Hivi kuna mtu mwenye akili timamu atakayempigia kura yake Magufuli na kumuacha Lowassa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kuna mtu mwenye akili timamu atakayempigia kura yake Magufuli na kumuacha Lowassa?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mendz, Aug 19, 2015.

 1. m

  mendz Senior Member

  #1
  Aug 19, 2015
  Joined: Dec 9, 2013
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nauliza swali hilo kwa kigezo kimoja tu nacho ni wizi wa mali ya umma.

  Lowassa anatuhumiwa kwenye wizi wa Richmond bila ushahidi wowote ule mpaka sasa. Wanaomtuhumu ni walewale ambao wanaoweza kuwa na ushahidi ambao kama kweli alikwapua basi walitakiwa wawe wameshamburuta mahakamani tangu wakati ushahidi ulipopatikana kama kweli wanauchukia wizi wa mali ya umma na kama kweli wao wenyewe sio wezi.

  Magufuli sio tu anatuhumiwa bali kuna ushahidi wa kitaalam uliotolewa na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) ukimuhusisha na taarifa za uongo za kudai mabilioni ya pesa yametumika kujenga barabara wakati sio hivyo. Ni wazi kwamba Magufuli kakwapua hizo hela na hivyo HAFAI KUKAA IKULU HATA SEKUNDE MOJA.

  Sasa jiulizeni hivi CCM imeshindwa kuja na mgombea wake ambaye sio mwizi? Kwa nini waweke mgombea ambaye ni mwizi kama wao wenyewe sio wezi?

  Kifupi ni kwamba Magufuli atapigiwa kura tu na wezi wenzake wanaoliibia taifa hili usiku na mchana bila kunawa na hivyo kulifanya taifa hili lenye rasilimali lukuki kuendelea kuwa taifa masikini.

  Watanzania wote wenye uchungu na nchi yao kama wamepewa kuchagua wa kumpigia kura kati ya mtu anayetuhumiwa tu bila ushahidi wowote na ambaye ameshathibitishwa kwamba ni mwizi na taasisi maalum yenye utaalamu kuhusu uthibitishaji huo basi watapiga kura kwa yule ambaye hajathibitishwa kwamba ni mwizi.

  Je wewe kura yako iko kwa nani kati ya hawa wawili?
   
 2. Crocodiletooth

  Crocodiletooth JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2015
  Joined: Oct 28, 2012
  Messages: 9,646
  Likes Received: 3,514
  Trophy Points: 280
  ------->>>>Endapo atatokea wa kuipigia ccm italazimu kwanza AKAPIMWE AKILI YAKE

  NDANI YA CCM 75% NI TIMU LOWASA!!
   
 3. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2015
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,796
  Likes Received: 13,802
  Trophy Points: 280
  Mbona unaongea kinyume? Mataahira wote na misukule ndio watakaompigia kura Lowasa
   
 4. Lizaboni

  Lizaboni JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2015
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 33,796
  Likes Received: 13,802
  Trophy Points: 280
  Siku zote ni CCM ndio inayopigiwa kura. Hao wengine ni wasindikizaji tu
   
 5. N

  Nyambiti Senior Member

  #5
  Aug 19, 2015
  Joined: Jul 27, 2015
  Messages: 160
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wewe ndo hauko timamu!!!
   
 6. congobe

  congobe JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2015
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 504
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  KWELI na hakika ,
  wa mguse Lowasa waone wote ccm wanaingia jela ,Malaika wema wamemuitaji Lowasa ,ila malaika waovu wanamlilia arudi kwao ,
  nape alijua kusema rufaa imefungwa hadi uchaguzi umalizike,atakuwa amemweka lock up Rais Lowasa.
  taharuki ni pale kaibukia upande wa adui ,
  anacheza na Lowasa jeshi la Ukawa .
   
 7. C

  CHADODO Member

  #7
  Aug 19, 2015
  Joined: Aug 11, 2015
  Messages: 89
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Ushahidi wa wizi wa EL anao Dr Slaa huko mafichoni.Huo wizi Magufuli unaujua wewe tu..
   
 8. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2015
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,673
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Mtu anayempigia mtu ambaye kwa miaka mingi amekuwa akitangazwa ni mchafu kimaadili na mpaka alitimuliwa ktk ofisi ya umma kwa kushindwa kuwa muadilifu ghafla tena baada ya kuambiwa na chama chake kuwa yeye bado hana sifa za kuwa kiongozi muadirifu then wewe unampigiaje kura mtu wa sampuli hiyo. Mtu ambaye atampigia mtu huyo namshangaa
   
 9. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #9
  Aug 19, 2015
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,160
  Likes Received: 522
  Trophy Points: 280
  Mtoa mada amewauliza nyinyi ccm ushahidi wa kuwa Lowasa alikula pesa za richmond uko wapi na ni kiasi gani? Usituletee porojo hapa wee dada
   
 10. rallphryder

  rallphryder JF-Expert Member

  #10
  Aug 19, 2015
  Joined: Jan 24, 2015
  Messages: 3,135
  Likes Received: 505
  Trophy Points: 280
  Hivi yuko mtu mwenye akili timamu atakayempigia kura fisadi na kumuacha mtu muadilifu kama Magufuli kweli!?
   
 11. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #11
  Aug 19, 2015
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,160
  Likes Received: 522
  Trophy Points: 280
  Acha porojo njoo na ushahidi kwamba Lowasa kaiba kiasi fulani kwenye richmond kama huna kaa kimya mnajiabisha mbele ya umma. Lowasa alisema kilichotokea ikulu na ccm imekaa kimya halafu wewe unaleta porojo tu utakuwa na akili kweli!?
   
 12. P

  Pohamba JF-Expert Member

  #12
  Aug 19, 2015
  Joined: Jun 2, 2015
  Messages: 16,259
  Likes Received: 25,166
  Trophy Points: 280
  Mi nashauri Uchunguzi ufanyike kwn Hicho kipimo cha Akili kabla ya kupima Akili zenyewe
   
 13. m

  mendz Senior Member

  #13
  Aug 19, 2015
  Joined: Dec 9, 2013
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama ni kweli alikuwa hana maadili ina maana aliiba. Kwa nini Serikali iliyokuwa na ushahidi wote wa wizi wake isimburute mahakamani akaozee jela na hela ya umma irudi?

  Kushindwa kwa Serikali kumburuta mwizi mahakamani ni wazi kwamba Serikali nayo ni wezi kwani huwezi kumuacha mwizi wa mali ya umma anatanua mitaani na hela ya wizi wa mabilioni bila kuchukua hatua yoyote.

  Sasa kama wewe una akili timamu utawezaje kumpigia kura mgombea aliyewekwa na Serikali hiyo hiyo ya wezi?

  Ndio maana nasema atakayempigia kura Magufuli basi atakuwa ama yeye mwenyewe mwizi wa mali ya umma au anastahili kupelekwa Mirembe.
   
 14. m

  mendz Senior Member

  #14
  Aug 19, 2015
  Joined: Dec 9, 2013
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usizungumze kama mtoto mdogo. Sio lazima uchangie. Kama unataka kuchangia njoo na hoja dhidi ya hoja zangu.
   
 15. m

  mendz Senior Member

  #15
  Aug 19, 2015
  Joined: Dec 9, 2013
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ungekuwa uko timamu ungekuja na hoja dhidi ya hoja zangu.
   
 16. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #16
  Aug 19, 2015
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,605
  Likes Received: 5,492
  Trophy Points: 280
  Lowassa, Ukawa watashinda zaidi ya 83%

  MAGUFULI, CCM... 16%....

  MTASHANGAAA OCTOBER...

  Ndio mkome kutukana wananchi..na kudharau maskini wa nchi hii...!!!
   
 17. amos pastory

  amos pastory Member

  #17
  Aug 19, 2015
  Joined: Aug 14, 2015
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Magufuri atashida kwa kura nyigi sana
   
 18. J

  Jang Bo Go JF-Expert Member

  #18
  Aug 19, 2015
  Joined: Oct 22, 2011
  Messages: 852
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  hao 75% wakapimwe akili
   
 19. m

  mendz Senior Member

  #19
  Aug 19, 2015
  Joined: Dec 9, 2013
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna kila dalili kwamba mlimtumia Slaa kumpa ushahidi wa uwongo dhidi ya Lowassa na mlikuwa mnamtumia kwa maslahi yenu akiwa kama kibaraka wenu ndani ya CHADEMA.

  Kama kweli Slaa ana akili timamu kwa nini asusie kiasi hicho ujaji wa Lowassa wakati Lowassa ameshasema yeye hausiki na mwenye ushahidi apeleke mahakamani? Kwa nini Slaa asipeleke ushahidi alionao mahakamani au asiwabane wale waliompatia huo ushahidi kumburuta Lowassa mahakamani badala yake anakimbilia kumsusia Lowassa?

  Sasa suala la wizi wa Magufuli liko wazi kama lilivyoanishwa na CAG. Huwezi kutunga mradi hewa wa mabilioni na ukaupatia namba hewa kama wewe sio mwizi uliyekubuhu.
   
 20. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #20
  Aug 19, 2015
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,673
  Likes Received: 521
  Trophy Points: 280
  Japo mie sio mwana ccm lakini kaka naona kwa mawazo haya ni kama unajitekenya mwenyewe.

  Inshort ni kuwa watanzania tunataka Transformation na sio Changes.

  Siku vyama vya upinzani vikijivunja na wote kuchanachana kadi zao na kuanzisha chama kimoja tu cha upinzani chenye sera na nia moja basi ujue hapo ndipo tutakapoiweza kuitoa ccm. Otherwise jua Lowasa kaja kuuwa nguvu ya upinzani. Na amekuwa akiwakatisha tamaa lakini hamjayaelewa maneno yake subirini Nov mtakavyogawana mbao
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...