Hivi kuna mtu mwenye akili timamu atakayempigia kura yake Magufuli na kumuacha Lowassa? | Page 4 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kuna mtu mwenye akili timamu atakayempigia kura yake Magufuli na kumuacha Lowassa?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by mendz, Aug 19, 2015.

 1. m

  mendz Senior Member

  #1
  Aug 19, 2015
  Joined: Dec 9, 2013
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nauliza swali hilo kwa kigezo kimoja tu nacho ni wizi wa mali ya umma.

  Lowassa anatuhumiwa kwenye wizi wa Richmond bila ushahidi wowote ule mpaka sasa. Wanaomtuhumu ni walewale ambao wanaoweza kuwa na ushahidi ambao kama kweli alikwapua basi walitakiwa wawe wameshamburuta mahakamani tangu wakati ushahidi ulipopatikana kama kweli wanauchukia wizi wa mali ya umma na kama kweli wao wenyewe sio wezi.

  Magufuli sio tu anatuhumiwa bali kuna ushahidi wa kitaalam uliotolewa na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) ukimuhusisha na taarifa za uongo za kudai mabilioni ya pesa yametumika kujenga barabara wakati sio hivyo. Ni wazi kwamba Magufuli kakwapua hizo hela na hivyo HAFAI KUKAA IKULU HATA SEKUNDE MOJA.

  Sasa jiulizeni hivi CCM imeshindwa kuja na mgombea wake ambaye sio mwizi? Kwa nini waweke mgombea ambaye ni mwizi kama wao wenyewe sio wezi?

  Kifupi ni kwamba Magufuli atapigiwa kura tu na wezi wenzake wanaoliibia taifa hili usiku na mchana bila kunawa na hivyo kulifanya taifa hili lenye rasilimali lukuki kuendelea kuwa taifa masikini.

  Watanzania wote wenye uchungu na nchi yao kama wamepewa kuchagua wa kumpigia kura kati ya mtu anayetuhumiwa tu bila ushahidi wowote na ambaye ameshathibitishwa kwamba ni mwizi na taasisi maalum yenye utaalamu kuhusu uthibitishaji huo basi watapiga kura kwa yule ambaye hajathibitishwa kwamba ni mwizi.

  Je wewe kura yako iko kwa nani kati ya hawa wawili?
   
 2. C

  CHAZA JF-Expert Member

  #61
  Aug 20, 2015
  Joined: Dec 21, 2012
  Messages: 6,795
  Likes Received: 2,255
  Trophy Points: 280
  Hata wale Team ya Ushindi si umeona majina yaleyale ya mfumo uleule. Kwa lugha nyingine pamoja na ukweli kwamba Dr Magufuli ni jembe, sioni namna bora atautosa mfumo ambao tayari umeshaundwa! Akitaka afanikiwe awatose na afanye mambo yake. Haki ya Mungu akitoa fadhila tu ndo mwanzo wa yeye kuyumba( hii ni endapo Magufuli akishinda). Anatakiwa awe bandidu kama Rais wa Malawi au Zambia kama sikosei. Wale wote wa chama chake aliwatosa akaunda team mpya. Hivyo washauri wa Magufuli kama akishinda na kuendelea kukumbatia watu walewale, atakuja kushangaa analaumiwa tu.
  Hata huyu mheshimiwa anaemaliz muda wake wanamtandao ndiyo wamechangia kumpotosha na kumyumbisha kuja kushangaa madudu lukuki!
   
 3. NDAGLA

  NDAGLA JF-Expert Member

  #62
  Aug 20, 2015
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 2,492
  Likes Received: 349
  Trophy Points: 180
  TUNAENDELEA. Hili ndo jibu pekee nililohitaji the rest was simply inconsequential.

  Kumbe ni watuhumiwa tu? Toka lini mmegundua kuwa ni watuhumiwa na siyo mafisadi kama mlivyokuwa mnaimba?

  Sasa rudini pale pale Mwembeyanga mkayaseme haya mtupe na sababu ni kwa nini mliamua kutudanganya na kwa manufaa ya nani.

  Na kama mlitudanganya basi mtushawisi upya kwamba mtakachotuambia tena hakitakuwa uongo otherwise tuwapuuze milele.

  Hivi wewe mtu akikuambia tu hahusiki halafu anakutajia mtu mwingine bila hata kuweka ushahidi wowote unakubali?

  Unakuwa una akili kweli?

  Halafu ni wapi alimtaja Kikwete kama mhusika? Weka clips kama unazo.

  Alichokisema ni mamlaka za juu na kwa sisi walokole hakuna mamlaka za juu duniani instead iko mbinguni tu.

  Sasa kama hakukubaliana na hiyo mamlaka kwa nini hakuachia ngazi?

  Twende taratibu.
   
 4. m

  mendz Senior Member

  #63
  Aug 20, 2015
  Joined: Dec 9, 2013
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa una quote post yangu halafu unaweka utumbo huu ambao hata hauhusiani na points zilizopo kwenye post yangu!!! Jibu hoja au kaa kimya. Anzisha thread yako upost huo utumbo wako.

  Hapa tunajadili masuala nyeti ya mustakabali wa taifa letu na kuweka hoja kwa nini Magufuli HAFAI KUINGIA IKULU HATA SEKUNDE MOJA. Jibu hoja hizo kama unataka kuchangia kwenye post hii.
   
 5. barafuyamoto

  barafuyamoto JF-Expert Member

  #64
  Aug 20, 2015
  Joined: Jul 26, 2014
  Messages: 24,343
  Likes Received: 16,396
  Trophy Points: 280
  Magufuli mwiziiii?????
  Sababu kama hizi ndo zanifanya nione watu ni wanafiki na hawana hoja! Lowasa na magufuli ni nani anayesemekana ni mwizi??
   
 6. L

  Lenatuschacha Senior Member

  #65
  Aug 20, 2015
  Joined: Jul 29, 2015
  Messages: 153
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  ukawa mbele kwa mbele
   
 7. barafuyamoto

  barafuyamoto JF-Expert Member

  #66
  Aug 20, 2015
  Joined: Jul 26, 2014
  Messages: 24,343
  Likes Received: 16,396
  Trophy Points: 280
  Ukweli ni kwamba Lowassa atamletea Magufuli upinzani mkali, ila Magufuli ataibuka kidedea! Ukweli ni mchungu kwa watu ila ndo ukweli wenyewe huo!
   
 8. Mavipunda

  Mavipunda JF-Expert Member

  #67
  Aug 20, 2015
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 4,796
  Likes Received: 3,560
  Trophy Points: 280
  Lowasa gonjwa gonjwa
   
 9. m

  mendz Senior Member

  #68
  Aug 20, 2015
  Joined: Dec 9, 2013
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usiwe na wasiwasi. Tutaenda taratibu.

  Kwa nini majina yale yalitajwa pale Mwembeyanga kama mafisadi? Ili vyombo vya sheria viweze kuwashughulikia na hivyo kuthibitisha au kutothibitisha ufisadi wao. Kwa nini vyombo vya sheria havikufanya hivyo wakati mabilioni ya pesa yalishathibitishwa kwamba yamepotea na kilichokuwa kimebaki ni kuthibitisha nani aliyeingia nayo mitini? Ni kwa sababu Serikali ya CCM haikuwa na nia ya kuliona suala hilo linaenda mahakamani kwa sababu wanafahamu kwamba wezi ni wao wenyewe Serikali.

  Sasa suala la mamlaka ya juu kwa mazingira yale ya aliyokuwa anayasemea Lowassa akiwa kama Waziri Mkuu ni lazima iwe ofisi ya Rais. Ndio mamlaka ya juu ya Waziri Mkuu. Hayo ya mbinguni sioni mantiki yoyote ya kuyaingiza hapa kwani tunazungumzia mambo ya wanasiasa na sio viongozi wa dini.

  Suala la kuachia ngazi ni suala jingine tofauti kabisa ambalo haliingiani na maudhui ya post yangu ambayo inaonyesha jinsi Magufuli alivyokuwa mwizi aliyekubuhu kwa kuiba hela za walipa kodi kwa kutunga mradi wa uwongo bila haya, wizi ambao umethibitishwa na CAG.

  Lakini sio kila siku mtu unaachia ngazi kama hukubaliani na mamlaka fulani kwani wakati mwingine unapoteza fursa ya kuweza kupata nafasi ya kufikia kwenye ngazi hiyo usiyokubaliana nayo ili uweze kupata fursa ya kurekebisha yale ambayo uliyoyaona ni mabaya. Ndicho alichokifanya Lowassa. Akaamua kukaa kimya na baadaye akakubali kujiuzulu baada ya kushinikizwa kufanya hivyo ili asipoteze nafasi yake ndani ya chama ya kurudi tena na kugombea nafasi ya juu ndani ya chama chake ambacho amechangia mno kukijenga tangu ujana wake.

  Sasa na wewe tueleze. Kama yeye ndie alihusika katika wizi ule wa Richmond, kwa nini Kikwete hakumburuta mahakamani ili arejeshe hela za walipa kodi pamoja na kutumikia kifungo kinachoendana na kosa lake la wizi wa mali ya umma na badala yake ameamua kutumia hiyo issue ya Richmond kama karata ya CCM ya kumuengua Lowassa kwenye kinyan'ganyiro cha Urais kwa kumpachika majina ya fisadi, asiye na maadili, n.k.?
   
 10. Queen Esther

  Queen Esther JF-Expert Member

  #69
  Aug 20, 2015
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,707
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Siku nitakapomsikia Dr. Slaa akimsafisha mamvi ndio nitaelewa hichi ulichoandika.

  Queen Esther

   
 11. Usher-smith

  Usher-smith JF-Expert Member

  #70
  Aug 20, 2015
  Joined: Jul 7, 2015
  Messages: 6,280
  Likes Received: 5,093
  Trophy Points: 280
  We hujui demokrasia
   
 12. Jerry santonga

  Jerry santonga JF-Expert Member

  #71
  Aug 20, 2015
  Joined: Oct 12, 2014
  Messages: 554
  Likes Received: 385
  Trophy Points: 80
  Low hasa atopata kabisa kura yangu
  Vigezo
  1.Afya mbovu
  2.sio mwadilifu
  3.tamaa ya madaraka
  4.mbadhilifu
  5.anatumia pesa kununua wapga kura
  Gud example ni chuoni kwe2 udom tumegegeda hela zake nimenunua plate 2 za jiko la gesi na samsung oven,hvyo
  HAFAI ATABAKI KUWA LOW TENA HASA
   
 13. Dan Zwangendaba

  Dan Zwangendaba JF-Expert Member

  #72
  Aug 20, 2015
  Joined: Apr 25, 2014
  Messages: 2,054
  Likes Received: 1,929
  Trophy Points: 280
  Naona kama swali liko kinyume. Nadhani wa kupimwa akili ni atakayempigia Lowasa mtu ambaye Chadema walihifadhi ushahidi wa ufisadi wake kwa miaka 8 lkn wakamsafisha kwa wiki moja na kubadili agenda eti ni "mfumo". Mfumo ni nini kama sio lowasa, mbowe na mtei nk? (WATU).
   
 14. M

  Mahnaim Member

  #73
  Aug 20, 2015
  Joined: Mar 10, 2015
  Messages: 91
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lowassa mpango wa Mungu lazima aingie IKULU mwaka huu mtake msitake wajinga wakubwa mnaongelea mambo ya wizi cha muhimu ni mabadolilo team UKAWA ndio watakaoendesha nchi wamemtumia EL kuoondoa ccm madarakani na hakuna atatayezuia mabadiloko haya mambo ya afya peleka hayahusiani na maendelea ya nchi hii kama hamtaki mabadiliko mkale malimao na mafisadi wenu ccm watesi na waonevu wakubwa.
   
 15. Sharif

  Sharif JF-Expert Member

  #74
  Aug 20, 2015
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 2,466
  Likes Received: 1,660
  Trophy Points: 280
  mimi bahati mbaya si mhafidhina..
  si muoga wa mabadiliko..
  ukiona mke miaka 50 anakuzalia vichaa na magoigoi..
  usiogope kujaribu mke mwengine..
  huenda ukapata magenious na hata usipopata..
  you have made a progress in an adventure where a step forward is more meaningful.
   
 16. m

  mendz Senior Member

  #75
  Aug 21, 2015
  Joined: Dec 9, 2013
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku hizi hakuna shule. Vijana mnaingia tu madarasani kutimiza wajibu. Sasa hapo unajibu hoja yangu au unajaza tu server.
   
 17. m

  mendz Senior Member

  #76
  Aug 21, 2015
  Joined: Dec 9, 2013
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama ushahidi ulikuwepo kwa nini Serikali isimburute mahakamani? Mbona mnashindwa kujibu swali rahisi sana? Hela zile zimeibiwa Serikalini zikiwa hela za walipa kodi. Anayetakiwa kuwa na uchungu wa wizi ule kwanza ni Serikali kwa sababu yenyewe ndio imepewa dhamana ya kulinda na kutumia vyema kodi za wananchi. Sasa iweje wamuache Lowassa apete na hela za wizi wa mali ya umma mtaani kipindi chote hicho mpaka leo?

  Mimi sijadili CHADEMA hapa wala CCM. Nawajadili watu wawili ambao ni Lowassa na Magufuli ni nani mwenye afadhali kulinganisha na mwingine. Na nimeelezea jinsi wizi wa Magufuli ulivyo wazi na wenye vithibitisho ukilinganisha na tuhuma kwa Lowassa.

  Sasa hii ndio hoja inayotawala post yangu hii na wanaojikita kwenye post hii waji confine kwenye boundaries za theme ya post hii na si vinginevyo.
   
 18. undugukazi

  undugukazi JF-Expert Member

  #77
  Aug 21, 2015
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 307
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Ubaya wa watu wa ukawa muchknow sana. Yani wanajua kila kitu na wakisema nyoka ni mbuzi basi mkubali tu. Acha kilatu apige kura yake kwa yule anaempenda yeye sio kujifanya unajua sana kujaji mambo.
   
 19. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #78
  Aug 21, 2015
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 6,241
  Likes Received: 1,198
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 20. Kirikou Wa Kwanza

  Kirikou Wa Kwanza JF-Expert Member

  #79
  Aug 21, 2015
  Joined: May 24, 2013
  Messages: 3,137
  Likes Received: 981
  Trophy Points: 280
  Sifikirii kama kuna mtanzania yeyote mwenye akili timamu anaweza kumpigia kura fisadi Lowassa ambae kwa zaidi ya miaka 8 amekuwa akipewa tuhuma za ufisadi na viongozi ambao walituaminisha kuwa ni fisadi halafu leo kwa miezi mitatu tu wanataka kutuaminisha kuwa fisadi Lowassa ni mtu safi. Kwa kweli watanzania hasa wale wazalendo tunataka mabadiliko, lakini si haya ya kununuliwa na mafisadi tunaowajua kwa zaidi ya miaka 8 na kujaribu kuwasafisha kwa miezi 3.
   
 21. Kirikou Wa Kwanza

  Kirikou Wa Kwanza JF-Expert Member

  #80
  Aug 21, 2015
  Joined: May 24, 2013
  Messages: 3,137
  Likes Received: 981
  Trophy Points: 280
  Unauliza kushtakiwa kwa Lowassa? Teh teh teh Butiku ameshawajibu hilo swali, acheni kushabikia ujinga hiv kumbe huwa mnabwabwaja tu humu JF bila kufatilia haya mambo kwa kina.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...