Hivi kwa hii hali Dr Slaa ni kiongozi wa serikali au ni katibu mkuu wa chama cha siasa tu?

Kweli Mkuu kama tuna mawaziri vivuli na waziri mkuu kivuli (KUB) kwa nini tusiwe na Rais Kivuli na Makamo wake Kivuli?
no is a ghost president yaani hakai magogoni lakini anaongoza, akipita watu wanajitokeaza kumlaki,ukiangalia mioyoni mwa watanzania unamuona! kuna rafiki yangu mkenya huwa ananiuliza kila mara kuwa rais dr.slaa hajambo? yaani hata wakenya wanajua kuwa ndio chaguo la watanzania kama sisi tunavyojua kuwa kipenzi cha wakenya ni raila,waganda ni dr.besije, kongo ni etiene na zanzibar ni maalim seif
 
Mie naunga mko hoja iliyowahi kutolewa mwaka jana kwa JK ni wa NEC-uchaguzi na ANATAWALA akiwa ikulu wakati Dr.Slaa ni rais wa wananchi na ANAONGOZA akiwa nje ya ikulu
 
Unaambiwa kwa kilomita 22 walikuwa pembeni ya barabara wengine wakiwa mbele ya gari laki wengine wakiambatana na gari wakishangilia kwa vigelegele na shangwe ,Polisi mmoja alisikika akisema nchi imefilisika, maisha yamekuwa magumu watu wana hasira na serikali leo hii hawa wananchi wanaomuona Dr Slaa mkombozi wao tuwazuie waje watugeuzie kibao cha kutuadhibu sisi waache watembee naye mpaka kiu yao iishe , kwa maana nyingine kulikuwa na maandamanao ya mapokezi wakimpokea Raisi wao wa mioyoni

Ukiona hivyo wivu utamjaa KIkwete mtasikia kamanda wa polisi mbeya anarudishwa makao Makuu bench....Kama Yule kamanda wa polisi Arusha ...pamoja na busara Yake iliyookoa Arusha kuwa Lindi la damu..hivi sasa yupo bench la nguvu makao Makuu....kazi Yake ni kukaa kwenye kaofisi kadogo..,LASIK kuwa na faili..judoka magazeti ,kunywa chai na ku chat na kukimbizana na mabinti wanaodeki .....sasa afanyeje......kwa walio serikalini wanajuwa maana ya bench......unasubiri mshahara tu....hakuna cha overtime,safari wala semina.....ni frustrations kwa kwenda mbele...
 
Umenikumbusha kitu mkuu machozi yananilenga

kweli mkuu nakumbuka siku aliyokuja akitoka zanibar kutafuta wadhamini nilikuwepo pale mwl jk.airport, halafu tukaja naye taratibu mpaka jangwani,huku helkopita ikuruka juu nakumbuka watu walivyotaka kutandika nguo zao chini ili akanyage akakataa akisema kwa imani yake hiyo itakuwa kufuru.
 
ndo mama mungu anambariki
 
slaa-na-sugu.jpg

Dk. Slaa akikaribishwa na mbunge wa mbeya mjini, Mh. Joseph Mbilinyi mara baada ya kuwasili maeneo ya Uyole jijini Mbeya jana jioni.

Baadhi ya wabunge na wanachama wa Chadema wakimsikiliza kwa makini Dk Slaa mara baada ya kuwasili jijini Mbeya jana jioni.

Dk. Slaa akishangiliwa na wanachama wake alipokuwa akipita maeneo ya Mwanjelwa jijini Mbeya jana jioni.

DSC00463.JPG
Hapa ndugu zangu nimejiuliza maswali mengi sana kuwa kama Dr Slaa ni katibu mkuu wa chama cha siasa (chadema) na si kiongozi wa serikali, na wananchi wanampokea zaidi ya rais, kiashilio chake ni nini??, je Maalimu seif hupokelewa hivi kama katibu mkuu wa CUF? Katibu mkuu wa ccm Mkama je nae hupokelewa hivi??
Hayo ndoo maswali yangu machache kwa JF.

una umri gani? 1995 Mrema alikuwa na nyomi nchi nzima mpaka lindi na Mtwara,hilo halikumfanya kuwa Rais,2015 kama mna ndoto za kwenda Ikulu itakuwa kupigwa dozi ya kikombe cha juice baada ya kupata gonjwa la kukataa matokeo!!
 
Mzee slaa miaka inavyokwenda remind me of an old, dying dog with just a few kicks left in it. anatembea mikoa CDM inaguvu ili ajipe moyo hayo mapokezi ya Mbeya was one of those kicks.......

Una haki yako ya kimsingi ya maoni ila usifikiri ile mikoa walikuwa wakiisujudia ccmtmpaka sasa wanaendelea na uvumilivu waliokuwa nao tangia 2005 hadi na 10 wamekwisha kuona mwelekeo mbovu wa serikali ya Magamba na ndo maana takwimu zilizofanya mwaka jana zilionyesha kama uchaguzi ungefanyika dr. Slaa angeshinda yote hayo yalitokana na mwenendo mzima wa serikali ya Jk
 
Hiyo ni meseji kwa magamba 2015 wajiandae sehem za kuiba kura maana kuna mikoa wa akosa kura hata moja
 
una umri gani? 1995 Mrema alikuwa na nyomi nchi nzima mpaka lindi na Mtwara,hilo halikumfanya kuwa Rais,2015 kama mna ndoto za kwenda Ikulu itakuwa kupigwa dozi ya kikombe cha juice baada ya kupata gonjwa la kukataa matokeo!!
nakumbuka 1995 ile ilikueww nguvu ya mrema lakini hii ni nguvu ya umma yaani ni mbingu na ardhi
 
Dr Slaa ni kiongozi anayependwa na wananchi kwa record/CV yake iliyochapwa kwenye kila moyo wa mtanzania mwenye uzalendo na uchungu na jinsi tunavyofanywa masikini na watu wachache. msimamo wake katika ufisadi serikalini ni wa kitakatifu kwa viwango vyote vya dini yoyote inayomwabudu Mungu wa Ukweli.
Hata wanaombeza kwa kutumia dini, hawana ubavu wa kupinga hoja zake wakiwa wameshika vitabu vyao vitakatifu. Maana vitabu vyote vya Mwenyezi Mungu huhimiza uadilifu na kupinga dhuluma. Haya ndiyo anayoyafanya Dr Slaa kwa nguvu na moyo wake wote.
Mwenyezi Mungu amzidishie Upeo, Hekima na zaidi sana afya njema na maisha marefu na kumlinda na kila njama za maadui zake maana kazi anayoifanya ni kazi ya Mungu.
 
Sugu ongeza bidiii, kuwa msikivu kwa wakubwa zako ndio na wananchi waliokuchagua kama unavyoonekana pichani
 
Ukiona hivyo wivu utamjaa KIkwete mtasikia kamanda wa polisi mbeya anarudishwa makao Makuu bench....Kama Yule kamanda wa polisi Arusha ...pamoja na busara Yake iliyookoa Arusha kuwa Lindi la damu..hivi sasa yupo bench la nguvu makao Makuu....kazi Yake ni kukaa kwenye kaofisi kadogo..,LASIK kuwa na faili..judoka magazeti ,kunywa chai na ku chat na kukimbizana na mabinti wanaodeki .....sasa afanyeje......kwa walio serikalini wanajuwa maana ya bench......unasubiri mshahara tu....hakuna cha overtime,safari wala semina.....ni frustrations kwa kwenda mbele...

Basilio Matei huyo mkuu, ila kwa sasa kala shavu kama kawaida kapewa kitengo cha polisi jamii.
Yule ni kamishna mkuu anakula kiyoyozi tu.
 
Back
Top Bottom