na kuendelea kuomba fedha za misaada kwa hao wanaochuma maliasili zetu,hii nchi ina kila kitu tamka unachoweza kutamka kipo katika nchi, fikiri mwenyewe anza sasa hujachelewa nenda wilayani utokako au ulikowahi kufika kaangalie fursa mbalimbali anza polepole,Nina uhakika kama utaanza leo hicho unachofikiri baada ya miaka mitano itakuwa legacy.

  Nne; Uspende kuajiriwa penda kuajiri wengine ndipo utakapopata kile unachotamani kuwa nacho katika mawazo yako, inakuweje unafikiria kununua au kujenga nyumba au kuwa na mshahara mkubwa kwa maono ya mwingine hutafanikiwa kwa wakati utakao! huwezi jua labda huyo aliyekuajiri atasitisha au kukuachisha kazi akizidiwa au akifirisika!

  Tano, Jamii forum ni maono ya mtu na alianza kama wazo limekuwa kama lilivyo kwakuwa alikuwa jasiri na mbunifu wa nini anataka awe na nini anategemea kupata na sasa anaweza kupanua wigo kibiashara si haba atapata chai ya watoto na atafika mbali kama atakuwa mbunifu zaidi na itafika mahali tutakuwa tunalipia hata haya tunayoyaandika hapa maana hii ni huduma.So be creative my bretheren!

  Sita, Usipende kujilinganisha na mtu alivyofanikiwa huwezi jua alivyofanikiwa na amechukua muda gani kufika hapo, wewe chukua hiyo kuwa ni changamoto na ujifunze kuwa na bidii na kuvumilia acha kuwa kama mimi wakati wewe si kama mimi ni wewe na utabaki wewe na una destination yako.

  Saba, Mtegemee Mungu naye atakusaidia.No Vision No Provision.

  Ndaga,
   
 10. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #10
  Sep 8, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  <br />
  <br />
  Toa mifano ya kazi zilizopo.
   
 11. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #11
  Sep 8, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Umesoma na kuishia level gani na results zako zipoje.
   
 12. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #12
  Sep 8, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,146
  Trophy Points: 280
  Siamini kabisa kama hakuna ajira Tanzania. Tusingeona waajiri wengi wakileta waajiriwa kutoka nje ya Tanzania.

  Mimi naona hakuna waajiriwa Tanzania. Tanzania tulijazwa ujing wa kuwa kila kitu ni mali ya umma, sasa muajiriwa akianza kazi hata leo anajiona kuwa ile ni mali yake na anaweza kufanya anachotaka.

  Waajiriwa wa Tanzania, hawaishi kufiwa, kuumwa, kuwa na shughuli binafsi wakati wa kazi, kutoka kwenda kunywa chai wakati wa kazi, kuchelewa kazini, kuzembea, uvivu, kuona waajiri wao (mabosi zao) wajinga, kutumia kwa wizi mitandao ya wa muajiri kama yao binafsi (kuingia JF n.k), wezi (kazi kama haina mishe hawaitaki). Kwa kifupi hawakosi sababu za kutojituma.

  Kuna tajiri mmoja aliniambia, gharama za kuajiri Watanzania kumi sawa na kuajiri Mhindi mmoja, Kwanini nisiajiri Mhindi?

  Ukweli ni kwamba hata mimi kila nnapoweza ku 'avoid" kuajiri Mtanzania huwa siajiri. Hata House Girl wangu ni kutoka Malawi, Watanzania wamenichosha kwa visingizio, uzembe na kutokuwajibika.
   
 13. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #13
  Sep 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,091
  Likes Received: 6,558
  Trophy Points: 280
  tz kila kitu ni lazima uzunguke mbuyu;
   
Loading...