Nimeingia kwenye ugomvi na girlfriend wangu baada ya kumtamkia maneno mabaya nikiwa na hasira. Sababu ya kufikia hatua ya kumtamkia maneno hayo ni baada ya yeye kunigombeza kwa sababu ya kumtafuta kwenye simu ya rafiki yake baada ya kumkosa yeye kwenye simu yake. Jambo hilo lilinikera sana kwa sababu sikuona mantiki ya yeye kunikoromea kwa sababu ya issue ndogo kama hiyo.Hilo lilipelekea nikapata hasira na kumtamkia maneno mabaya. Lakini baada ya hasira kuisha, niligundua kuwa sikufanya jambo jema kumtamkia maneno hayo, hivyo nikaamua kumwomba radhi kwa hilo. Kitendo cha kujishusha na kuomba msamaha imekuwa kama ndio nimewasha moto kwa sababu hataki kunisikiliza hata kidogo na hata simu hapokei, na hii ni wiki ya 3 hataki kupokea simu yangu? Halafu tatizo ni kwamba ninaishi mbali sana na yeye. Mimi nipo Shinyanga na yeye yupo Dsm. Nimejaribu kuhusisha baadhi ya marafiki zake wamweleweshe ili anisamehe, lakini ndio kwanza anazidi kuwa mkali. Cha kusikitisha ni kwamba nilipoanza tu kuomba msamaha alinitumia sms kwamba "ameamua tu-break up". Sasa najiuliza, hivi kuomba msamaha ni makosa? Wana JF naombeni maoni yenu.
... ulikua huna sababu ya kuendelea kujishusha
Mhh kwenye mahusiano wote tukipenda kuwa juu na kuogopa kujishusha kweli tutakuwa tunajenga au tunabomoa..., (although not on this case) lakini nadhani sometime mmoja kati ya couples inabidi awe a man enough (or a woman enough) na ajishushe, sababu as you know mafahari wawili hawakai zizi moja.... "unajua sometimes kwenye hizi battle unamuchia mwenzako ashinde, (although not in this case)"
Inaonekana siyo mara yako ya kwanza KUMGOMBEZA - sasa G/Friend unamgombeza...................... akiwa mke si ndio UTAMPIGA KABISA????
UMEMGOMBEZA MARA HII - kaamua hataki tena KUGOMBEZWA GOMBEZWA - anataka KUBEMBELEZWA...
WASEMAVYO; MKE HAPIGWI NA NGUMI - BALI ANAPIGWA NA NGUO................... mwombe MSAMAHA KWA GIFT ..... EXPRESS U R FEELINGS WITH GIFTS ..................... si unampenda????? KAZI KWAKO!!!!!!
ni kweli kuna watu "you give them an inch they take a mile" yaani wanatasfiri wema wako na upole kama ujinga.Kwa wengine hata ukijishusha, ndio unazidi kupandiwa juu . . . .
Kuna aina ya mtu kutaka kuabudiwa ukiona hivi
ni kweli kuna watu "you give them an inch they take a mile" yaani wanatasfiri wema wako na upole kama ujinga.
Hivi ukifanyiwa hivi unatakiwa uchukue hatua gani?
Asante!!Kuomba msamaha sio kosa ila jiulize ni maneno gani ulitumia. Je ni mara ya kwanza kutumia maneno hayo au huwa unarudia rudia? Je maneno hayo ya kashfa uliyotumia yanaukweli ndani yake? kuna maneno mengine yana -touch sana..na pia mwenzako anaweza kuwa ametafsiri vibaya... na yataendelea kutawala kichwani kwa muda mrefu kwani ni kashfa lakini kweli...Mfano.. umemsadia sana rafiki yako..yaani bila wewe asingekuwa hapo... unaweza kutoa neno moja la kashfa na kuhusisha msaada huo.. hili litachoma moyo..kwani utakuwa umemuua..kwani unayosema ni kweli..kama dhiki ni kweli..lakini hana jinsi..mtu kama huyu itachukua muda kusahau kashfa yako..anaweza kukata mawasiliano hata kama anakupenda kupita kiasi...kwani maneno yako yamevunja mifupa na yanajirudia mara 100 kwa siku..Ushauri wangu fikiri maneno uliyosema na background ya uhusiano wenu.. anaweza kukusamehe..lakini itachukua muda kusahau kwani utakuwa umepiga sehemu mbaya..ila usikate tamaa kama una nia ya kweli na usirudie tena..
Mhh kwenye mahusiano wote tukipenda kuwa juu na kuogopa kujishusha kweli tutakuwa tunajenga au tunabomoa..., (although not on this case) lakini nadhani sometime mmoja kati ya couples inabidi awe a man enough (or a woman enough) na ajishushe, sababu as you know mafahari wawili hawakai zizi moja.... "unajua sometimes kwenye hizi battle unamuchia mwenzako ashinde, (although not in this case)"
Kweli mkuu, huyo anataka kumchota akili demokrasia wetu!Kaka demokrasia,...ukizidisha hiyo demokrasia ni kero,...kama vip mpotezee mpaka aje mwenyewe,asipo kuja we sepa kivyako bana.