Hivi kuna maisha baada ya kifo?

Baada ya kufikiria hili jambo nimekuja na conclusion ifuatayo; As far as the onlookers are concerned we are just identities (labels) Jon Doe akiwa na miezi 2 (miaka sifuri); akiwa 20; na akiwa na miaka mia moja Ni nani ambaye ni Huyo Jon Doe; sababu hata memories huenda at 100 akawa hana hizo memory na akawa ni dubwasha tu kama alivyokuwa akiwa na miezi 2; and absolutely nothing is the same as he was at his childhood...

Pili identity inategemea muda unaokaa na zile features (Hata mashati fulani tuliya-identify kwamba ni mashati ya Mandela) au hio Ship huenda ule mlingoti uliowekwa at year 50 kwa miaka mingine hamsini watu wali-identify na huo mlingoti ingawa huenda at year 10 hata huo mlingoti haukuwepo...

Thus we are just Identities / labels as far as onlookers are concerned; As far as we are we are concerned we are who we are at that particular age (childhood, teens, adulthood or old age)
But I am not talking about identities or labels, neither the ones given by others nor self identified.

Obama anaitwa black, yeye anajiita black, but he is actually biracial. Mama yake mzungu.
 
Mwaka jana mwishoni kuna chuo kimeanzishwa ujerumani Kinachohusu mambo haya ya uchawi.

Uchawi ni neno kama ambavyo na wewe kwenye akili yako umeweka neno linaloitwa sayansi,
Na kila moja inaelezea kwa namna yake inavyofanya kazi.


Huyu anaeamini/kujua kuhusu uchawi peke yake akikwambia haijui sayansi wala haitambui sayansi anakosea ?
Hilo neno "uchawi" linamaanisha nini?

Neno unaweza kutunga tu hata wewe, lisiwe na maana, kitu muhimu ni maana.

Mtu akisema haijui sayansi, labda haijui tu, sasa anakosea nini kama haijui? Sayansi kuwa kweli haitegemei mtu kuijua.

Huo uchawi ni nini?

Tumeiangalia definition ya uchawi kama mambo yaliyo nje ya sheria za fizikia, tukaiona definition hii imepwaya, kwa sababu hata hizo sheria za fizikia hatuzijui vizuri, sasa tutasemaje hiki kipo ndani ya sheria za fizikia, na hiki kipo nje, wakati kinaweza kuwa ndani ya sheria za fizikia ila sisi hatujazijua tu?

Kwa nini tunasema "huu ni uchawi, ni kitu kilicho nje ya sheria za fizikia" badala ya kusema "inawezekana huu si uchawi, hauko nje ya sheria za fizikia, bali sisi ndiyo hatujazielewa vizuri tu sheria za fizikia, hapa inabidi tuchunguze vizuri zaidi"?.

Katika mfano wa kilichoripotiwa kuwa uchawi huko Mombasa, niliouweka hapo juu, Polisi walitumia hiyo option ya pili walipoona watu wanacheza uchi, wakakuta ushahidi kwenye CCTV kuwa hakuna uchawi hapo, ni mioango ya watu tu kuhadaa umma.

Sass, kwa nini tunakimbilia kusema huu ni uchawi badala ya kuchunguza?
 
Ukifa unaoza unakuwa mbolea ya mimea / hayo mafuta na nishati kadhaa almasi n.k. ni viumbe vilivyokufa zamani...

Kabla haujaziliwa ulikuwa haupo chanzo chako ni mbegu ni kama vile unashangaa huu muindi umetoka wapi wakati ulipanda mbegu / indi
Mbegu imetokea wapi?

Sasa kama nishati hutokea kwenye mazali ya viumbe, basi inamaana mtu akifa anaenda ku exist in another form of life
 
Wafia dini washauharibu huu uzi.

Uzi ulitakiwa kujibiwa kwa facts na vithibitisho vinavyomake sense visivyoegemea upande wa dini wala imani yoyote.

Vithibitisho vya kweli sikuzote havichagui hali yako ya kiimani wala rangi yako, facts ni facts tu, wanaothibitisha kwa kutumia biblia na quran na kuconclude kuwa jambo liko hivi au vile hawa ni waongo wakubwa, maana vitabu vyao haviwezi hata kujithibitisha vyenyewe ukweli wa maandiko yao yanayopingana.

Ukifa umekufa, subiri huko huko ndiko utajua kama kuna linakofuata, tusiaminishane uongo hapa maana hakuna aliyewai kufa akarudi na kuleta ushahidi wa aliyoyaona, hivyo basi hizi nadharia za maisha baada ya kifo ni porojo na stories za kuwadanganya watu wasi enjoy maisha ya dunia kwa kutegemea maisha mengine ambayo kiuhalisia hayapo na hayatokuwepo.
 
Habari wana JF,

Hivi kuna maisha baada ya kifo?
Au bado sijui maana ya kifo?
Yaani babu yangu liyemzaa bibi yangu bado anaishi baada ya kufa? Kwamba hawa waliokufa wanaishi ila waneshakufa?

Au naombeni maana ya kifo ili ning'amue huu mzozo.

(Kuna mtu kaniambia kuwa kuna maisha baada ya kufa)
sasa naww kwani amuaminiani na uyo shogako adi uje uku kuuliza kitu kilekile ?
 
umezungumza sawia kabisa mwili sasa huyo mtu yuko wapi kama mwili wake unaenda kushambuliwa na bakteria huko ardhini.
na hata ukifa leo tutasema mwili wa marehemu ila bado ww hatutakutaja hapo uko wapi?
Msingi wa Swali lako hauna maana yoyote ile

Kukosa huko maana kunasababishwa na kutoelewa vitu kadhaa, ikiwemo

Mtu ni nini

Mwili wa marehemu ni nini

Je waweza kunijibu maswali haya ili tuelewane?
 
Kumbe ulikua na jibu lako tayari, Ulileta mada ya nini sasa
Jibu gani nilikuwa nalo sijakuelewa, na sio kila anaeleta mada hapa hana majibu au ana majibu kuna wengine wana majibu ambayo hayawaridhishi kuna wengine hawana majibu kabisa
 
Mbegu imetokea wapi?
Kabla ya yote hivi unajua kwamba nothingness haipo yaani hakuna kitu kama nothingness kukuwa na volume basi lazima kuna vitu ndani yake; hata leo ukiweka chupa tupu kwa macho yako ifunge kabisa kama kuna favorable conditions utakuta kuna life forms humo ndani.... Kwahio utaona kwamba with favorable conditions unicellular can become multicellular....

Sasa kama nishati hutokea kwenye mazali ya viumbe, basi inamaana mtu akifa anaenda ku exist in another form of life
nimeongelea nishati as in petrol and gas kwamba hii petroleum sio kwamba Mungu aliweka ni life forms zilizokufa miaka na miaka hata Biogas ni kwamba vitu vikioza sio kwamba vyote vinakuwa Biogas; bali kuna gesi inapatikana kutokana waste ambayo inatokea wakati bacteria wanachakata hayo masalia (unaongelea life form kwahio unamaanisha petroli au almasi inaishi )?
 
HABARI DRACE GLORY, NAKUSHUKURU SANA KWA KUULIZA SWALI HILI KWA KWELI JIBU LA SWALI HILI NDILO LITAKALOKUFANYA UJUE UISHI VIPI HAPA DUNIANI. MAJIBU MENGI YA WALIOKUJIBU HAPO JUU WAMEKOSEA NA HUTAPATA MAJIBU SAHIHI KWA MUELEKEO WA MAJIBU NILIYOYAONA BALI UTAPATA MKANGANYIKO ZAIDI.

UKWELI USIO NA SHAKA NI KUWA MAISHA BAADA YA KUFA NI JAMBO LISILOKUWA NA SHAKA YEYOTE. MAISHA HAYO BAADA YA KIFO NI BORA NA YENYE KUDUMU. HILI LINATHIBITISHWA NA KITABU KITAKATIFU CHA QURANI AMBACHO MPAKA SASA WAPINGAJI HAWAJAWEZA KUINGIZA MANENO YAO. QURANI INASEMA:
{ وَٱلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ وَأَبۡقَىٰٓ }

[Surah Al-Aʿlā: 17]

Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi.


IN SHAA ALLAH JIBU HILI LITAKUWA USHAHIDI SIKU YA MWISHO KUWA NIMEFIKISHA NENO LA ALLAH KWA WAJE WAKE. NAKUHUSIA HALA HALA USISIKIE MANENO YA WATU WAPOTEFU...GRACE USIJE UKAFA KABLA HUJAWA MUISLAMU.
Kwamba quran ni kitabu kitakatifu?
 
Wewe ulipouliza kama kuna maisha baada ya kifo ulimaanisha nini?
Nilimaanisha kuwa kuna maisha baada ya kifo ? Na ndivyo ulivyojibu (ndio) na kutoa tafsiri yakwanini umesema ndio, sasa hapo hata ungejibu hapana bado ningekudai sababu za kusema hapana.
Umenielewa mr Kiranga ?
 
HABARI DRACE GLORY, NAKUSHUKURU SANA KWA KUULIZA SWALI HILI KWA KWELI JIBU LA SWALI HILI NDILO LITAKALOKUFANYA UJUE UISHI VIPI HAPA DUNIANI. MAJIBU MENGI YA WALIOKUJIBU HAPO JUU WAMEKOSEA NA HUTAPATA MAJIBU SAHIHI KWA MUELEKEO WA MAJIBU NILIYOYAONA BALI UTAPATA MKANGANYIKO ZAIDI.

UKWELI USIO NA SHAKA NI KUWA MAISHA BAADA YA KUFA NI JAMBO LISILOKUWA NA SHAKA YEYOTE. MAISHA HAYO BAADA YA KIFO NI BORA NA YENYE KUDUMU. HILI LINATHIBITISHWA NA KITABU KITAKATIFU CHA QURANI AMBACHO MPAKA SASA WAPINGAJI HAWAJAWEZA KUINGIZA MANENO YAO. QURANI INASEMA:
{ وَٱلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ وَأَبۡقَىٰٓ }

[Surah Al-Aʿlā: 17]

Na Akhera ni bora na yenye kudumu zaidi.


IN SHAA ALLAH JIBU HILI LITAKUWA USHAHIDI SIKU YA MWISHO KUWA NIMEFIKISHA NENO LA ALLAH KWA WAJE WAKE. NAKUHUSIA HALA HALA USISIKIE MANENO YA WATU WAPOTEFU...GRACE USIJE UKAFA KABLA HUJAWA MUISLAMU.
Nashukuru kwa jibu lako murua kabisa , nahitaji kujua maana ya kufa/kifo ni ipi?
 
Mkuu, hoja ya kuishi baada ya kufa imekaa kiimani zaidi.Kama huamini hivyo ni sawa Hakuna kuishi baada ya kifo. Lakini kama unaamini, basi jibu ni Ndio kuna maisha baada ya kifo.
Maana ya kufa ni pale Kitendo cha mwili kutengana na Roho iliyo ndani mwako. Ni pale mwili wako unapotwaa hali ya Umauti. Baada ya Umauti watu wenzako wanakufukia ardhini (wanakuzika) kwani huna tena maslahi/faida kwao. Mwili wako ni maiti na punde utaingia katika mchakato wa kuyarudia mavumbi(utaoza).
Roho sio kiumbe bali ni Nafsi hai au unaweza kusema roho ndiyo UZIMA.
Mkuu, Uzima ni sifa (kivumishi)

Hivyo unaposema roho ndiyo uzima ni sawa, lakini ukidai uzima huo (roho) ndiyo unaenda mahali pengine baada ya kufa, unakuwa unafanya makosa makubwa.

Yaani hauna tofauti na mimi kukuiliza kuwa mtoto anapokuwa mdogo anakuwa mfupi, akifikisha miaka 40 huo ufupi unaenda wapi?

Kwahyo naweza sema habari ya roho ina utata mkubwa, na utata huo ni kwasababu tu roho hiyo haipo katika uhalisia.
 
Mkuu, sio lazima uone kila kitu ili uamini kipo. Hivi (kwa utani lakini) unapoongea na simu unaamini kwamba huyo unayeongea naye ndiye kweli yeye?
Kwa habari za roho mm naamini ipo kutokana na matendo yake yanayoonekana. e.g. Umewahi kujiuliza hivi Wale watoto /wanafunzi wanaokimbia-kimbia na kupagawa wanaona au wanasikia nini hadi wafanye hivyo? Nina hakika Umewahi kusikia mara nyingi watu wakisema ''Aisee, Huyo jamaa ana roho mbaya sana kaa naye mabali" Je, kwa nini wasiseme ana moyo mbaya? Hiyo roho wanamaanisha waliionaje/nini? hata wakaithaminisha (grade) kuwa ni mbaya?
Wewe kama ni mtu wa imani Mkristo, soma Math 15:18-20 i.e. "kile" kilicho ndani ya mtu kinajidhihirisha kwa matendo tunayoyaona kwa macho yetu kama ushuhuda.
Mkuu, inawezekana kabisa ninaunda dhana za kufikirika (Imaginations) lakini mm ninaamini sio mtu wa kwanza kukubali kwamba kuna kitu kinaitwa Roho.
Je mm ni mjanja kuliko hao wengine? Kila mtu anaweza kuamini kile anachoona ni sahihi au ni cha ukweli kwake.
Asante.
Usikamatwe na mtego wa lugha.

Lugha ya kiswahili ni finyu sana.

Ili tutafute usahihi na umaana wa kitu kwa sauti moja kama walimwengu pasina kubase jamii tulizokulia,
Unaweza kuniambia kwa kiingereza hiyo kauli ya kwamba "una roho mbaya" ? Ili tuijadili hapa
 
Usikamatwe na mtego wa lugha.

Lugha ya kiswahili ni finyu sana.

Ili tutafute usahihi na umaana wa kitu kwa sauti moja kama walimwengu pasina kubase jamii tulizokulia,
Unaweza kuniambia kwa kiingereza hiyo kauli ya kwamba "una roho mbaya" ? Ili tuijadili hapa
Evil behavour
 
Hii Kwa wasioamini dini(wazee wa logic and seenable things)
💥Kama umezaliwa hukuwa unajua utaish ,vip useme hamna maisha baada ya kifo ,we unatakiwa useme tu sijui maana ukisema hamna maisha manake ushajua na una elimu ingali hujakufa ukafika huko ukapata experience.
Na usijiaminishee unajua kila ktu Mana Kuna vtu vingi tu vimewashinda mfano mpak leo hamuwez hta kutibu vidonda vya tumbo kwa logic zenu kazi tu kutupa miji-antiacid,cancer imewashinda pia manake kumbe mna upungufu wa elimu .so atheist mkiulizwa kuhusu kifo mjibu hamjui.
Unaelewa hata maana ya kifo?

Kwanini unataka kuwepo na maisha ilihali umeshakufa?
Wenye Imani zetu(mnaotukebehi mkatuita wafia dini).
Tunaamini maisha yapo kwa kutumia mitume na vitabu ambavyo vimeshushwa kutupa muongozo.
Mfano waislamu sisi Tuamini hivi kuhusu kifo:
a)siku yako ya kufa watakuja malaika wengne watasimama kulia kwako na kushoto kwako haf Yule anaetoa roho atasimama sehemu ya kichwa ataamuru roho itoke na ikitoka wale malaika wengne wataichukua na kuivisha vazi flani (halijulikan namna yake) Kisha watapaa na roho kuelekea mbinguni.
b)kwa sisi waislamu mbigu zpo tabaka Saba ,so watapaa kuelekea tabaka la Saba kuipeleke hyo roho ambapo Kuna vtabu viwil Cha watu wema na waovu,na kila mbigu Ina malaika ambapo roho inapokuwa inapitishwa huulizana Ni Nani (baadhi ya malaika watakutaja kwa jina lako ulokuwa waitwa duniani)Mana lile vazi roho huvishwa huwa na harufu mbaya kwa muovu na nzuri kwa mwema.
C)Kama Ni mwema roho huenda mpak tabaka la Saba na huuandikwa kweny ktabu kinaitwa "iliyyin" ktabu ambacho huuandikwa watu wema tuu. Kama muovu huishia mbigu ya kwanza tu na hutupwa ardhini Mana Allah ameahid milango ya mbigu haitofunguliwa kwa watu waovu(mbigu kiimani Zina milango Ila haimanishi Kama hii ya nyumbani Yani Ni jina tu lakushabihisha,NB:vtu vyote ambavyo vpo baada ya kufa havifanan na hivi vyetu Ila Ni majina tu ili tuelewe Mana hakuna aliyewahi viona kwa macho). kwahyo muovu ataandkwa kweny ktabu Cha waovu kinachoitwa "sijjin".
c)uwe muovu au mwema wote roho zao ztarudishwa ardhini kweny miili yao baad ya kuzikwa Mana Allah katika suratul-twaha amesema "kutokana na hyo ardhi tmuekuumbeni(Yani adamu Mana ya ndo wa kwanza na asili yetu) na humo tutakurejesheni na tutakutoeni kwa Mara nyengne Tena (ufufuo)".
Roho zikirudishwa Kuna malaika watakuja kaburini kukuuliza maswali matatu tuu 1.Nani mola wako 2.Muhammad Ni Nani 3.umemjuaje Muhammad.
d)Kama Ni mwema,atajibu maswali yote na atakapoulizwa amemjuaje Muhammad atasema alisoma Quran.
Hvyo malaika watamuonyesha Moto aloambiwa na pepo aloahidiwa na Yale matendo mema alofanya duniani yatamjia Ni Kama kiumbe flani umbile la binadamu ,Yani kitaumbwa kiumbe kibinadamu lakini Ni matendo yake mema ili kumfariji yeye na upweke. Basi mtu mwema ataomba kiama kisimame mana ameona mambo yote na yey Ni katika walofaulu ili alipwe pepo yake.
d) Kama Ni muovu atashindwa kujibu maswali Mana atapatwa na uoga na haya maswali hujibu kwa ujanja Bali vle we ni muovu au mwema tu, akiulizwa kuhusu Muhammad atasema alikuwa anaskia watu wakisema Yani hamjui ,hvyo malaika watamuadhibu vikali , na Kuna adhabu mbalimbali Kama Kuna majoka ambayo Kama sumu yake itafika ardhini hakuna mmea utaota na Ni wakubwa wanatisha na matendo yake maovu yataubwa kuwa kiumbe kitakacho muadhibu ,na ataomba kiama kisisimame Mana atonyeshwa Moto na utafunguliwa milango yake hivyo joto lake na mrindimo wake utamfikia.
💥Haya maisha ya Kaburini yanaitwa maisha ya barzakh na Ni endelevu mpak siku ya hukumu.
NB: 1.maelezo Ni marefu nkipata mda ntaandika Uzi wa maisha ya milele kulingana na Imani yangu Mimi inshallah.
2.namsikitikia mtu anaye tarajia kufa haamini chochote manake anakufa Kama mnyama ambaye Hana akili ya kufikirii , hajipangii future yake anasubir future impangie.
Mitume na manaabii + vitabu hivyo unavyoviamini, je ni vya kweli..??

Ukigundua kama haabari za manabii, mitume na vitabu hivyo ulivyodanganywa kwamba vimeteremshwa kutoka sehemu isiyopo (mbinguni) ni za uongo na zimejaa migongano ya wazi kabisa utaendelea kusema kuna maisha mengine baada ya kufa?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom