Hivi kuna watu wanatumia Kifurushi cha Internet cha Tigo?

Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
26,132
34,104
Habarini Wadau,

Kwa kawaida huwa natumia kifurushi cha mwezi cha Vodacom, ila kimekata ghafla usiku huu na sikuwa na pesa yoyote ya kujiunga na kifurushi kingine

Ila kwenye line ya Tigo nina 4.7 GB ambazo huwa nazawadiwa na Tigo yaani MB 500 kila mara

MAAJABU SASA, yaani nimejaribu kufungua chochote hata Jamii Forums App haifunguki. Kuingia Twitter hata picture tu haifunguki achilia mbali video clips

Hivi kweli Tigo Tanzania mnaweza kusema nanyi mnaprovide huduma ya Internet? Au ni geresha tu?
 
Hivi kweli @Tigo Tanzania mnaweza kusema nanyi mnaprovide huduma ya Internet? Au ni geresha tu?
Tatizo hapa nchini ni kwamba kasi ya intaneti inayotolewa na watoa huduma wa intaneti (ISP) hutegemea eneo alipo mtumiaji.

Hivyo ni jukumu lako kutafiti na kugundua ni mitandao ipi ina kasi kubwa eneo ulilopo.

Kwa mfano, hapa nilipo, Tigo inanipatia kasi kubwa ya intaneti kiasi kwamba wakati mwingine nalazimika kubadilisha "settings" ili kutumia 3G pekee ili niweze "angalau" kutumia kiwango cha GB nilichopanga kwa siku husika, kuepuka kununua GB zaidi nje ya hesabu.
 
Habarini Wadau,

Kwa kawaida huwa natumia kifurushi cha mwezi cha Vodacom, ila kimekata ghafla usiku huu na sikuwa na pesa yoyote ya kujiunga na kifurushi kingine

Ila kwenye line ya Tigo nina 4.7 GB ambazo huwa nazawadiwa na Tigo yaani MB 500 kila mara

MAAJABU SASA, yaani nimejaribu kufungua chochote hata Jamii Forum App haifunguki. Kuingia Twitter hata picture tu haifunguki achilia mbali video clips

Hivi kweli Tigo Tanzania mnaweza kusema nanyi mnaprovide huduma ya Internet? Au ni geresha tu?

Sasa hivi tigo ukiweka GB1:4 kwa sh 3000 ndan ya nusu saa zimeisha kwa kufingua app za kawaida kama JamiiForums au whats app hivi tatzo ni nin?TCRA waingilie kati hizi mitandao tunakoelekea ni pabaya sana aisee
 
Tatizo ni kasi ya internet na GB 1.4 ni kidogo sana, binafsi napata GB 30 kwa mwezi ila bado ni ndogo sizitumii kwa kujiachia maana hazitatoboa mwezi.

Kingine angalia kwa mwezi unatumia kiasi gani cha pesa kujiunga na vifurushi vya data ukiona unazidi 30000 basi jiunge na vifurushi vya postpaid utaokoa gharama kubwa sana.
 
Sasa hivi tigo ukiweka GB1:4 kwa sh 3000 ndan ya nusu saa zimeisha kwa kufingua app za kawaida kama JamiiForums au whats app hivi tatzo ni nin?TCRA waingilie kati hizi mitandao tunakoelekea ni pabaya sana aisee
Tumelalamika sana tena sana lkn TCRA hawajali maana nadhan wao si wanahongwa na makampuni ,
 
Back
Top Bottom