Ilikuwa orodha ya watuhumiwa wa ufisadi na si mafisadi. Lowassa ameshasema yeye hausiki na mhusika ni Kikwete. Hivyo Lowassa anatolewa rasmi kwenye listi ile ya watuhumiwa na mtuhumiwa hapa ni Kikwete.
Hata kwenye kutajwa kwa Lowassa kwenye maeneo mengine ukiacha Richmond bado ni kumtuhumu tu. Serikali iliyokuwepo madarakani wakati huo ilikuwa na jukumu la kumburuta mahakamani ili ajibu tuhuma kama zilikuwa na ushahidi wa uhusika wake kwenye matukio hayo. Kwa nini haikufanya hivyo?
Kama kweli Lowassa alihusika katika wizi anaoutuhumiwa, basi Serikali ya wakati huo nao ni wezi kwa kushindwa kumchukulia hatua kama walikuwa na ushahidi kwa sababu huwezi kumuacha mtu anaiibia Serikali mabilioni ya pesa bila kuchukua hatua yoyote kama wewe mwenyewe sio mwizi.
Sasa kwa issue ya Magufuli hii iko wazi kabisa kwamba kuna ushahidi wa kitaalam uliotolewa na CAG kwamba alitunga mradi hewa wa ujenzi wa barabara na kuupatia namba hewa ili kuiba mabilioni ya walipa kodi.
Inaingia akilini namna gani mtu ambaye amethibitishwa kuwa mwizi wa mali ya umma aliyekubuhu kwa kudanga mradi pamoja na namba ya mradi ndio huyo CCM inatuletea eti tumpigie kura ya kuwa Rais wa Tanzanina?
Kama aliweza kuiba mabilioni wakati akiwa waziri, ni wazi kwamba ataiba matrilioni akiwa rais tena bila kutunga uongo wa kuhalalisha wizi wake bali atakwapua mchana kweupe bila justification yoyote ile hata ya uongo.
Kwa nini CCM watuletee mwizi aliyekubuhu kwenye kinyang'anyiro cha mgombea urais? Bila shaka ni kwa sababu waliompigia debe ili agombee ni wezi wenzake ili waendelee kuliibia taifa hili kupitia mgongo wa mwizi mwenzao atakapoingia ikulu.
Watanzania mumuogope Magufuli kama Ebola ama sivyo nchi itafilisiwa kabisa katika kipindi chake cha mwaka mmoja tu.
Ilikuwa orodha ya watuhumiwa wa ufisadi na si mafisadi. Lowassa ameshasema yeye hausiki na mhusika ni Kikwete. Hivyo Lowassa anatolewa rasmi kwenye listi ile ya watuhumiwa.
KILIMANJARO , ARUSHA NA MANYARA- WALISUSA KUJIANDIKISHA BVR- LOWASA ATAISOMA NUMBER.
MKUKI WA KULENGEA HUU HAPA; ASUBUHI NA MAPEMA ; CCM BIASHARA WALISHAMALIZA.
UKANDA WA KASKAZINI WAMEMSUSA SASA WA NN HUKU
TUNAENDELEA. Hili ndo jibu pekee nililohitaji the rest was simply inconsequential.
Kumbe ni watuhumiwa tu? Toka lini mmegundua kuwa ni watuhumiwa na siyo mafisadi kama mlivyokuwa mnaimba?
Sasa rudini pale pale Mwembeyanga mkayaseme haya mtupe na sababu ni kwa nini mliamua kutudanganya na kwa manufaa ya nani.
Na kama mlitudanganya basi mtushawisi upya kwamba mtakachotuambia tena hakitakuwa uongo otherwise tuwapuuze milele.
Hivi wewe mtu akikuambia tu hahusiki halafu anakutajia mtu mwingine bila hata kuweka ushahidi wowote unakubali?
Unakuwa una akili kweli?
Halafu ni wapi alimtaja Kikwete kama mhusika? Weka clips kama unazo.
Alichokisema ni mamlaka za juu na kwa sisi walokole hakuna mamlaka za juu duniani instead iko mbinguni tu.
Sasa kama hakukubaliana na hiyo mamlaka kwa nini hakuachia ngazi?
Twende taratibu.
Nauliza swali hilo kwa kigezo kimoja tu nacho ni wizi wa mali ya umma.
Lowassa anatuhumiwa kwenye wizi wa Richmond bila ushahidi wowote ule mpaka sasa. Wanaomtuhumu ni walewale ambao wanaoweza kuwa na ushahidi ambao kama kweli alikwapua basi walitakiwa wawe wameshamburuta mahakamani tangu wakati ushahidi ulipopatikana kama kweli wanauchukia wizi wa mali ya umma na kama kweli wao wenyewe sio wezi.
Magufuli sio tu anatuhumiwa bali kuna ushahidi wa kitaalam uliotolewa na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) ukimuhusisha na taarifa za uongo za kudai mabilioni ya pesa yametumika kujenga barabara wakati sio hivyo. Ni wazi kwamba Magufuli kakwapua hizo hela na hivyo HAFAI KUKAA IKULU HATA SEKUNDE MOJA.
Sasa jiulizeni hivi CCM imeshindwa kuja na mgombea wake ambaye sio mwizi? Kwa nini waweke mgombea ambaye ni mwizi kama wao wenyewe sio wezi?
Kifupi ni kwamba Magufuli atapigiwa kura tu na wezi wenzake wanaoliibia taifa hili usiku na mchana bila kunawa na hivyo kulifanya taifa hili lenye rasilimali lukuki kuendelea kuwa taifa masikini.
Watanzania wote wenye uchungu na nchi yao kama wamepewa kuchagua wa kumpigia kura kati ya mtu anayetuhumiwa tu bila ushahidi wowote na ambaye ameshathibitishwa kwamba ni mwizi na taasisi maalum yenye utaalamu kuhusu uthibitishaji huo basi watapiga kura kwa yule ambaye hajathibitishwa kwamba ni mwizi.
Je wewe kura yako iko kwa nani kati ya hawa wawili?

Low hasa atopata kabisa kura yangu
Vigezo
1.Afya mbovu
2.sio mwadilifu
3.tamaa ya madaraka
4.mbadhilifu
5.anatumia pesa kununua wapga kura
Gud example ni chuoni kwe2 udom tumegegeda hela zake nimenunua plate 2 za jiko la gesi na samsung oven,hvyo
HAFAI ATABAKI KUWA LOW TENA HASA
Naona kama swali liko kinyume. Nadhani wa kupimwa akili ni atakayempigia Lowasa mtu ambaye Chadema walihifadhi ushahidi wa ufisadi wake kwa miaka 8 lkn wakamsafisha kwa wiki moja na kubadili agenda eti ni "mfumo". Mfumo ni nini kama sio lowasa, mbowe na mtei nk? (WATU).
Siku hizi hakuna shule. Vijana mnaingia tu madarasani kutimiza wajibu. Sasa hapo unajibu hoja yangu au unajaza tu server.
Sasa una quote post yangu halafu unaweka utumbo huu ambao hata hauhusiani na points zilizopo kwenye post yangu!!! Jibu hoja au kaa kimya. Anzisha thread yako upost huo utumbo wako.
Hapa tunajadili masuala nyeti ya mustakabali wa taifa letu na kuweka hoja kwa nini Magufuli HAFAI KUINGIA IKULU HATA SEKUNDE MOJA. Jibu hoja hizo kama unataka kuchangia kwenye post hii.
Kama ushahidi ulikuwepo kwa nini Serikali isimburute mahakamani? Mbona mnashindwa kujibu swali rahisi sana? Hela zile zimeibiwa Serikalini zikiwa hela za walipa kodi. Anayetakiwa kuwa na uchungu wa wizi ule kwanza ni Serikali kwa sababu yenyewe ndio imepewa dhamana ya kulinda na kutumia vyema kodi za wananchi. Sasa iweje wamuache Lowassa apete na hela za wizi wa mali ya umma mtaani kipindi chote hicho mpaka leo?
Mimi sijadili CHADEMA hapa wala CCM. Nawajadili watu wawili ambao ni Lowassa na Magufuli ni nani mwenye afadhali kulinganisha na mwingine. Na nimeelezea jinsi wizi wa Magufuli ulivyo wazi na wenye vithibitisho ukilinganisha na tuhuma kwa Lowassa.
Sasa hii ndio hoja inayotawala post yangu hii na wanaojikita kwenye post hii waji confine kwenye boundaries za theme ya post hii na si vinginevyo.