Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,258
- 20,708
Sikumbuki kama jambo hili lilishajadilia,lakini hata kama tayari lilishajadiliwa nilitaka kujua na nina sababu.Ni kwamba tangu nizaliwe sijawahi kuona ndoa ya uke wenza ina amani baina ya hao wake wawili au wa idadi yoyote.Miezi miwili iliyopita kuna binti aliolewa na mume mwenye mke tayari,lakini leo binti ameachika na amerudi kwao kwa sababu,tangu ameolewa vurugu na mke mkubwa haziishi,bi mdogo kuumwa kila leo,akipelekwa hospital ugonjwa hauonekani,lakini watu wazima wamemwambia kuwa ake mwenzie ndie anamroga!Nae binti kusikia hivyo amefungasha na kuondoka kwa mumewe na anadai talaka.Huo ni mfano mmoja,najua iko mingi,nimekua nikijiuliza sana;hivi kuna mwanamke anakubali kushea mume na mwanamke mwenzie bila kulazimishwa na dini,umaskini,wazazi au mila?Kama hakuna kwanini wanawake waendelee kujitesa na ndoa hizi?Au wapo wanakubali ndoa hizi?Kama wapo ningependa kusikia kutoka kwao . . . . . . !!!!