Hivi kusoma ni kugumu kiasi hiki?

LINCOLINMTZA

JF-Expert Member
Mar 15, 2011
1,639
516
Kwa matokeo haya ya kidato cha nne, wanafunzi wengi wamepata divison zero yenye F zote. Hii kwamba hawawezi kusoma, wavivu, au matatizo ya shule? Hata kama ni hivyo, basi naona kusoma ni kugumu sana. Ukimwona mtu alipata au amepata division one, basi anasitahili pongezi.

Wana JF, munasemaje?
 
Sidhani kama wanafunzi ni wabovu kiasi hicho. Kiasi cha kupata F zote kwenye masomo yao.
Kuna tatizo somewhere tena kubwa tuu wala sio dogo.
Ilikuwa nadra tena aibu kwa shule kuwa na zero 10 ila now unakuta shule haina Div 1 wala 2 wala 3 eti ni four na zero zinafukuzana
Tuseme wanafunzi wote hao hawajui kitu toka wameanza form one mpaka wanafikia kufanya mtihani wa mwisho
Je hakukuwa na report ya maendeleo ya wanafunzi toka wameanza form one
Je report hiyo ilionyesha nini
Mock exams si zilikuwa zinafanyika
Je walimu walichukua hatua gani baada ya kuona matokeo mabovu ya mitihani ya muhula na mock
Je hao walimu walivyowaangalia wanafunzi wao waliwaamini kuwa wameiva kuja kusit for final exams au ilikuwa bora mmalize muondoke
Je wanafunzi nao hawakuwa hata na vikundi vya kusoma among themselves hata vya wanafunzi wa shule nyingine wakabadilishana mawazo na materials au ndio wale walikuwa wote samaki wa kapu moja
Je tatizo ni walimu au tatizo ni wanafunzi
Je hizo shule ambazo mwaka jana zilikuwa na the same matokeo bado walimu ni wale wale wanaendelea kuzalisha zero au wamebadilisha wakajikuta aheri ya wale walioondoka
Je maofisa elimu wa wilaya na mikoa wanafanya nini kuhusu huku kuzalishwa kwa genge la vijana ambao hawana hata cheti cha kuombea kuuza duka kwa kuwa wana zero
Je walimu wakuu wa hizo shule bado wanaendelea kupokea mshahara wao kama kawaida
Maswali ni mengi sana ila naamini tatizo ni kubwa zaidi ya tunavyoamini. Sidhani kweli elimu imekuwa ngumu kiasi hicho kiasi cha asilimia sabini na tano ya baadhi ya shule kupata zero au four kwa wanafunzi wao
Tatizo sio elimu tuu bali kuna tatizo somewhere tena kubwa sana
 
Back
Top Bottom